Daktari wa Kichina afariki akimuokoa mama aliyekuwa anazama majini Kigamboni

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,581
Reaction score
10,110
1750244471514.jpg

Tumempoteza daktari bingwa wa dawa za usingizi hospitali ya taifa Muhimbili. Dr.Zhang Junqiao amefariki juzi tarehe 15/06/2025 huko Kigamboni baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dr.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dr.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dr.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).

Dr.Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. Dr.Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. Huu ni upendo wa ajabu. Dr.Zhang amefariki akiwa na umri wa miaka 38. Tumuombee pumziko la amani.!

Malisa
 
View attachment 3374554

RIP Jasusi
 
Aisee

Bachelar of Medicine
Bachelar of Surgery
Mmed internal medicine
Mmed anasthelogy

Halafu ana umri wa miaka 38

Kweli sisi bongo tunapoteza sana muda shuleni kwa elimu hizo zote angekua babu kama angesomea Bongo.

R.I.P specialist
 
Dr.Zhang alikua alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).
Hao jamaa huwa wakiamua kula kitabu wanakitendea haki hasa, siyo ku beep
 
Back
Top Bottom