Daktari feki akamatwa Mtwara

Akhy D

JF-Expert Member
Jun 10, 2013
365
500
Jeshi la Polisi mkoani hapa limemkamata na kumfikisha mahakamani Halima Sanga au Halima Hamadi mkazi wa jijini Dar es Salaam, kutokana na kosa la kughushi vyeti na kujipatia ajira serikalini ya udaktari wa daraja la pili kwa njia ya udanganyifu, akijulikana kwa jina la Dkt. Sarah Matuja.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, alisema mtuhumiwa huyo ambaye aliajiriwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kama daktari bingwa, alipangiwa kufanya kazi katika hospitali ya rufaa ya Ligula mkoani hapa na alianza kazi Mei 29 mwaka huu.
Alisema, uchunguzi ulianza baada ya wagonjwa wengi waliokwenda kutibiwa hospitalini hapo wakiwemo askari polisi kutoa malalamiko yao kutokana na kutoridhishwa na huduma zake, ambapo alikua anashindwa hata kusoma vipimo na kuandika kama madaktari wengine.
Alisema baada ya kupta taarifa hizo, ofisi ya mkuu wa mkoa iliamua kumuandikia barua ya kutaka uthibitisho wa uganga wake ambapo alijibu kuwa yeye ni mganga halali na amefuzu kufanya shughuli hiyo lakini watu wanampiga vita.
“Uchunguzi ulipoanza, alitakiwa kuripoti polisi lakini akawa anajificha..ila alikamatwa Agosti 2 mwaka huu akiwa ndani ya basi la Msimbati Line akiwa anataka kutoroka kuelekea jijini Dar es Salaam..” alisema.
Alisema kuwa, jeshi la Polisi baada ya kujiridhisha kuwa ni mdanganyifu, likaanza kumtafuta Dkt. Sara Matuja ambaye ndio jina alilokuwa akilitumia hospitalini hapo, na kubaini kuwa Sara Matuja ni Mganga katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza na ni daktari halisi baada kupata uthibitisho kutoka kwa baadhi ya watu wanaomfahamu ikiwa ni pamoja na mwalimu wake aliemfundisha.
“Mtuhumiwa tumemuhoji wapi alivipata vyeti vilivyomfanya apate ajira hiyo lakini alishindwa kueleza, pia hata kututajia ndugu zake, kabila lake kwao wapi alikataa..tumechunguza tumegundua ni msichana hatari sana, mwaka 2013 aliandikwa sana katika magazeti ya Uwazi akidai mara amebakwa na Mhe. Kapuya au amezaane..ana majina mengi, Felister, Leylate, Leyta, Halima Hamad..” aliongeza.
Aidha, alisema ana kesi katika ofisi ya Ustawi wa Jamii wilaya ya Ilala jiini Dar es Salaam juu ya matunzo ya watoto na mzazi mwenzie mtumishi wa serikali ambaye hakutaka jina lake liandikwe, ambapo huko alitumia jina la Halima Sanga.
Nipashe ilimtafuta Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Shaibu Maarifa kutaka kujuwa undani wa jambo hilo, ambapo alizungumza kwa wasiwasi kwa madai kuwa kesi yake ipo mahakamani huku akisema hakuna athari zozote za kimatibabu zilizosababishwa daktari huyo.
“Hakukuwa na athari zozote ila tu sisi tulipoona tuna mashaka juu ya utendaji wake tukampa taarifa katibu tawala ambaye aliamua ufikisha taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama..” alisema Dkt. Maarifa.
Alipoulizwa kama aliwahi kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya huduma zake labda ndio ilikuwa sababu ya kutokuwa na imani naye, alisema hakukuwa na malalamiko yoyote lakini walimtiliashaka tu kutokana na utendaji wake.
“Aliripoti hapa mwanzoni mwa mwezi Juni na tulimpokea kutoka katika ofisi ya katibu tawala, maana ndio utaratibu huo kwahiyo kama haturidhiki nao ndio tunampa taarifa” aliongeza.
Alisema Daktari huyo alikuwa amewekwa katika kitengo cha kushughulika na wagonjwa wan je (OPD) kwasababu ndio utaratibu ulivyo kwa madaktari wageni wanaoripoti na alikuwa anafahamika kwa jina la Dkt. Sara.
Alitoa wito kwa serikali kuwa makini na namna wanavyotoa ajira kwa kuchunguza vizuri vyeti na tabia za waombaji, na iwe hivyo kwa katika taasisi zote sio tu kwa hospitali.
Jitihada za kumpata Dkt. Sara Matuja mwenyewe ambae ni mwajiriwa katika hospitali ya Bugando, Mwanza hazikufanikiwa kutokana na simu yake kuzuiliwa katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoani hapa.
ImageUploadedByJamiiForums1440283731.182701.jpg ImageUploadedByJamiiForums1440283751.705711.jpg ImageUploadedByJamiiForums1440283769.995547.jpg
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
11,539
2,000
Tz kuna vitu feki vingi hv unaweza kuta unakwenda hosp ukahudumiwa na daktari feki alafu na dawa nazo ukapewa feki!
 

mbusage

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
444
250
Usiombe ukutane na huyuu hicho kisa kimemkuta mmke wangu daa huyuu Sala is a killer....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom