Daktari Feki akamatwa akitoa huduma ICU

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Ulrich Matei amesema mtu huyo ameshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tuhuma zinazo mkabili na mara baada ya kubaini ukweli wa jambo hilo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Wakizungumza na ITV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni walinzi na wauguzi waliomkamata mtuhumiwa huyo wameeleza namna hali ilivyokuwa huku muuguzi wa zamu akieleza utaratibu unaotumika kuwabaini wafanyakazi halali.

DDD.jpeg

Jamani me nadhani hata matapeli wanatakiwa kuangalia sehemu za kutapeli sasa ICU kweli wakuu
 
Habari wanaJF,

Daktari feki amekamatwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro.

===========

Weka basi ata kapicha
 
Pesa imekuwa ngumu sana ,!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Habari wanaJF,

Daktari feki amekamatwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro.

===========
Jamani me nadhani hata matapeli wanatakiwa kuangalia sehemu za kutapeli sasa ICU kweli wakuu

Source, au umejitungia tu?
 
sasa akifanya kazi ICU nani atakaemlipa mshahara? au ataiba vifaa akauze? lkn Kaingiaje ICU bila kufahamiana na uongozi wa hospitali husika? mi nadhani hapo kamchezo mshenzi Fulani hivii
 
Habari wanaJF,

Daktari feki amekamatwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro.

===========
Jamani me nadhani hata matapeli wanatakiwa kuangalia sehemu za kutapeli sasa ICU kweli wakuu
FOR WHAT PURPOSE AWE HUKO ICU AU KUNA JAMBO ALITAKA KUFANYA?
 
Daktari feki amekamatwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro.
 
sasa akifanya kazi ICU nani atakaemlipa mshahara? au ataiba vifaa akauze? lkn Kaingiaje ICU bila kufahamiana na uongozi wa hospitali husika? mi nadhani hapo kamchezo mshenzi Fulani hivii
Hapo lazima kuna Mwenyeji wake au ni kutoka na loose secirity procedures za uongozi wa Hospital. Mfano yule aliyekamatwa Mwanza mwezi wa 2 mpaka na meza na kiti cha kukalia anacho hapo Mganaga Mkuu eti anatuzuga kuwa hakuwa na taarifa yoyote. Nchi hii mhhhhh kazi ipo
 
Sijuwi kaanza lini kutoa Huduma na sijuwi kafikaje hapo mpaka awe anatowa huduma wakati ni daktari feki?
Tanzania sasa kila kitengo kuna kuna watumishi wa kupest Du hatari sijuwi lakini labda kasoma lakini alikosa hajira.
 
Habari wanaJF,

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Ulrich Matei amesema mtu huyo ameshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tuhuma zinazo mkabili na mara baada ya kubaini ukweli wa jambo hilo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Wakizungumza na ITV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni walinzi na wauguzi waliomkamata mtuhumiwa huyo wameeleza namna hali ilivyokuwa huku muuguzi wa zamu akieleza utaratibu unaotumika kuwabaini wafanyakazi halali.

View attachment 365188
Jamani me nadhani hata matapeli wanatakiwa kuangalia sehemu za kutapeli sasa ICU kweli wakuu
Si wiki iliyopita tuu alikamatwa nesi feki hapo hapo? Duh watu wanaroho ngumu
 
Mi swali langu kama daktari feki amekamatwa wodini huwa anategemea nini na wagonjwa hawalipi fedha cash kwa madaktari? shida hapa nini alichotegemea huyu munayemwita daktari feki?
 
Back
Top Bottom