Daily news yasifia CCM kijinga

Daily news yasifia CCM kijinga

Highlander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
3,093
Reaction score
1,077
Heshima kwako ndugu msomaji. Si busara sana kubishana na magazeti kwa sababu huwa hawapendi sana kukubali makosa. Lakini hili la Daily News naona nilisemee japo kidogo.

Wameandika taarifa hapa kusifia Chama Cha Mapinduzi na vyama vinavyounda Ukawa eti Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu CAG hajakuta kosa katika ukaguzi wa mahesabu ya vyama hivyo.

Huu ni upotoshaji unaotokana na ujinga katika mambo ya kihasibu. Najua waandishi wa habari wengi mambo ya hesabu yanawasumbua, lakini hata hili? Kama CAG kaweka QUALIFIED OPINION kwenye mahesabu ya vyama hivyo vinne, yaana CCM, CHADEMA, CUF na NCCR, hiyo ina maana mahesabu ya vyama hivyo yana utata.

Ndugu Zetu wa Daily News wao wanadhani eti hiyo Qualified Opinion eti ni sifa njema hiyo... Jamani Waandishi, haya mambo ya Uhasibu kama hamjui muwe mnaulizia kabla ya kuandika hivo vichwa vya habari...

TAARIFA YA DAILY NEWS HII HAPA, ETI...

CCM, 3 Other Parties in CAG Good Books

THE Controller and Auditor General (CAG) has given qualified opinion to all the big political parties' accounts, the Public Accounts Committee heard in Dar es Salaam.

Findings of the CAG indicate that some nine out of 21 political parties' accounts were audited on grounds of directives issued by the Parliamentary Public Account Committee (PAC) in October, last year.

The directive was then to audit political parties account from 2009/2010 to 2012/2013. The Political Parties Act stipulates that political parties that receive grants from the government to submit their audited report to the office of the Registrar of Political Parties by October 31.

On Tuesday, Assistant Auditor General, Mr Benja Majura presented the findings to the PAC, at a meeting attended by the Registrar of Political Parties; Judge (retired) Francis Mutungi. It shows that six political parties without representation in the House have a disclaimer opinion. Political parties that got qualified opinion, according to Mr Majura, are the ruling CCM, Chadema, CUF and NCCR Mageuzi.

However, UDP was the only political party, which is represented in the Parliament that was not audited. Mr Majura said the remaining six political parties, which were audited got disclaimer opinion after documents that they presented before the CAG failed to reconcile with parties accounts.

They are the National Reconstruction Alliance (NRA), Union for Multiparty (UMD), Africa Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo), National League for Democracy (NLD), Alliance for Democratic Change (ADC), Sauti ya Umma (SAU) and Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma).

It now turns out that the political parties that didn't submit their audited report risk losing some money, which they are given through grants. Judge Mutungi said Section 18 (4) of 1992 of the Political Parties Act requires his office to withhold some political parties' grants if they fail to submit audited report.

According to the Deputy Registrar of Political Parties, Mr Sisty Nyahoza, Section 18 (5) of the same Act gives the registrar powers to report any political party or politicians who will be implicated of embezzlement of public funds to police for necessary legal action.

He noted that in the event that any political party leader is found to have embezzled funds, the registrar has powers to report him to police so that they can investigate and bring the culprit before legal organs. Eight political parties, which are represented in the Parliament, are entitled to receive grants from the government. These include CCM, Chadema, CUF, NCCR, UDP, TLP, APPT Maendeleo and DP.

The CAG told the committee that his office encountered various challenges during the process of auditing political parties' accounts. Among the challenges, according to Mr Majura, is that many political parties don't have professional accountants. Mr Majura also added that various laws which govern political parties contradict one another.

"The Political Parties Act require the CAG to audit political parties by September, so that they can submit their report by the end of October but political parties are closing their books of accounts by the end of a calendar year; this makes it very difficult for the auditors," said Mr Majura.

The assistant CAG also added that it was difficult for his office to independently verify parties' properties, which were declared in the forms since most of them were not officially verifiable. Mr Majura also said some of political parties wanted the CAG to audit the accounts, which contained grants money and not those that contain money which are contributed by members and other institution.
 
Mie nafikiri baada ya kukuta mahesabu ya CCM yana matatizo basi CAG akaamua vyama vyote avipe hiyo...
"Qualified Opinion"
 
Nina wasiwasi na uelewa wa uhasibu wa cag,huwezi kutoa qualified opinion kwa chadema kisa wana akaunti nyingi..alitakiwa kutoa unqualified opinion with emphasis of matter paragraph...instead kaweka taaluma pembeni akatumikia kadi yake ya ccm ili apate uteuzi kamili.
 
Mie nafikiri baada ya kukuta mahesabu ya CCM yana matatizo basi CAG akaamua vyama vyote avipe hiyo...
"Qualified Opinion"

nakubaliana na wewe kabisa. ni njia ya kuepusha mzozo, au hata kunyanganywa cheo. Joto ya jiwe mwanasheria wa Zanzibar si unaikumbuka. Utouh analijua sana hilo.
 
Mie nafikiri baada ya kukuta mahesabu ya CCM yana matatizo basi CAG akaamua vyama vyote avipe hiyo...
"Qualified Opinion"
Hivi ingekuwa CCM wako safi na CHADEMA ndio wanakasoro kwenye ukaguzi unadhani sasa ingekuwaje hasa namna magazeti ya UHURU, JAMBO LEO, DAILY NEWS na MAJIRA ambavyo yangeandika? Na huko TBC ingekuwa ni Breaking news ya kila baada ya robo saa!
 
hivi nani huwa anamkagua CAG? yaani auditor anayemkagua ni nani?
 
Heshima kwako ndugu msomaji. Si busara sana kubishana na magazeti kwa sababu huwa hawapendi sana kukubali makosa. Lakini hili la Daily News naona nilisemee japo kidogo.

Wameandika taarifa hapa kusifia Chama Cha Mapinduzi na vyama vinavyounda Ukawa eti Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu CAG hajakuta kosa katika ukaguzi wa mahesabu ya vyama hivyo.

Huu ni upotoshaji unaotokana na ujinga katika mambo ya kihasibu. Najua waandishi wa habari wengi mambo ya hesabu yanawasumbua, lakini hata hili? Kama CAG kaweka QUALIFIED OPINION kwenye mahesabu ya vyama hivyo vinne, yaana CCM, CHADEMA, CUF na NCCR, hiyo ina maana mahesabu ya vyama hivyo yana utata.

Ndugu Zetu wa Daily News wao wanadhani eti hiyo Qualified Opinion eti ni sifa njema hiyo... Jamani Waandishi, haya mambo ya Uhasibu kama hamjui muwe mnaulizia kabla ya kuandika hivo vichwa vya habari...

Binafsi sioni kasoro kwenye habari hii ya Daily news. Hebu tujuze external auditors wana nafasi gani baada ya CAG kutoa ripoti yake?. Tunahitaji wakaguzi huru kwenye suala hili,
 
Mie nafikiri baada ya kukuta mahesabu ya CCM yana matatizo basi CAG akaamua vyama vyote avipe hiyo...
"Qualified Opinion"

unawezaje kufikiria wakati wewe haupo kwenye kichwa cha yule aliyeandaa ripoti?
 
hivi nani huwa anamkagua CAG? yaani auditor anayemkagua ni nani?
Hoja yako ni ya msingi sana!

Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia maoni ya CAG katika taasisi mbalimbali na kugundua kuwa ni maoni binafsi ya mkaguzi aliyepitia taarifa ya taasisi husika na siyo maoni ya taasisi nzima ya CAG! Kwa ufafanuzi ni kuwa taarifa hiyo hiyo ikipitiwa na mkaguzi mwingine maoni tofauti hutolewa!

Nilichogundua ni kuwa maoni mengi ya wakaguzi hutolewa kutegemea na mapokezi wanayoyapata katika taasisi husika! Na hapo usisahau RUSHWA!!

Hivyo nadhani utendaji kazi wa CAG kama taasisi unapaswa kuchunguzwa pia!!!
 
Hivi ingekuwa CCM wako safi na CHADEMA ndio wanakasoro kwenye ukaguzi unadhani sasa ingekuwaje hasa namna magazeti ya UHURU, JAMBO LEO, DAILY NEWS na MAJIRA ambavyo yangeandika? Na huko TBC ingekuwa ni Breaking news ya kila baada ya robo saa!

Nimecheka sana ndg yangu yaani kwao lingekuwa tukio lakiHISTORIA duh,,,,!
 
Ninavyo fahamu mimi ni kwamba National Audit huwa wanafanya Quality review tu..ila issue ya kukagua mahesabu huwa wanawapa tender external firms kufanya ukaguzi then ndio office ya CAG watapokea reports from independent firm..from there watafanya general conclusion bt kama wataona hawaridhika labda waende tu for clearance
 
Binafsi sioni kasoro kwenye habari hii ya Daily news. Hebu tujuze external auditors wana nafasi gani baada ya CAG kutoa ripoti yake?. Tunahitaji wakaguzi huru kwenye suala hili,

Kasoro iliyopo kwenye taarifa ya Daily News ni kwamba mkaguzi wa mahesabu wa nje ya shirika (katika case hii chama) anapokutana na mazingira yanayompa mashaka kuwa taarifa alizopewa hazielezi ukweli wote, kwamba pengine kuna utata umefichwa, hapo ndo mkaguzi anapoweka neno qualified. Mwandishi aliyeandika kichwa cha habari na ninadhani hata hiyo habari yenyewe alidhani qualified ni kufaulu. Kumbe lugha ya Uhasibu kuna wakati hutumia maneno ya Kiingereza kuwa na maana za kihasibu ambazo ni tofauti na maana yake katika lugha ya kawaida. Labda Adverse Opinion ndo haipishani sana na maana halisi.

CAG ni mrithi wa Tanzania Audit Corporation ya Zamani. Huyu alikuwa aina ya External Auditor katika taasisi zenye uhusiano na serikali kama vile SU na CCM au TANU wakati huo. Kwa hiyo unaposema Hebu tujuze external auditors wana nafasi gani baada ya CAG kutoa ripoti yake? unaleta hoja kwamba Baada ya CAG kutoa ripoti, aje na mkaguzi mwinginewe kutoka nje arudie kazi aliyoifanya CAG. Kama hivi ndivyo ulivyokuwa na maana, basi napenda kusema nakuunga mkono.

Maeneo mangine awe anakuja na Mkaguzi mwingine ambaye hafungamani na Serikali wala Chama tuone kama hizi taarifa zitakuwaje. Hasa hizi za vyama vya siasa. Nakubaliana nawe kabisa. Sidhani kama CAG ni huru... aje aliye huru afanye hizi kazi tuone taarifa zitafananaje.
 
Hakika una-deserve kuitwa Highlander,jamii forums inapata sifa kwa sababu ya watu kama nyie. Hoja inapaswa kujibiwa kwa hoja na siyo matusi wala porojo,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom