Dai hili la wana UAMSHO lisipuuzwe, kwani lina harufu ya madhara makubwa hapo baadae

Wewe! Boko haram imesajiliwa wapi na lini. Kundi haramu lililoanzishwa na wahausa huko Naijeria. Rudi kwenye hiyo thread na usome kwa makini.

nitakuja na info zote. na hiyo link ili zjisomee. muda wa kuswali huu Juma nenda masjid sheikh
 
hebu rudi kwenye thread na uisome kwa makini sio ukurupuke tu kuja kuandika hapa, hata hao BOKO HARAM walisajiliwa kama UAMSHO lakini sasa wanachoma moto makanisa, na uamsho nao washaanza kuchoma moto makanisa na hawa UAMSHO sio kwamba wapo Zanzibar tu mpaka Oman, Iran pia ndio wamewatuma hawa kuleta propaganda na wazenji elimu dunia kichwani ni sifuri wanameza kila kitu

Usitoke povu mkuu nia yangu ilikuwa kukusaidia tu. Kuna huu utaratibu wa ubongo kujiandaa kubisha kabla ya kutafakari ndio unasababisha wewe huelewi jambo dooogo kama hili
UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

Twende step by step:
1. kundi huru, bila uficho, usajili wa serikali anamaanisha lipo katika jamii na serikali inalitambua (inawajua wahusika wake na inajua pa kuwapata)
2. Tofauti na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB (ambayo yenyewe wahusika wake hawapatikaniki kirahisi)
3. Sasa njoo kwenye bluu = anachoshangaa Jumakidogo ni kwamba, pamoja na serikali kuwajua na kuwatambua (kwa sbb ni huru na wanafahamika) tofauti na BOKO HARAM (ambao wanajificha), mbona serikali haiwachukulii hatua stahiki zaidi ya kutoa matamko tu?

''Kwa kifupi Jumakidogo anaishangaa serikali kwamba inashindwa nini kudhibiti kundi hili hatari wakati lipo karibu na mkono wake?''

Kama hutaelewa hapo napo kwa kweli nitakuwa nimechoka
 
Last edited by a moderator:
Serikali imeshindwa nini kuwashughulikia hawa mahayawani?
 
Ma UAMSHO yamekimbia maswali, mijitu minafiki inataka kutufanya wote hatuna akili hapa. Eti Zanzibar huru! Itakuwa huru wakati mnataka kuiuza Oman? Nia ya kuchoma makanisa ni kuwahamisha mnaowatilia mashaka kuwa hawatakuwa tayari kushiriki uuzaji wa Zanzibar kwa wafanyabiashara wa kiarabu.

Mnajitia kutaka kura ya maoni kuamua, haya mnayoamua nyinyi mmefanyia wapi kura ya maoni? Nyie kimbieni lkn nitakapowaona, swali langu nitalirejesha mlijibu
 
Tatizo lako wewe nini Jumakidogo?

Umetishwa nini/ na ibara ya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya watu wa Zanzibar 1984 kuwa Zanzibar ni nchi na ina mipaka yake na mikoa yake kabla ya Muungano wa Ilokuwa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa laumihimu kwako kama umetishwa na Kivuli cha Jumuia ya Uamsho nikurudisha Katiba ya nchi yako ya Tanganyika na kulinda mipaka na rasilimali zenu zisije zikachukuliwa ukivunjika Muungano .

ikiwa una hofu hio saidia katika Kuvunja Muungano sio kuwa kinganganizi wa Muungano huku hufaidiki chochote ispokuwa hasara? vunja Muungano ulinde utajiri na mali zenu.

Au unaona huto zaa mtoto mwenye nyele za Singa? maana kama musemavyo wenywewe muna kila utajiri na majisimu na majigambo lakini kukataliwa tu hamuhuwi bado muko vingaganizi, aibu imawafiki wezanzu mwajitao Watanzania mukaiwacha Tanganyika yenu kwenda na maji.
kasome historia upya maili 10 za pwani zilibadilishwa na kisiwa cha witu.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye bluu ndio panapoonesha unafiki wenu. Ndio uthibitisho kuwa mmetumwa na waarabu fulani kukipora hiki kisiwa.

Kama nyinyi mnadai kura ya maoni ili Wazanzibari waamue wenyewe juu ya htma ya Zanzibar yao, mbona hapa mmeanza kuwaamulia kuwa DSM mtaiacha ipotee? Mlifanya wapi kura ya maoni kuamua msimamo huu? Mnasema Karume aliikabidhi Zanzibar kwa Nyerere bila ridhaa ya Wazanzibari, mbona na nyie wanafiki mnaikabidhi DSM kwa Kikwete?

" sijashuhudia wala kusikia waZanzibari wakidai warejeshewe kipande cha ardhi yao cha Tanganyika, wala kudai eneo la dola yao, kilio chetu kikubwa ni eneo hili hili tulilonalo baada ya uhuru/mapinduzi, hata kama itatokezea hivyo bila ya shaka watu si wataulizwa kupitia kura ya maoni iliyopo kisheria?

hakutakuwa na ubaya ati tukianza kuirejesha dola yetu kidogo kidogo mwishowe tufikie ile dola yetu ya asili waliyoanza kutupora wakoloni, walipokaa na kupanga mipaka ya africa (mkutano wa berlin mwaka nimeusahau).

ila kwa sasa ni kutoka kwenye huu muungano feki wa kidola, ama ule wa kijamii abadan hatuwezi kuuepuka n atutakuwa nao ndani ya damu zetu"
 
Serikali imeshindwa nini kuwashughulikia hawa mahayawani?

" tutukane upendavyo, ila sisi si mahayawani, maana hili jumuiya ni yetu waZanzibari inayotusimamia tu kupata matakwa yetu baada ya kuon alongo longo nyingi za vyama vya siasa. SOVEREIGN ZANZIBAR FIRST!"

Usitoke povu mkuu nia yangu ilikuwa kukusaidia tu. Kuna huu utaratibu wa ubongo kujiandaa kubisha kabla ya kutafakari ndio unasababisha wewe huelewi jambo dooogo kama hili

Twende step by step:
1. kundi huru, bila uficho, usajili wa serikali anamaanisha lipo katika jamii na serikali inalitambua (inawajua wahusika wake na inajua pa kuwapata)
2. Tofauti na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB (ambayo yenyewe wahusika wake hawapatikaniki kirahisi)
3. Sasa njoo kwenye bluu = anachoshangaa Jumakidogo ni kwamba, pamoja na serikali kuwajua na kuwatambua (kwa sbb ni huru na wanafahamika) tofauti na BOKO HARAM (ambao wanajificha), mbona serikali haiwachukulii hatua stahiki zaidi ya kutoa matamko tu?

''Kwa kifupi Jumakidogo anaishangaa serikali kwamba inashindwa nini kudhibiti kundi hili hatari wakati lipo karibu na mkono wake?''

Kama hutaelewa hapo napo kwa kweli nitakuwa nimechoka

Kaenda kuswali mkuu. Nadhani kwa somo hilo ataelewa, acha tusubiri aje.
 
Last edited by a moderator:
" sijashuhudia wala kusikia waZanzibari wakidai warejeshewe kipande cha ardhi yao cha Tanganyika, wala kudai eneo la dola yao, kilio chetu kikubwa ni eneo hili hili tulilonalo baada ya uhuru/mapinduzi, hata kama itatokezea hivyo bila ya shaka watu si wataulizwa kupitia kura ya maoni iliyopo kisheria?

hakutakuwa na ubaya ati tukianza kuirejesha dola yetu kidogo kidogo mwishowe tufikie ile dola yetu ya asili waliyoanza kutupora wakoloni, walipokaa na kupanga mipaka ya africa (mkutano wa berlin mwaka nimeusahau).

ila kwa sasa ni kutoka kwenye huu muungano feki wa kidola, ama ule wa kijamii abadan hatuwezi kuuepuka n atutakuwa nao ndani ya damu zetu"

Nina maswali mengi nimeuliza naona unajibu kamoja. Hata hivyo, hujaniambia bado mmepata wapi mamlaka ya kuwasemea Wazanzibari. Na je kwa nini vuguvugu hili libebewe kwenye jukwaa la dini na si siasa ili Wazanzibari wote washiriki?

Kama unataka kushindana na mipaka waliyoiweka wakoloni walipokaa Berlin, huo unaoutambua wewe kuwa unaipa Zanzibar 10miles along the coastal strip uliwekwa na nani? Watumbatu au Wakojani?
 
nadhani uelewa wako una matatizo, nimekwambia hebu ingia google ujisomee hao AL KAIDA na BOKO HARAM walianzaje? na wakapewa usajili kama uamsho?
Tatizo letu waTanganyika huwa tunachukulia mambo mzaha sana. Hao Boko Haram walianza kwa madai ya kipuuzi Kama haya. Angalia leo hii wanachofanya huko Nigeria. Mbali na hiyo, kuna copycats ambao wanaweza kujitoa mhanga kwa ajili ya imani na msimamo wa hao Uamsho. Mimi ni Muislam lakini siungi mkono hizi hisia za udini kwenye mambo ya siasa na nchi nzima kwa ujumla. Mifano ya hatari ya machafuko ipo mingi.
 
Ndugu watanganyika wenzangu wana wa JF, Hebu tukae chini na kujadili japo kwa uchache kuhusu moja kati ya madai ya ndugu zetu Wazanzibar wanaowakilishwa na wana wa UAMSHO katika harakati za kudai uhuru wa nchi yao.

Tujadili kwa amani bila jazba wala kuingiza kashfa kutoka dini moja kwenda nyingine. Jambo moja tu, nalo ni dai lao hili hapa chini…

(Maili 20 kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar)

Kwa hesabu za haraka haraka kama unaenda Morogoro, bila shaka ni mpaka maeneo ya Kimara au Kimara Suka hivi.

Maili 20 kutoka fukwe za bahari ya hindi kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar. Hayo ni madai ya kushangaza kutoka kundi la UAMSHO, Ni dai lenye kila dalili kuwa lina chokochoko zaidi ya lile dai lao la msingi la kutaka kuuvunja muungano. Pamoja na madai mengine kutoka kwa wanajumuia wanaojiita UAMSHO.

Hili ndilo moja kuu ambalo kwa upande wangu naona linatisha zaidi, bila ya shaka hii taarifa ni ngeni sana miongoni mwa watanganyika lukuki ambao wanaijua vizuri historia ya nchi yao. Sijaona sababu ya mamlaka zinazohusika kuyakalia kimya na kuyapuuza madai ya ajabu kama haya.

Kuna kauli za kupuuzwa kutokana na aina ya mtoaji kauli mwenyewe, kwa kuwa kundi hili la UAMSHO limeonyesha kuwa lina dhamira ya dhati ya kudai Zanzibar huru na matokeo ya dhamira yao yameonekana kwa kuteketeza majumba ya ibada ya watu wa imani nyingine, pamoja na kuharibu mali za watu wasio na hatia.

Sioni sababu ya kupuuzwa maneno ya watu hawa hata kidogo. Itakapofikia muda wao wa kuja kudai ardhi yao ambayo wanadai vibali na hati wanazo. Ni mashaka yangu kutakuwa na madhara makubwa hapo baadaye ambayo nina hakika yanaweza kutafutiwa dawa mapema.

UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

Sitarajii kama kutatokea waislamu wa kweli hapa na makini wakatetea aina hii ya makundi na wanaharakati wanaoangamiza bila sababu badala ya kuhubiri amani kama sifa ya mwislamu wa kweli inavyotakiwa iwe.
HIYO NI KWA MUJIBU YA MIPAKA YA MWARABU KARNE YA 14, NA HIYO SIO DAR PEKEE MPAKA TANGA NA MOMBASA KENYA NI ENEO LA ZNZ.LAKINI BAADA YA BERLIN MIPAKA AFRIKA ILIWEKWA UPYA,hivyo hata umoja wa mataifa wanaitambua znz kama unguja na pemba tu kutokana na mipaka hiyo,hata muingereza alivotawala znz ilikuwa ni unguja na pemba.WASIKUUMIZE KICHWA KWA HIZO HADITHI ZAO,huu muungano ni wa kuvunja haraka sana TUMEKOSA TU KIONGOZI,viongozi wetu wanang'ata na kupuliza sio ajabu wanajua a-z ya kila kitu.
dawa ni kuuvunja fasta alafu wakitaka tuwatawale sasa wawe watumwa vizuri wajidai kusema dar ni yao hapo tutateka kisiwa chote maana watakuwa wanafanya uhaini.berlin conference ambayo mikapa yake ndio hutumika inaijua znz kama pemba and unguja only.
 
Nilipo Blue.

Hitimisho lako ni khatari sana na tusi kubwa sana kwa waislam na uislam.

labda utudadavulie waislam wa kweli na makini wana swifa gani na akina nani?

Lakin pia ningependa nikujuze kuwa Jumuiya ya UAMSHO viongozi wake ni wasomi na wengi wao kama sio wote ni graduates na wengine wameenda mbali zaidi mpaka kufikia shahada za uzamili na wamesomea sio tu Tz bali na hata nje ya nchi.

Sasa siku zote unapomuona msomi analeta hoja basi ujue ana mashiko yaani wana evidence zinazowapelekea kusema hayo. sasa pima sababu zao kisha na wewe ulete hoja badala ya kutaka kuwagawa na kuwatusi bila sababu.

Skuli ni muhimu sna kwa mwan'Adam kuweza kujipambanua.

:A S-omg:
 
Mwenyenu mnisamehe.
Hili neno UAMSHO me nakosea kila wakati nasema MRISHO sijui kwanini
 
BWANA YESU ANAOKOA, KWA NINI MNAUMIZA AKILI HIVI?KWA NINI MNASONONEKA?KWA NINI MNAHANGAIKA NA HII DUNIA? MPE BWANA YESU MAISHA YAKO NA KUHAKIKISHIA HUTA JUTA,roho ya hasira,chuki na mambo mabaya yataondoka nawe utakuwa mwenye furaha muda wote.KARIBU KANISA LOLOTE LILILOKARIBU NAWE LINALOAMINI WOKOVU.
AU TUWASILIANE KWA EMAIL :johnhella2007@yahoo.com hiyo email naitumia hata facebook ukisearch kwa email hiyo utanipata
 
  • Thanks
Reactions: F2S
Hivi hawa waislamu nani kawaroga?!!!! Mahakama ya kadhi wanataka waanzishiwe na serikali!!!! Sensa wanataka wafanyiwe na serikali!!! Hadi mitihani wanataka serikali iwasaidie kupass!!!! Sasa nusu ya jiji la Dar es salaam ni sehemu ya Zanzibar... Huu nao ni uendawazimu mwingine!!
 
we hujui hayo makundi yalianza kama huu UAMSHO? unaoupigia debe. huu UAMSHO ni kikundi cha maharamia na watakuja kusumbua sana ikiwemo kuteka meli, na washaanza kuchoma moto makanisa, hawa sio watu wema kabisa na washukuru hizi ni zama za baba MwanaAsha na Saidi Mwema waislamu wenzao ndio maana wanapumua,,, lakini huu nao ni upepo watapita haraka
Pitia hapa unaweza kujifunza kitu. Link https://www.jamiiforums.com/kenyan-...a-kukutana-na-kundi-lisilo-halali-la-mrc.html
 
HIYO NI KWA MUJIBU YA MIPAKA YA MWARABU KARNE YA 14, NA HIYO SIO DAR PEKEE MPAKA TANGA NA MOMBASA KENYA NI ENEO LA ZNZ.LAKINI BAADA YA BERLIN MIPAKA AFRIKA ILIWEKWA UPYA,hivyo hata umoja wa mataifa wanaitambua znz kama unguja na pemba tu kutokana na mipaka hiyo,hata muingereza alivotawala znz ilikuwa ni unguja na pemba.WASIKUUMIZE KICHWA KWA HIZO HADITHI ZAO,huu muungano ni wa kuvunja haraka sana TUMEKOSA TU KIONGOZI,viongozi wetu wanang'ata na kupuliza sio ajabu wanajua a-z ya kila kitu.
dawa ni kuuvunja fasta alafu wakitaka tuwatawale sasa wawe watumwa vizuri wajidai kusema dar ni yao hapo tutateka kisiwa chote maana watakuwa wanafanya uhaini.berlin conference ambayo mikapa yake ndio hutumika inaijua znz kama pemba and unguja only.
Nimesoma katika hii link https://www.jamiiforums.com/kenyan-...a-kukutana-na-kundi-lisilo-halali-la-mrc.html

They should also convince MRC that the 1963 Lancaster agreement between the British, the Sultan of Zanzibar and the Kenyan government on the coastal strip will not expire next year as the group is claiming.
 
Ndugu watanganyika wenzangu wana wa JF, Hebu tukae chini na kujadili japo kwa uchache kuhusu moja kati ya madai ya ndugu zetu Wazanzibar wanaowakilishwa na wana wa UAMSHO katika harakati za kudai uhuru wa nchi yao.

Tujadili kwa amani bila jazba wala kuingiza kashfa kutoka dini moja kwenda nyingine. Jambo moja tu, nalo ni dai lao hili hapa chini…

(Maili 20 kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar)

Kwa hesabu za haraka haraka kama unaenda Morogoro, bila shaka ni mpaka maeneo ya Kimara au Kimara Suka hivi.

Maili 20 kutoka fukwe za bahari ya hindi kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar. Hayo ni madai ya kushangaza kutoka kundi la UAMSHO, Ni dai lenye kila dalili kuwa lina chokochoko zaidi ya lile dai lao la msingi la kutaka kuuvunja muungano. Pamoja na madai mengine kutoka kwa wanajumuia wanaojiita UAMSHO

Tanganyika ina mkataba kama huu wa Kenya?

They should also convince MRC that the 1963 Lancaster agreement between the British, the Sultan of Zanzibar and the Kenyan government on the coastal strip will not expire next year as the group is claiming.
Link https://www.jamiiforums.com/kenyan-...a-kukutana-na-kundi-lisilo-halali-la-mrc.html

Hata hivyo, UAMSHO wamesema hivi,"Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid:
Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang'ang'ania hiki tu!
link » Blog Archive » Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

CCM imeshikwa sehemu nyeti,"muungano"
 
Nilipo Blue.

Hitimisho lako ni khatari sana na tusi kubwa sana kwa waislam na uislam.

labda utudadavulie waislam wa kweli na makini wana swifa gani na akina nani?

Lakin pia ningependa nikujuze kuwa Jumuiya ya UAMSHO viongozi wake ni wasomi na wengi wao kama sio wote ni graduates na wengine wameenda mbali zaidi mpaka kufikia shahada za uzamili na wamesomea sio tu Tz bali na hata nje ya nchi.

Sasa siku zote unapomuona msomi analeta hoja basi ujue ana mashiko yaani wana evidence zinazowapelekea kusema hayo. sasa pima sababu zao kisha na wewe ulete hoja badala ya kutaka kuwagawa na kuwatusi bila sababu.

Skuli ni muhimu sna kwa mwan'Adam kuweza kujipambanua.

Nafikiri hata maana ya usomi haieleweki kwa wengi. Usomi siyo kukaa tu darasani bali ni elimu uliyotoka nayo baada ya kukaa darasani. Hata kama ungekaa darasani miaka hamsini, kama utakapotoka darasani unaanza kuchoma nyumba za majirani zako wewe siyo msomi wala si binadamu wa kawaida, wewe ni kichaa, ni mtu hatari kuliko ambaye hakuwahi kukaa darasani hata siku moja.

Osama bin Laden na wale madaktari wake wa kuua watu nao tuwaite ni wasomi? Akina Konyi na falsafa zao za kuongoza nchi kwa amri 10 za Mungu huku wakiua watoto na kuvitumia visichana vidogo kwa ngono, nao utawaita ni wasomi kwa vile tu Konyi aliwahi kuhudhuria madarasa? Nao akina Savimbi waliokuwa wakiwavunja na kuwakata miguu raia wakiwa hai, na wengine kushona midomo kwa sindano na nyuzi za kushonea nguo, nao utawaita ni wasomi eti tu kwa vile walikaa miaka mingi darasani?

Kwenye kundi la Wanauamusho, hata kama kuna mtu alikaa darasani mpaka akazeekea huko, kutokana na matendo yao, hakuna hata mmoja mwenye sifa ya kuitwa msomi. Hawa ni mashetani na ni majambazi, si viongozi wa dini, si wasomi wala watu waliostaarabika ambao wanastahili kupewa heshima ya ubinadamu. Hawa ni binadamu kimaumbile lakini ni hayawani kifikra na kimoyo. Hakuna aliye mzima anayeweza kuhamasisha wafuasi wake wachome nyumba za ibada. Hawa wanatafuta mahali pakuanzia, kuchoma makanisa ilikuwa na nia ya kuamsha hasira za wakristo ili kama wangejibu kwa namna yeyote ile, waweze kuanzisha vita za kihuni halafu waiite ni vita ya kidini.

Mahali alikosomea kiongozi wao ni Sudani, ambako kuna shule za siri za ugaidi. Huko ndiko walikoanzia akina Osama bin Laden na wenzake. Usomi walioenda kuutafuta Sudan ni usomi wa kuangamiza binadamu.

Tanzania ni lazima tutambue kuwa kuna adui ameingia nchini mwetu ambaye anastahili kupigwa kwa nguvu zote, huyu si mwingine bali ni hawa wanaojiita wanauamsho. Hawa wakiachwa watakuja kutuangamiza sisi na watoto wetu. Watakapoanza kujilipua, hawatachagua kama wewe ni mtoto au mtu mzima, kama ni mwanamke au mwanaume, kama ni muislam au ni mkristo, kama ni Mtanganyika au Mzanzibari. Huko kote yanakotokea mauaji, makundi yanayowaangamiza wenzao yalianza hivihivi kama Wanauamsho.
 
Back
Top Bottom