Dai hili la wana UAMSHO lisipuuzwe, kwani lina harufu ya madhara makubwa hapo baadae

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Ndugu watanganyika wenzangu wana wa JF, Hebu tukae chini na kujadili japo kwa uchache kuhusu moja kati ya madai ya ndugu zetu Wazanzibar wanaowakilishwa na wana wa UAMSHO katika harakati za kudai uhuru wa nchi yao.

Tujadili kwa amani bila jazba wala kuingiza kashfa kutoka dini moja kwenda nyingine. Jambo moja tu, nalo ni dai lao hili hapa chini…

(Maili 20 kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar)

Kwa hesabu za haraka haraka kama unaenda Morogoro, bila shaka ni mpaka maeneo ya Kimara au Kimara Suka hivi.

Maili 20 kutoka fukwe za bahari ya hindi kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar. Hayo ni madai ya kushangaza kutoka kundi la UAMSHO, Ni dai lenye kila dalili kuwa lina chokochoko zaidi ya lile dai lao la msingi la kutaka kuuvunja muungano. Pamoja na madai mengine kutoka kwa wanajumuia wanaojiita UAMSHO.

Hili ndilo moja kuu ambalo kwa upande wangu naona linatisha zaidi, bila ya shaka hii taarifa ni ngeni sana miongoni mwa watanganyika lukuki ambao wanaijua vizuri historia ya nchi yao. Sijaona sababu ya mamlaka zinazohusika kuyakalia kimya na kuyapuuza madai ya ajabu kama haya.

Kuna kauli za kupuuzwa kutokana na aina ya mtoaji kauli mwenyewe, kwa kuwa kundi hili la UAMSHO limeonyesha kuwa lina dhamira ya dhati ya kudai Zanzibar huru na matokeo ya dhamira yao yameonekana kwa kuteketeza majumba ya ibada ya watu wa imani nyingine, pamoja na kuharibu mali za watu wasio na hatia.

Sioni sababu ya kupuuzwa maneno ya watu hawa hata kidogo. Itakapofikia muda wao wa kuja kudai ardhi yao ambayo wanadai vibali na hati wanazo. Ni mashaka yangu kutakuwa na madhara makubwa hapo baadaye ambayo nina hakika yanaweza kutafutiwa dawa mapema.

UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

Sitarajii kama kutatokea waislamu wa kweli hapa na makini wakatetea aina hii ya makundi na wanaharakati wanaoangamiza bila sababu badala ya kuhubiri amani kama sifa ya mwislamu wa kweli inavyotakiwa iwe.
 
Hayo waachichie slaa chadema na wanaharakati wa zanzibar. Kila mbinu ya kuingia ikulu haiwezekani. Kelele hazimnyimi usingizi mwenye nyumba.
 
UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

we hujui hayo makundi yalianza kama huu UAMSHO? unaoupigia debe. huu UAMSHO ni kikundi cha maharamia na watakuja kusumbua sana ikiwemo kuteka meli, na washaanza kuchoma moto makanisa, hawa sio watu wema kabisa na washukuru hizi ni zama za baba MwanaAsha na Saidi Mwema waislamu wenzao ndio maana wanapumua,,, lakini huu nao ni upepo watapita haraka
 
Nilisha sema serikali legelege hushindwa kuzibi magaidi kama tunavyo ona.

Nakataa kauli ya kusema uamsho ni tofauti na boko haramu na alsha bab, hakuna tofauti ya kikundi cha uamsho na vikundi vingine kama boko haram,alshabab wote ni magaidi wachoma makanisa.

Hadi leo kikundi cha uamsho hakijawai kusema sababu za kuchoma makanisa.

Nashauri serikali ianze taratibu za kukiangamiza kikundi hiki cha magaidi kwa maslai ya nchi. Ni kazi ndogo ambayo inayowezwa kumalizwa na JWTZ .
 
we hujui hayo makundi yalianza kama huu UAMSHO? unaoupigia debe. huu UAMSHO ni kikundi cha maharamia na watakuja kusumbua sana ikiwemo kuteka meli, na washaanza kuchoma moto makanisa, hawa sio watu wema kabisa na washukuru hizi ni zama za baba MwanaAsha na Saidi Mwema waislamu wenzao ndio maana wanapumua,,, lakini huu nao ni upepo watapita haraka

Aisee! Ntake radhi ndugu haraka. Mi siwezi kupigia debe upuuzi. Hujaelewa maana ya kuyatofautisha makundi hayo. Kwamba UAMSHO wamesaliwa na wanapatikana ki rahisi tofauti na hao wengine.
 
Tatizo lako wewe nini Jumakidogo?

Umetishwa nini/ na ibara ya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya watu wa Zanzibar 1984 kuwa Zanzibar ni nchi na ina mipaka yake na mikoa yake kabla ya Muungano wa Ilokuwa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa laumihimu kwako kama umetishwa na Kivuli cha Jumuia ya Uamsho nikurudisha Katiba ya nchi yako ya Tanganyika na kulinda mipaka na rasilimali zenu zisije zikachukuliwa ukivunjika Muungano .

ikiwa una hofu hio saidia katika Kuvunja Muungano sio kuwa kinganganizi wa Muungano huku hufaidiki chochote ispokuwa hasara? vunja Muungano ulinde utajiri na mali zenu.

Au unaona huto zaa mtoto mwenye nyele za Singa? maana kama musemavyo wenywewe muna kila utajiri na majisimu na majigambo lakini kukataliwa tu hamuhuwi bado muko vingaganizi, aibu imawafiki wezanzu mwajitao Watanzania mukaiwacha Tanganyika yenu kwenda na maji.
 
Last edited by a moderator:
yaani ninyi wapemba watu wa ajabu sana hivi mnajua kuwa ninyi siyo raia wa hapo mnapopadai? Hebu nendeni kwenu pemba kule msumbiji ndipo mkadai hiyo maili 20. naomba uamsho waende Taiwan wawaulize vizuri walipoleta upuuzi kama wenu serikali ya China iliwaambia nini na mpaka leo wameishia wapi.

ningekuwa na uwezo ningevizamisha hivyo visiwa bahari ya Hindi
 
Tatizo lako wewe nini Jumakidogo?

Umetishwa nini/ na ibara ya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya watu wa Zanzibar 1984 kuwa Zanzibar ni nchi na ina mipaka yake na mikoa yake kabla ya Muungano wa Ilokuwa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa laumihimu kwako kama umetishwa na Kivuli cha Jumuia ya Uamsho nikurudisha Katiba ya nchi yako ya Tanganyika na kulinda mipaka na rasilimali zenu zisije zikachukuliwa ukivunjika Muungano .

ikiwa una hofu hio saidia katika Kuvunja Muungano sio kuwa kinganganizi wa Muungano huku hufaidiki chochote ispokuwa hasara? vunja Muungano ulinde utajiri na mali zenu.

Au unaona huto zaa mtoto mwenye nyele za Singa? maana kama musemavyo wenywewe muna kila utajiri na majisimu na majigambo lakini kukataliwa tu hamuhuwi bado muko vingaganizi, aibu imawafiki wezanzu mwajitao Watanzania mukaiwacha Tanganyika yenu kwenda na maji.

Ha ha ha haaaaaa! Nimecheka! Nmecheka mpaka nimekosa cha kuchangia, ntakujibu lakini. Subiri kwanza.
 
Last edited by a moderator:
UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

Sitarajii kama kutatokea waislamu wa kweli hapa na makini wakatetea aina hii ya makundi na wanaharakati wanaoangamiza bila sababu badala ya kuhubiri amani kama sifa ya mwislamu wa kweli inavyotakiwa iwe.

Nilipo Blue.

Hitimisho lako ni khatari sana na tusi kubwa sana kwa waislam na uislam.

labda utudadavulie waislam wa kweli na makini wana swifa gani na akina nani?

Lakin pia ningependa nikujuze kuwa Jumuiya ya UAMSHO viongozi wake ni wasomi na wengi wao kama sio wote ni graduates na wengine wameenda mbali zaidi mpaka kufikia shahada za uzamili na wamesomea sio tu Tz bali na hata nje ya nchi.

Sasa siku zote unapomuona msomi analeta hoja basi ujue ana mashiko yaani wana evidence zinazowapelekea kusema hayo. sasa pima sababu zao kisha na wewe ulete hoja badala ya kutaka kuwagawa na kuwatusi bila sababu.

Skuli ni muhimu sna kwa mwan'Adam kuweza kujipambanua.

Ndugu watanganyika wenzangu wana wa JF,

(Maili 20 kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar)

Kwa hesabu za haraka haraka kama unaenda Morogoro, bila shaka ni mpaka maeneo ya Kimara au Kimara Suka hivi.

Maili 20 kutoka fukwe za bahari ya hindi kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar. Hayo ni madai ya kushangaza kutoka kundi la UAMSHO, Ni dai lenye kila dalili kuwa lina chokochoko zaidi ya lile dai lao la msingi la kutaka kuuvunja muungano.

Hii ndio moja ya sababu ya Zanzibar kubaki kuwa mali yetu daima!
 
Ndugu watanganyika wenzangu wana wa JF, Hebu tukae chini na kujadili japo kwa uchache kuhusu moja kati ya madai ya ndugu zetu Wazanzibar wanaowakilishwa na wana wa UAMSHO katika harakati za kudai uhuru wa nchi yao.

Tujadili kwa amani bila jazba wala kuingiza kashfa kutoka dini moja kwenda nyingine. Jambo moja tu, nalo ni dai lao hili hapa chini…

(Maili 20 kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar)

Kwa hesabu za haraka haraka kama unaenda Morogoro, bila shaka ni mpaka maeneo ya Kimara au Kimara Suka hivi.

Maili 20 kutoka fukwe za bahari ya hindi kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam ni ardhi ya Zanzibar. Hayo ni madai ya kushangaza kutoka kundi la UAMSHO, Ni dai lenye kila dalili kuwa lina chokochoko zaidi ya lile dai lao la msingi la kutaka kuuvunja muungano. Pamoja na madai mengine kutoka kwa wanajumuia wanaojiita UAMSHO.

Hili ndilo moja kuu ambalo kwa upande wangu naona linatisha zaidi, bila ya shaka hii taarifa ni ngeni sana miongoni mwa watanganyika lukuki ambao wanaijua vizuri historia ya nchi yao. Sijaona sababu ya mamlaka zinazohusika kuyakalia kimya na kuyapuuza madai ya ajabu kama haya.

Kuna kauli za kupuuzwa kutokana na aina ya mtoaji kauli mwenyewe, kwa kuwa kundi hili la UAMSHO limeonyesha kuwa lina dhamira ya dhati ya kudai Zanzibar huru na matokeo ya dhamira yao yameonekana kwa kuteketeza majumba ya ibada ya watu wa imani nyingine, pamoja na kuharibu mali za watu wasio na hatia.

Sioni sababu ya kupuuzwa maneno ya watu hawa hata kidogo. Itakapofikia muda wao wa kuja kudai ardhi yao ambayo wanadai vibali na hati wanazo. Ni mashaka yangu kutakuwa na madhara makubwa hapo baadaye ambayo nina hakika yanaweza kutafutiwa dawa mapema.

UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likuwa na usajili halali wa serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB. Inashangaza kuona ni kwa nini serikali za jamhuri ya muungano na ile ya mapinduzi Zanzibar wanatoa matamshi mepesi bila ya kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti watu hawa ambao tayari wameshasababisha madhara makubwa.

Sitarajii kama kutatokea waislamu wa kweli hapa na makini wakatetea aina hii ya makundi na wanaharakati wanaoangamiza bila sababu badala ya kuhubiri amani kama sifa ya mwislamu wa kweli inavyotakiwa iwe.

wacha kuwapotosha watu, soma hapo chini mahojiano ya JAMHURI na SHEIKH FARID hasa katika swali la Maili 10 za Dar (nimeweka rangi) alivyolijibu sheikh kwa ufasaha kabisa.

Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

5 June 2012
Mwandishi Manyerere aliyefanya mahojiano haya akiwa na wanauamsho
Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano
*Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State', ijitawale yenyewe
*Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
*Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele
Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?

Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao, kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?

Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakataa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini.
Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.
JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?

Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale – wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawakukubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie

.
JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.

JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?

Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita "Dini na Siasa". Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa "siasa". Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni "uongozi", kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.

JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?

Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.

JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?

Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote – ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?

Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?

JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi – ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?

Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?

JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.

Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.

JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?

Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng'ombe na gari ya ng'ombe halafu ng'ombe ukamweka nyuma gari ya ng'ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.

JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?

Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang'ang'ania hiki tu!

JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?

Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.
 
Back
Top Bottom