Dada yangu anataka aachane na mume wake ila sioni sababu kuu

Macho kodo

Senior Member
Dec 22, 2016
122
127
Nilipata simu ya sista wangu mtoto wa baba mkubwa akaniambia dhamira yake kutaka kuachana na mume wake, kwa sababu yeye ana kazi nzuri na amefanikiwa kujenga nyumba ya ghorofa na mume wake kwa sasa hana kazi ana anamtegemea yeye kwa kila kitu, mume amekua hana kitu kwa takribani mwaka mmoja.

Ila yeye anadai amechoka kutegemewa kwenye kila kitu na hataki akaishi na mume wake kwenye nyubma yake aliyoijenga, tatizo la mumewe kubwa ndo baada ya mkwara ndo kafungua kibiashara ka ilimradi tu, aonekane ana kazi.

Sasa kwa kuwa na mimi nilishawahi kupoteza kazi na ku hastle muda mrefu nashindwa kumkubalia jambo lake coz najua hali kama hiyo ya kupoteza kazi msoto mtu anaoupitia wakati asipokua na kazi, coz jamaa nae alikua na kazi ila ndo hivyo ikaja bahati mbaya, hebu mpeni ushauri wadau.
 
Dah inasikitisha sana. Huyo Sista kaona status ya mume wake imeshuka, lakini ana sahau kua hata yeye kuna siku kibarua kinaweza ota nyasi. Wanawake wanapenda security sana lakini sio fair. Kama ameshaamua kumuacha msela mwache na maamuzi yake ila uhudhurie ufunguzi wa gorofa mpya utakuta kuna njemba huko inakata utepe kwa mkasi kufungua nyumba. I feel sorry kwa mshkaji usipokaa sawa unaweza ukawa chizi haya maisha. Ilishamtokea mzee mmoja kitaa alikua kama na 60s na mke mid 40s na watoto kadhaa daah tukasikia tu mzee kapigwa chini na yule maza kajenga bangaloo na ana mimba ya msela mwengine. Yule mzee mpaka leo hakutoa talaka ila ndo hivo wife anaishi maisha yake fresh tu na msela mwingine mzee yuko anauguza kiharusi na watoto wake. Life noma sana mazee.
 
Nilipata simu ya sista wangu mtoto wa baba mkubwa akaniambia dhamira yake kutaka kuachana na mume wake, kwa sababu yeye ana kazi nzuri na amefanikiwa kujenga nyumba ya ghorofa na mume wake kwa sasa hana kazi ana anamtegemea yeye kwa kila kitu, mume amekua hana kitu kwa takribani mwaka mmoja.

Ila yeye anadai amechoka kutegemewa kwenye kila kitu na hataki akaishi na mume wake kwenye nyubma yake aliyoijenga, tatizo la mumewe kubwa ndo baada ya mkwara ndo kafungua kibiashara ka ilimradi tu, aonekane ana kazi.

Sasa kwa kuwa na mimi nilishawahi kupoteza kazi na ku hastle muda mrefu nashindwa kumkubalia jambo lake coz najua hali kama hiyo ya kupoteza kazi msoto mtu anaoupitia wakati asipokua na kazi, coz jamaa nae alikua na kazi ila ndo hivyo ikaja bahati mbaya, hebu mpeni ushauri wadau.

HIYO NI LAANA KAKA KAMA NDO SABABU YA KUACHANA NA MME, MWAMBIE AMVUMILIE MWENZAKE BASI, AU AMPE MTAJI WAENDE SAMBAMBA, HUO UHURU ANAOUTAFUTA, MH HAUNA MAANA. ILA KAMA JAMAA NI MBABE ANAMPIGA, ANAMWONEA, ASIKII NA SI MWAMINIFU, HAPO LABDA!!!!
 
Dada yako haelewi kuwa Mungu anaweza kuleta rizki ya ndoa kupitia mikono yake yeye na mume anaweza kuondoka na hiyo rizki.
Kuna watu wanapenda UMIMI kuliko historia ya mafanikio yake. Kwa sasa hajui umuhimu wa mume wake lakini ipo siku atamtafuta kwa kisingizio cha watoto kumkumbuka baba yao na atalala huko huko ili akeshe nalo(na huo ndio umuhimu wa mume).
 
Kama ni muislamu huyo dada yako mwambie kabla hajamuacha huyo mume wake apitie kidogo kitabu cha Allah katika aya ya 103,akishamaliza kuisoma ndo aamue kumuacha,Na pili mwambie sie wanaadamu tunatakiwa tuamini yakuwa kupata na kukosa kwetu Allah ndo mpaji
 
Kichwa cha kuku hakistahiri kilemba.
Dada yako anaona akiwa na pesa hahitaji kua na mume asiyekua na pesa?
Jamaa anaweza kuondoka sawa ila Mungu ni wa ajabu kweli kweli, anaweza kupata mwanaume atakayomtendea atakumbuka jamaa yake wa mwanzo. Mali na kila kitu bado haviwezi kuzidi utu na thamani ya mke au mume uliyewahi kuishi nae.
 
Kuna vijiswali hapa

1.Dada yako aliolewa kipind tayar amepata kaz au kaipata kipind yuko ndan ya ndoa?
2.Kutokuwa kazin kwa shemej yako ni uzembe binafs au ilikuwa kwa namna nyengne?
3.Maisha ya nyumban kwenu ki ujumla ni wa kishua kapuku au average.
4.Dada yako amegusia chochote kuhusu kuwa na mahusiano mengne nje ya ndoa?
 
Back
Top Bottom