BLACK SUPERMAN
Senior Member
- Nov 28, 2013
- 158
- 195
Akiongea na mtangazaji Paul Thomas kwenye kipindi cha Kingstone Riddimz cha Safari FM ya Mtwara, Dabo alisema kuwa kuna baadhi ya redio huwezi kusikia muziki wa reggae zaidi ya kwenye kipindi cha Reggae peke yake.
“Kuna kuwa na kipindi cha Reggae lakini pia kuna kuwa na kipindi cha Hip Hop, kwahiyo kunakuwa na kipindi cha Reggae lakini pia kinaweza kuchezwa kwenye rotation nyingine regular hilo ndiyo tatizo kubwa. Kuna radio nyingine husikii kabisa reggae unasikia kwenye kipindi tu cha reggae tu peke yake,” alisema Dabo.