CV za CCM zinazowapa ushindi wa Kishindo!!!

CV za CCM zinazowapa ushindi wa Kishindo!!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
950
229968_517927984902080_952203736_n.jpg

Kazi ambazo mwanachama amekifanyia chama ni "ZIARA" za mwaka mzima, "matembezi ya Mshikamano" mwaka Mzima, kumsimika "Kamanda" mwaka mzima.
 
Ngoshwe,
Ukiiona ya Alhaj Bulembo aliyeshinda uenyekiti wazazi unaweza kuchanganyikiwa kabisa.
 
Ngoshwe,
Ukiiona ya Alhaj Bulembo aliyeshinda uenyekiti wazazi unaweza kuchanganyikiwa kabisa.

unamaanisha ni huyu aliyewahi kuwa refa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)???.

8431712.png

Jamaa amewalamba sana miguu xo mwacheni akomae na huo unaibu meya he deserve so
 
unamaanisha ni huyu aliyewahi kuwa refa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)???.

8431712.png

.......
Hujakosea mkuu. Ndiye huyo.
 
Tangu uchaguzi wa ndani ya ccm uanze msisimko umekuwa mdogo sana ndani na nje ya chama.na uchaguzi unavyoendelea ndiyo msisimko huo mdogo unazidi kufifia.kwa mfano,hadi muda huu matokeo ya jumuia ya wazazi hayajabandikwa kwenye jf ingawa yalijulikana tangu jana.
Hii ni hatari kupita kiasi.ina maana hakuna wanaccm humu jf.
Kwa taarifa tu aliyeshinda uenyekiti wa jumuia hii ana historia ya utapeli,wizi na hakuna ushahidi kama alimaliza hata darasa la saba.
 
CCM inazidi kuimarika,hii imedhihirishwa na chaguzi ndogo za madiwan zilizomalizika hivi juzi,pamoja na kelele nyingi bado wananchi wana iman kubwa na chama chao,mambo yaliyofanywa na ccm ni mengi na makubwa,na bado inasonga mbele,kikubwa zaidi ni utulivu wa nchi pamoja na watu wachache kutaka kuharibu utulivu kwa makusudi lakin serikali na vyombo vyake imekuwa imara sana.
Hongera mwenyekiti wa ccm na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kutupatia uongozi uliotukuka.
Barabara tunaziona,mahospitali,mashule,vyuo vikuu,viwanda na kupanuka kwa biashara vyote hivi ni juhudi zako
 
Tangu uchaguzi wa ndani ya ccm uanze msisimko umekuwa mdogo sana ndani na nje ya chama.na uchaguzi unavyoendelea ndiyo msisimko huo mdogo unazidi kufifia.kwa mfano,hadi muda huu matokeo ya jumuia ya wazazi hayajabandikwa kwenye jf ingawa yalijulikana tangu jana.
Hii ni hatari kupita kiasi.ina maana hakuna wanaccm humu jf.
Kwa taarifa tu aliyeshinda uenyekiti wa jumuia hii ana historia ya utapeli,wizi na hakuna ushahidi kama alimaliza hata darasa la saba.
Asante sana mtoa mada,huyu jamaaa namfahamu vizuri alianzia nimzaliwa wa kagera, bahati mabaya sana kaishia darasa la saba sijui ilikuwaje hata haja enda sekondari maana wahayawengi wameenda sekondari,akaanzia maishayake ya kubangaiza Musoma alikuwa akiuza nguo kutoka uganda anazisambaza kwenye maduka, badae ndo akajiunga na mabo ya mpira akapata uongozi, akaingia kwenye siasa akawa diwani, akahamia dar es salam na kuomba kuteuliwa kuwania ubunge akaanguka huyu ndiye mwenyekiti siyo wa wazazi wote bali wa ccm,je atafika au ni pandikizi lamtu na je pesa za kuhonga kazitoa wapi kama sio za mafisadi
 
:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa
 
Unajua wagoniwa wote wanapokaribia kufa afya zao huwa zinaimarika hivyo haishangazi kuwa afya ya mgonjwa ccm inaimarika pia.kifo kipo palepale na kwa muda uleule, kitanda kilekile na mgonjwa yuleyule.
 
Mtoa mada wewe ndo hujasoma,i guess ni mjinga wa mwisho,mtu kusoma si lazima asome kipindi kile unakijua wewe,jamaa kasoma kajiendeleza na ana shahada ya mambo ya siasa na uongozi,kuna vyuo vingi kwa sasa kama open university.usikalili mkuu
 
Bulembo?Si ndiye yy huyu kwenye miaka ya 1990 alikuwa anauza mboga mboga hasa mchicha kwenye kioski chake pale sokoni Musoma?

Kama ndiye yeye na leo kawa kiongozi wa kitaifa wa CCM basi nitashangaa sana!
 
Lakini mwisho wa siku sio cv ndo inayotupa kiongozi bora ingawa cv inaweza kutupa mwanga wa kiongoz bora! Kwa mtazamo wangu kua kiongoz tanzania haihitaji uwe na uwezo mkubwa sana wa kufikiria vitu vya utofauti sana. Sisi tunahitak kiongoz atakaetutolea matatizo yetu ambayo yako wazii na kila mtu anayajua na solution zake ziko wazi, kwa mfano

1. Tatizo la maji- kuchimba visima
2. Tatizo la umeme- kuongeza vyanzo vya umeme wa maji na upepo. Maja yapo na upepo upo.
3. Kuboresha usafiri wa miji na mikoa na wilaya, reli zipo ni marekebisho tu.
Na mengine mengi, hatuhitaj kiongoz atakaesababisha wanasayansi wetu waende mwezini au sijui tutengenez viwanda magar au compyuta. Tunahitaj viwand kama vya kubangua korosho tu!
 
hii cv inatia kinyaa. wenzio tumezoea cv zilizojaa mapulication. sasa hii ndo nini? bora asingeiweka tu hapa.
 
Mtoa mada wewe ndo hujasoma,i guess ni mjinga wa mwisho,mtu kusoma si lazima asome kipindi kile unakijua wewe,jamaa kasoma kajiendeleza na ana shahada ya mambo ya siasa na uongozi,kuna vyuo vingi kwa sasa kama open university.usikalili mkuu

Hivi kuhudhuria mkutano au kumsimika mtu ni kazi unayoweza kupimwa nayo eti umeifanya mwaka mzima? Yaani we unaweza kuandika kwenye wasifu wake mwaka wote wa 2010 ulihudhuria kikao cha NEC?? Pima kama kuna tija yeyote kwenye yaliyotajwa!
 
Back
Top Bottom