CV ya Patrobas mrithi wa John Heche BAVICHA

CV ya Patrobas mrithi wa John Heche BAVICHA

Ndo umekuja kumsafisha hapa?..Kwenda zako huko,huyo ni pandikizi tunamfahamu toka mwanzo!
 
Mleta mada umeandika maelezo ya huyo ndugu ila hujaandika wasifu wake
 
Makamanda habari za wakati huu..
Nimesikitishwa sana na baadhi ya watu ambao wamekua wakielezea ndivyo sivyo CV ya Mheshimiwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA )
Kulopoka ni uvivu wa kufikiri, tuache kuelezea mambo bila kuwa na ufahamu ama tafiti! Tukumbuke, "No research, no right to speak". Nafahamu ya kuwa miongoni mwetu huenda tuna kiu ya haki kutaka kufahamu ukweli juu ya wasifu wa kiongozi wetu mpya alierithi mikoba toka kwa John Heche, mwenyekiti aliemaliza muda wake. Lakini kiu hii isiwe ni chanzo cha kubuni na kusema tusioyajua kwa kina maana kufanya hivyo si uungwana hata kidogo.

Ukweli Ni Kwamba;

Mhe. PATROBASS, Paschal Katambi amekuwa mwana CHADEMA tangu 2005.
Baada ya kumaliza kidato cha sita alijiunga na Chuo Cha Mtakatifu Agustino na kujikita katika Sheria ngazi ya shahada ya kwanza naya pili katika sharia za UCHUMI.
Amekua mwanachadema mwaminifu tangu masomoni Sekondari, Chuo Kikuu hadi Kazini na kushiriki kazi zote za Chama na hata kushika na pia kushinda nafasi nyingi za uongozi katika kukijenga Chama bila woga kwani anajiamini na anamsimamo katika mambo ya msingi na utetezi wa haki na usawa kwaajili ya CHADEMA na taifa.

Anaaminika na anaheshimu watu wote, Ametumikia nafasi zifuatazo kwa Uaminifu, Uadilifu, tija na manufaa ya wengi toka s/msingi hadi chuo kikuu :- Kilanja, Chuo kikuu Serikali za wanafunzi- m/mkt Tume marekebisho katiba SAUTSO, Katibu Mkuu SAUTSO, MKt Kamati maalumu ya Sheria Umoja wa Marais wa vyuo vikuu Tanzania –Aliipinga kisheria na hoja Serikali kuondosha jina la Rais na Waziri vyuo vikuu, Akatetea haki ya kupiga kura wanafunzi 2010 hadi Mahakama kuu akiongoza jopo, Amekuwa Waziri wa Sheria, Mkt Tume ya Uchaguzi SAUTSO.

Kwa CHADEMA Amekua kiongozi tangu 2007 hadi leo katika nafasi mbalimbali za ujenzi na uhamasishaji kukuza Chama bila unafiki wala woga maana hana tabia ya kumuogopa mtu bali kuheshimu kwa kadri ya matakwa ya mila,tamaduni,desturi, sharia, taratibu na kanuni zinavyosema na matakwa ya wengi. Tangu 2007 hadi leo yeye ni kiongozi wa CHADEMA nafasi mbalimbali. Wenye akili na nia njema na chama chetu wanajua… nafasi aliyonayo sasa si ya mzaha,kuuzia sura wala kujifunzia uongozi ni nafasi ya kupanga na kutenda bila woga wala njaa.

Kuhusu kazi aliyokuwa nayo, hata makao makuu na uongozi wajuu CDM wanajua na amekifaa vipi chama na wanachama kwa ujumla. Ni mwanachama asietiliwa hata tone la shaka. Kulazimisha kumhusisha na Diallo ama CCM kwa kigezo alikua anafanya kazi hapo, wenye akili tunajua CHADEMA haina Viwanda, haina Makampuni, Haiongozi Serikali, hivyo wana CHADEMA wasomi na wasio wasomi watafanya kazi popote KWA MUJIBU WA SHERIA na si matakwa ya mwajiri (Ukiwa muislam ukaajiriwa na mkristo haikulazimu ubadili dini kwani haihusiani na itikadi hizo) Tuhukumu watu kwa ukweli na haki si kutumia elimu vibaya kupotosha na kupika maneno, CCM nawashirika wao ipo siku mtakwama na hakuna atakae ishi milele, kina Ghadafi na ubabe wao na uroho wa madaraka walifanya kila njia lakini mwisho ulifika.
Mwisho kabisa nasema, Tujenge hoja tujenge chama.
Na, MWANA WAKATI
hujui unachokisema unaropoka tu wewe. humjui gadafi na huna mamlaka ya kueleza historia yake wala hupaswi kuendelea kuropoka....aliyoyafanya gadafi kwa afrika na nchi yake hakuna anayeweza kukaribia hata robo...usikurupuke...acha ukibaraka. waliomuua gadafi leo hii wanajuta, laana imewapiga libya haina tena amani. watu wanamtaka ww unakuja na porojo hapa.
 
hivi jamani kwanini watu wanajifanya ni wajuaji kumbe mbele giza?? cv zinakuwaga hivi?? haya ambao hamkuogopa umande mtusaidie, sie tukisema tutaambiwa tunaongea uongo...
 
Ni vizuri kutujulisha' historia' yake. Tunashukuru. Sasa tunaomba weka CV. Kama hauna wasiliana nae akupe kisha uiweke hapa kwani inaonekana unamfahamu!
 
Naongezea,

PASCHAL K. PATROBASS, Alisoma elimu yake ya kidato cha 5-6 MALANGALI-IRINGA.

PASCHAL K.PATROBASS, Tumeajiriwa naye siku moja pale Sahara media, yeye aliajiriwa kama Mwanasheria wa Kampuni baadae kutokana na uwezo wake kampuni ikamteua kuwa MANAGER MSAIDIZI RASILIMALI WATU NA UTUMISHI.
 
hujui unachokisema unaropoka tu wewe. humjui gadafi na huna mamlaka ya kueleza historia yake wala hupaswi kuendelea kuropoka....aliyoyafanya gadafi kwa afrika na nchi yake hakuna anayeweza kukaribia hata robo...usikurupuke...acha ukibaraka. waliomuua gadafi leo hii wanajuta, laana imewapiga libya haina tena amani. watu wanamtaka ww unakuja na porojo hapa.

Nanusa harufu ya udini hapa, wewe huna lolote zaidi ya kuuwaza ule msikiti wa Dodoma uliojengwa na gadafi, nyie ndio yale mabakaji yanayotumia chakula kule somalia kwa lengo la kuwapata watoto wadogo. Ghadafi unayemsema wewe pamoja na mambo mengine aliendesha nchi kama nyumba yake hakuna kugombea udiwani wala uenyekiti wa mtaa,ndugu jamaa na marafiki ndio walijaa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi, kisa aliwapa wananchi fedha au unafuu lakini bila uhuru wa kukosoa? katika zama hizi?aliyofanya nje mengi ni udini na kusaidia magaidi mfano boko haramu, umesahau vita ya Idd amini au ulikuwa hujazaliwa?, wewe huna taarifa za gadafi hacha kuropoka hovyo.kinachotokea libya ni itikadi kali ya kiislam versus demokrasia, kila mtu anajua hilo(mwenye akili timamu lakini) mmekalia kuwasingizia wamarekani tu.
 
IVI MNAONIOMBA CV ya Mheshimiwa Mwenyekiti, ! MNATAKA MUMPE KAZI?

Sawa maafisa rasilimali watu ACT na CCM! nimewaelewa... Nawasamehe bure maana mmevurugwa tu na mfumo wa Elimu ya Kikoloni! CV ya mwanasiasa INAJENGWA NA HISTORIA YAKE, Juhudi na harakati ndani na nje ya Chama, katu haziandikwi kama za kuombea AJIRA. Naona wengi wenu ni wepesi vichwani na mna kungu la giza ila sii mbaya " Nayaacha magugu yamee pamoja na ngano".
 
Tanzania yangu niipendayo naiskitikia kwa kukosa watu hata wenye uwezo wa kuandika cv ya mtu what is cv? It is not story even history of somebody tafadhal tuwen na akl watanzania.
 
Nanusa harufu ya udini hapa, wewe huna lolote zaidi ya kuuwaza ule msikiti wa Dodoma uliojengwa na gadafi, nyie ndio yale mabakaji yanayotumia chakula kule somalia kwa lengo la kuwapata watoto wadogo. Ghadafi unayemsema wewe pamoja na mambo mengine aliendesha nchi kama nyumba yake hakuna kugombea udiwani wala uenyekiti wa mtaa,ndugu jamaa na marafiki ndio walijaa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi, kisa aliwapa wananchi fedha au unafuu lakini bila uhuru wa kukosoa? katika zama hizi?aliyofanya nje mengi ni udini na kusaidia magaidi mfano boko haramu, umesahau vita ya Idd amini au ulikuwa hujazaliwa?, wewe huna taarifa za gadafi hacha kuropoka hovyo.kinachotokea libya ni itikadi kali ya kiislam versus demokrasia, kila mtu anajua hilo(mwenye akili timamu lakini) mmekalia kuwasingizia wamarekani tu.

Hata wewe una elements za udini!Unaposema wamezoea kuwasingizia wamarekani unamaanisha akina nani!
 
Hata wewe una elements za udini!Unaposema wamezoea kuwasingizia wamarekani unamaanisha akina nani!

kuna mtu ambaye si mdini?, basi mpagani!! huwezi kuniambia kuwa unaswali kila siku alafu ukawa kinara wa kuvunja amri10 za mungu,wewe ni mgeni wa mijadala humu JF? kila mtu ni mdini isipokuwa dini isiingie kwenye mifumo ya kiserikali,unataka kujifanya hujui kuwe watu wenye upeo finyu(hasa kutoka Africa) ndio vinara wa kusingizia wamarekani eti tu kwa kuwa ndugu zao(wenye imani sawa) wanapigana?
 
Paschal Patrobas tuwekee jina la ukoo. Umeshakuwa mtu mkubwa sasa jina la ukoo ni muhimu. Hayo kizungu ebu yaongezee heshma
 
kuna mtu ambaye si mdini?, basi mpagani!! huwezi kuniambia kuwa unaswali kila siku alafu ukawa kinara wa kuvunja amri10 za mungu,wewe ni mgeni wa mijadala humu JF? kila mtu ni mdini isipokuwa dini isiingie kwenye mifumo ya kiserikali,unataka kujifanya hujui kuwe watu wenye upeo finyu(hasa kutoka Africa) ndio vinara wa kusingizia wamarekani eti tu kwa kuwa ndugu zao(wenye imani sawa) wanapigana?
Tuendelee na mjadala wa mrithi wa Heche
 
Back
Top Bottom