puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 1,057
- 2,195
Neno customer care, sio neno geni masikioni mwa watu wengi. Lakini pia ni kiungo muhimu sana katika biashara. Kwa lugha yetu ya nyumbani tunaita "Huduma kwa wateja".
"Huduma kwa wateja ni mfululizo wa shughuli iliyoundwa ili kuongeza kiwango cha mteja kuridhika - yaani, hisia kuwa bidhaa au huduma imekutana na matarajio ya mteja.
Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa walio wengi katika jamii yetu...sio sekta binafsi wala sekta ya umma. Watu wamekuwa wakifanya huduma kwa mazoea wakidhani kuwa na biashara ni uwepo wa bidhaa pekee bila kujali ubora wa huduma inayotolewa.
Hili limekuwa ni tatizo linalodhohofisha kama si kuua kabisa biashara nyingi sana hapa nchini.
Miongoni wa jamii yetu zipo biashara nyingi zinazotuwezesha kujikimu na maisha yetu ya kila siku...mfano: Biashara ya vyakula, Vinywaji, Usafirishaji, Maduka ya dawa, Huduma za Afya, Mavazi, Vifaa vya electric (Accessories) n.k
Sasa wakati Mtu/Kikundi au Taasisi inapoanzisha biashara hujitahidi sana kuwa na huduma nzuri ( Custumer care) ili kuweza kupata wateja, cha ajabu na kusikitisha akisha pata wateja anasahau kabisa kilichowafanya waje pale ni ubora wa bidhaa lakini pia huduma bora aliyokuwa akiwapatia.
Matokeo yake anaanza kujenga kiburi na dharau kiasi cha kujisahau kama anapaswa kutoa huduma bora kama aliyokuwa akiitoa mwanzo ikiwezekana iwe zaidi ya hapo. Yeye kufanya kwa mazoea akiamini hawezi kupoteza wateja kwa kudanganyika na wingi wa idadi ya wateja alio nao. Huo ni upofu wa mawazo ulio katika kiwango cha hali ya juu.
Matokeo yake biashara hufa na kuanza kulaumu watu, zaidi hata kusubutu kuhisi huenda ikawa amefanyiwa mambo ya kishirikina jambo ambalo lipo kwenye akili za watu wengi miongini mwetu.
Tukiangalia kwenye sekta ya umma, wapo watu waliowekwa kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali ili kuweza kuwasaidia wananchi lakini pia kuhakikisha serikali inaingiza pato kupitia hiyo biashara au mradi unaoendeshwa.
Matokea yake ndio wamekuwa vinara wa kutoa Lugha chafu kwa wateja, Kutojali muda kwa Wateja lkn pia usimamizi mbovu katika kuhakikisha wateja wanapata huduma. Lawama hizi ziende katika idara zifuatazo:
1. DART (Mwendokasi)
2. Huduma za Afya (Hospital na Zahanati)
3. Sekta ya Elimu (Mashuleni)
4. Wahudumu katika vivuko.
Maeneo haya serikali wapaangalia kwa jicho la tatu kwani watoa huduma hawaba weledi kabisa katika kazi yao...yamekuwa ni kero kubwa katika jamii.
Sent using Jamii Forums mobile app