CUF Yatangaza Maandamano Makubwa Dar es Salaam

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Wanawake wa chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mh Severena Mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu za CUF Buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu

Amesema kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni kina mama na watoto hivyo wameona ni bora kufikisha kilio chao hicho kwa makamu wa Rais ambaye ni Mwanamke mwenzao awasaidie.

Maandamano hayo yatapita barabara ya uhuru, ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Karume, Kariakoo, Mnazi mmoja, Central polisi, barabara ya sokoine , Bandarini, mahakama kuu, mahakama ya ardhi hadi ofisi ya makamu wa Rais.

Maandamano hayo bado hayajaruhusiwa na polisi licha ya polisi kupata barua kutoka CUF.
 
Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    27.6 KB · Views: 65
Ni busara kushiriki uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao badala ya kutafuta uhasama na vyombo vya dola,Matokeo yake ni kuumizwa na kuuguza vidonda peke yako bila hilo kundi kuwepo.Kwa jinsi CUF ilivyo na wafuasi wengi Zanzibar kama tulivyoaminishwa ni wazi sanduku la kura ndiyo suruhisho.
 
CUF wanaponzwa na UKAWA.... Hakuna maandamano yatakayo ruhusiwa..!

CUF na Chadema ni vyema mkamuuliza Lipumba kilicho tokea baada ya kukaidi agizo la jeshi la Polisi.
 
Ni busara kushiriki uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao badala ya kutafuta uhasama na vyombo vya dola,Matokeo yake ni kuumizwa na kuuguza vidonda peke yako bila hilo kundi kuwepo.Kwa jinsi CUF ilivyo na wafuasi wengi Zanzibar kama tulivyoaminishwa ni wazi sanduku la kura ndiyo suruhisho.
kwanini ule wa mwanzo ulifutwa ?
 
Kwa nini wasiende kuandamania Zanzibar kwenye ofisi za Jecha?

Wawe makini tu polisi nao wanataka kupandishwa vyeo so wanatafuta scenes za kuonesha uchapakazi wao kwa rais kama DC wa Iringa.
 
K
Wanawake wa chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mh severena mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu

Amesema kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni kina mama na watoto hivyo wameona ni bora kufikisha kilo chao hicho kwa makamu wa Rais ambaye ni Mwanamke mwenzao awasaidie.

Maandamano hayo yatapita barabara ya uhuru,ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam,karume,kariakoo,mnazi mmoja,Central polisi,barabara ya sokoine ,Bandarini,mahakama kuu,mahakama ya ardhi,Hadi ofisi ya makamu wa Rais.

Maandamano hayo bado hayajaruhusiwa na polisi licha ya polisi kupata barua kutoka CUF.

Chicken heads. Kama mlizoea JK akisema mnatikisa kiberiti kwa JPM mmekanyaga waya. Rais amesema katiba haimruhusu kuingilia zec. Wake up!
 
Ni busara kushiriki uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao badala ya kutafuta uhasama na vyombo vya dola,Matokeo yake ni kuumizwa na kuuguza vidonda peke yako bila hilo kundi kuwepo.Kwa jinsi CUF ilivyo na wafuasi wengi Zanzibar kama tulivyoaminishwa ni wazi sanduku la kura ndiyo suruhisho.
Ure not serious
 
haa haa mambo ya zanzibar maghufuli hayamuhusu. dikteta magu andaa polis wa kuzuia maandamano hayo haraka...
 
Ni busara kushiriki uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao badala ya kutafuta uhasama na vyombo vya dola,Matokeo yake ni kuumizwa na kuuguza vidonda peke yako bila hilo kundi kuwepo.Kwa jinsi CUF ilivyo na wafuasi wengi Zanzibar kama tulivyoaminishwa ni wazi sanduku la kura ndiyo suruhisho.
Kura zilishapigwa tarehe 25/10/2015
 
Back
Top Bottom