CUF yasambaratika Tanga:Mamia ya wanachama wajitoa chama hicho


Mkandara ingawa unaongozwa na nguvu ya kishabiki, lakini jitahidi usipoteze na uwezo wako wakufikiri...! Au hujui siasa? Hifadhi maneno yako!

Kwa kukuhakikishia tu CUF haijatikisika achilia mbali kusambaratika, usivutiwe na "matukio" huo ni upepo wa kisiasa tu unapita! Hata n'gombe akichinjwa haachi kupiga mateke (hicho ni kifo cha Hamad Rashid)! Hao wanachama unaoskia wanahama CUF hawana athari yoyote kwa CUF, utaskia mengi kipindi hiki kuhusu CUF, kama tulivyoskia alipoondolewa Mapalala, Jidawi na wenzake! Is a matter of time...wataondoka, kisha watafututika katika medani za siasa CUF itabaki pale pale!

Vyama vya siasa Tanzania haviishi kwa nguvu ya wanachama, bali wapenzi wa vyama hivo na ndio wanaovipigia kura! Wengi wa wanachama wa vyama vya siasa, wameingia kwenye vyama vya siasa kimaslahi zaidi (kuchumia tumbo), na pindi maslahi yao yanapokuwa mashakani au kubanwa, ndo utaona wanatafuta pakutokea! Wenye uchungu wa kweli na vyama vya siasa (wasio na maslahi yoyote), ambao wapo kwa ukombozi wa nchi, wengi wao si wanachama (ni wapenzi na washabiki tu)! Hio ndo siasa ya Tz we Mkandara!

Wakishaondoka Hamad Rashid na wenzake..CUF ndo itazidi kuwa imara! Ni wachache sana, ndo maana hawana nguvu ya kuuondosha uongozi wa uliopo madarakani, kama wangefika hata nusu tu ya wajumbe wa wabaraza kuu basi wangeshafanya mapinduzi! Lakini hawajai hata kikombe cha kahawa! Hivi sasa wanapata publicity sababu vyombo vingi vya habari vimenunuliwa na HR au vinamaslahi katika kukuza mgogoro (usiokuepo)! Hata "kikombe cha babau" kiliponya UKIMWI, KISUKARI na magonjwa yote SUGU kwa nguvu za VYOMBO VYA HABARI!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…