CUF yasambaratika Tanga:Mamia ya wanachama wajitoa chama hicho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yasambaratika Tanga:Mamia ya wanachama wajitoa chama hicho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Feb 27, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mzimu wa kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, na wenzake 10, umezidi kukiandama Chama cha Wananchi (CUF), baada ya wanachama wake 136, mkoani Tanga, akiwamo aliyegombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na 2010, Mohammed Salim Siu, kujitoa katika chama hicho.

  Habari zilizolifikia NIPASHE jijini Dar es Salaam kutoka Tanga zinaeleza kuwa Siu na wenzake walifikia uamuzi huo baada ya kurejesha kadi za CUF katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika jengo la Makorora Community Centre, mjini humo jana.

  Uamuzi huo ulifikiwa na Siu na wenzake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kile walichodai kuwa ni kuchoshwa na migogoro ndani ya chama isiyokuwa na ufumbuzi wa busara kiasi cha kusababisha wanachama kukikimbia chama kutokana na maamuzi yasiyoheshimu mawazo ya wanachama.

  Sababu nyingine zimetajwa kuwa ni vitendo vya kufukuzana katika chama kwa shinikizo la Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, bila sababu za msingi pamoja na ukimya wa Mwenyekiti Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, juu ya mgogoro mkubwa uliopo ambao haujawahi kutokea katika chama.
  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Siu alisema sababu nyingine iliyowafanya wafikie uamuzi huo, ni kushuka kwa kiasi kikubwa kwa utendaji na mvuto wa shughuli za chama.
  Alisema sababu nyingine ni kutokuwapo kwa haiba ya chama, kukithiri uzembe kwa viongozi, ubabe na matusi kwa wanachama na kuwavunjia heshima waasisi wa chama.
  Sababu nyingine alisema ni matumizi mabaya ya fedha za chama, kutowekwa wazi mapato ya chama, wanachama kutoambiwa kiasi cha fedha kilichomo kwenye akaunti za fedha za kigeni na nje ya nchi ."Anayejua ni Katibu Mkuu peke yake," alisema Siu.

  Alisema sababu nyingine ni ubadhirifu wa mali za chama na upendeleo wa wazi kati ya Tanzania Bara na Zanzibar katika mgawo wa fedha.
  Siu alisema sababu nyingine iliyowafanya kuihama CUF inatokana na kiapo cha Maalim Seif kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

  Alisema katika kiapo hicho, Maalim Seif aliapa kwamba, atailinda Katiba ya Zanzibar, kutokutoa siri za SMZ, kumtii Raisi wa Zanzibar.
  Siu alisema kwa viapo hivyo, ni dhahiri kuwa Maalim Seif kamwe hawezi kufanya kazi ya CUF yenye dhana ya kutetea demokrasia na haki kwa Watanzania.

  "Ndio maana akaambiwa wasipeleke mgombea ubunge Arumeru Mashariki ili CCM ishinde kirahisi na kuambiwa wasiunge mkono chama chochote cha upinzani," alisema Siu.

  Aliongeza: "Hizi ni dalili kuwa CUF haipo tena katika ushindani wa vyama vyenye nia ya kuwakomboa Watanzania na kwa mantiki hiyo ni wazi CUF ni kibaraka wa CCM na ndio maana wameisaidia CCM ishinde katika Jimbo la Uzini Zanzibar."

  "Nimetafakari kwa kina sana juu ya mwenendo wa chama chetu cha CUF na hatma yake hasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Chama chetu chini ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad wameshindwa kutoa dira ya chama, tumetoka wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi," alisema Siu.

  Alisema mbali na hilo, chama kimeshindwa hata kutoa mkono wa pole kwa wagombea wake wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo wa 2010 na kwamba hali hiyo imewakatisha tamaa wagombea na imeonyesha CUF haijali wagombea wake japo walifanya kampeni kama wagombea binafsi.
  "Hii inaonyesha kuwa chama kimekosa malengo na muelekeo," alisema Siu na kuitaja sababu nyingine iliyowafanya kufikia uamuzi wa kujitoa CUF, ni ubaguzi wa Maalim Seif miongoni mwa wanachama wa Tanzania Bara na Zanzibar.

  Alidai wengi walioajiriwa katika CUF ni Wazanzibari, huku Ofisi Kuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, ikiwa ina wanachama kutoka makabila mengine. Siu alidai makao makuu ya chama Zanzibar hakuna ofisi ya mwenyekiti wakati Tanzania Bara kuna ofisi ya Katibu Mkuu na ya Makamu Mwenyekiti.
  Aliongeza: "Kwa sababu hizo hapo juu, kuanzia sasa mimi si mwanachama wa CUF kwa sababu ya kauli mbiu ya 'CUF ni kwa ajili ya Seif Sharif Hamad' na sio kwa ajili ya Watanzania."

  Alinukuuu kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, aliyokaririwa na kituo kimoja cha televisheni nchini kwamba, kushindwa kwa CUF katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika Jimbo la Uzini, hivi karibuni, kulitokana na Wabara na Wakristo wanaoishi jimboni humo.
  "Kauli hiyo hakuna kiongozi wa CUF aliyeikanusha. Hivyo, maneno hayo ya Jussa ni ya CUF. Nawaomba Watanzania wazinduke na kujitoa CUF sababu ni chama cha kibaguzi," alisema Siu.

  Naye Abdallah Salim (Daiyadaiya) aliyejitambulisha kuwa ni muasisi wa CUF Tanga, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka Tanga jana, alidai Maalim Seif alitumia Sh. milioni 500 alipogombea urais Zanzibar wakati Profesa Lipumba aliyewania kiti hicho katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipewa Sh. miloni 70 tu kuzunguka nchi nzima.

  Alisema CUF imekosa mwelekeo kwa sasa na ndiyo maana hata uchaguzi mdogo wa mwakilishi Jimbo la Uzini imeshindwa kushika nafasi ya pili na kuzidiwa na Chadema.

  Hata hivyo, wanachama hao ambao hawakueleza wanakusudia kujiunga na chama gani, badala yake walisisitiza kuwa kuondoka kwao CUF ni mwanzo wa kukiua chama hicho mkoani humo kwani tayari kuna wanachama wengine kutoka matawi mbalimbali wameahidi kuwafuata.


  SOURCE:NIPASHE
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  rudini CCM kwa kuwa nyie sio wapinzani
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hamad Rashid kazini
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  karibuni chama makini
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Warudi ccm
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Haya CHADEMA vuneni wanachama hao Tanga. Acheni negativity kwao.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wozoza,

  Mlimfukuza wenyewe haya ndiyo matunda yake.


   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ametubomoa sana sisi wanamuafaka CCM B
   
 9. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Eti nini? nakubalianna zaidi na comment ya Osokoni na Kachanchabuseta kuliko hiyo yako Narubongo
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Binafsi yangu nafikiri hawa viongozi wa CUF Tanga wanatakiwa kwanza kufanya ushauri na wanachama wengine ili Maalim Seif Hamad na vibaraka wake ndio wavuliwe madaraka ndani ya CUF na pengine hata kufutiwa uanachama badala ya wao kukimbia matatizo. Mageuzi ya kweli yanaanza na watu wenyewe kudai na kufanya mabadiliko na sio kuyakimbia matatizo maana Seif sio Mungu halafu hutakamilisha nia na dhamira ya uanachama ikiwa mtajiunga na chama kingine. Sababu zote zilizoelezwa zinamvua mtu yeyote uongozi na Uanachama acha mbali kabisa maswala ya unafiki na ushabiki..

  Ni ushauri wangu kwamba baada ya Hamad Rashid kuonekana mshindi ktk sakata hili na mtu ambaye anakubalika sana kwa wananchi na wanachama wa CUF mnatakiwa kufanya mabadiliko wenyewe na sio kukimbia. Nina hakika na matumaini zaidi na Hamad Rashid na Prof. Lipumba wakiwa pamoja kisha mjenge mseto baina ya CUF na Chadema kuondoa zile tuhuma za udini pande zote basi mwaka 2015 CCM hawataona ndani wala nje hata kama NEC itakuwa iliyopo leo. Pingamizi kubwa la muafaka wa Chadema na CUF alikuwa Maalim Seif na maadam mnaweza kabisa kumwondoa kibaraka huyo basi ushindi upo mbele yenu kwa maamuzi madogo sana - Ondoweni vibaraka hawa ndani ya chama na muunde muafaka mpya na CDM ili kuiondoa CCM madarakani..
   
 11. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kuna taarifa zipo hapa mtwara mjini kwamba aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CUF mwaka 2010 mr. Uledi amejitoa CUF.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni ushauri mzuri sana. na kama wana hiyo nguvu wanayosema kuwa wanayo, haitakuwa vigumu kuwaondoa wale wanaoamini kuwa wanakiharibu chama
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hiyo nguvu wanachama wa CUF wanayo sana isipokuwa maajabu ni kwamba wao wameaachia hawa wahuni wachache kuonyesha wana nguvu kuliko sauti ya wanachama. Haya ndio makosa tunayotumia sisi wote, yaani tunakubali kuendeleshwa na watu wachache sana kutokana na zile fikra za Ukomunisti kuogopa viongozi wa chama. Enzi za Nyerere jamani zimekwisha, huu ni wakati tofauti kabisa wananchi ndio waloshika dume la karata..

  Mfumo ule haupo tena na maana ya demokrasia ni kwamba chama ni cha wananchi na wao ndio waajiri wa viongozi ndani ya chama sio kuhofia Ukomunist wa kina Lenin na Mao Tze Tung. wanachama wengi sana CUF bara na visiwani hasa Unguja hawampendi Seif kwa sababu wameshakuwa na experience mbaya naye akiwa waziri kiongozi na pia waziri wa elimu. Wanamjua vizuri zaidi kwa hiyo mageuzi yaanze ndani ya chama na sio kukimbia chama. CUF wanaweza kabisa kuwa chama kile kilichokuwa mwaka 2000 hasa wakionyesha nia ya kumwondoa CCM kwa kuunganisha nguvu na CDM.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Profesa Lipumba ameshindwa kutumia usomi wake kukisaidia chama hiki matokeo yake yeye anadhani neno mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano ni sehemu ya jina lake la ubini!!
   
 15. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ichambue vizuri hiyo taarifa ya huyo mbunge aliyejitoa CUF, JARIBU KUFUATILIA VIZURI KAMA UPO KARIBU.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hakuna sababu ya kumchambua mtu au habari ikiwa sisi wote tunaijua habari hii kuwa na ukweli japokuwa hatupo CUF. Madai yote yalosemwa yapo kweli na tunayajua yapo hii ilikuwa kuonyesha tu kilichowakera wao. naomba kichwa cha mada hii kibadilishwe na kusema - CUF YASAMBARATIKA!
   
 17. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wamechelewa kutambua ukweli lakini karibu nyumbani
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Chama huwa kinazaliwa,kinakua,kinazeeka na mwishowe kifo! ....
   
 19. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  RIP CUF....sisi tulikupenda sana! ila mungu amekupenda zaidi na ameamua kukuchukua jumla!
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa! jina la Bwana lihadimiwe daima na milele.
   
 20. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ukimuacha mtatiro, ni kiongozi gani amebaki katika hiki chama kwa upande wa bara anayeeneza chama.
   
Loading...