CUF yapinga polisi kushikilia viongozi wao bila kuwashtaki.


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,677
Likes
51,856
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,677 51,856 280
32a0fe0cba698dfe11853e4712a827a5.jpg

Chama cha wananchi (CUF) kimelitaka jeshi la polisi kuwapandisha mahakamani viongozi wake wanaowashikilia kwa tuhuma za uchochezi kisiwani pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa jana, mkurugenzi wa habari na mawasiliano ya umma wa chama hicho, Salim Bimani , alisema kama polisi wana ushahidi wa viongozi wa CUF na wafuasi wao kujihusisha na matukio ya uvunjifu wa amani basi wawapeleke mahakamani.

Bimani alisema wanasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kuwaweka ndani viongozi na wafuasi wao kwa muda mrefu bila ya kuwafikisha mahakamani kinyume na haki za binadamu.

Bimani alisema kuwa tokea kuanzishwa mfumo wa vyama vingi Tanzania kumekuwa na unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya raia hasa wanachama wa CUF jambo ambalo alisema kuwa linafanyika kwa nia ya kukikandamiza chama hicho.

"Ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo kila wakati Zanzibar imekuwa ikishuhudia kuletwa askari wengi katika kipindi cha uchaguzi "alisema Bimani.

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa oktoba 25.2015 kumekuwa na hatua kadhaa za unyanyasaji dhidi ya wafuasi wa chama hicho unaofanya na vyombo vya usalama.

Hata hivyo tunawaambia viongozi wa CCM na pamoja na vyombo vya dola tutaendeleza msimamo wetu wa haki sawa kwa wote, alisema Bimani.

Chanzo :Gazeti Nipashe
 

Forum statistics

Threads 1,239,181
Members 476,441
Posts 29,344,923