CUF yapinga kauli ya Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yapinga kauli ya Tendwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 26, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Raphael Kibiriti

  25th June 2012

  [​IMG]

  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa

  Chama cha Wananchi (CUF) kimeituhumu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na mkakati wa wazi wa kuvisajili vyama dhaifu kwa lengo la kuwa na utitiri wa vyama ambavyo huishia kuwa mawakala wa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi.

  Chama hicho kimetoa msimamo huo kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Julius Mtatiro kikijibu kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuwa atavifuta baadhi ya vyama alivyoviita kuwa ni vya mfukoni.

  Katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa facebook, Mtatiro alisema kuna makusudi ya wazi yanayoambatana na ujanja na hadaa kubwa zinazofanywa na ofisi ya Tendwa kuhakikisha vyama dhaifu na visivyo na vigezo vinasajiliwa.

  "Chanzo cha kuwepo kwa vyama vya siasa vya mifukoni ni yeye mwenyewe msajili na kauli yake ya kutaka kuvifuta vyama hivyo inamsuta, haitekelezeki na inamtia aibu. Leo msajili wa vyama anazunguka kuwahadaa Watanzania kuwa atavifuta vyama hivyo ni uzushi na uongo mkubwa," alisema.

  Aidha, Mtatiro aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na Bunge kuichunguza ofisi ya msajili, kutokana na kuwepo kwa mashaka na viashiria vya ufisadi wakati wa usajili wa baadhi ya vyama vya siasa vya mifukoni.

  Akiwa mjini Dodoma hivi karibuni, Tendwa alisema wakati umefika wa kuvifuta vyama vyote vya siasa ambavyo havina tija kwenye siasa za nchi huku baadhi yake vikishindwa kutoa mwakilishi hata mmoja kwenye ngazi ya ubunge na serikali za mitaa.

  Tanzania ina vyama 19 vyenye usajili ya kudumu, lakini kati ya hivyo ni vyama vinane vyenye uwakilishi katika ngazi ya ubunge na serikali ya mitaa.Vyama hivyo, ni CCM, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi. Vingine ni UDP, TLP, Chausta na PPT-Maendeleo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,905
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Mtatiro yupo sahihi, ila mahala aliposimamia ndo panamlet down
   
Loading...