CUF yamvaa Prof. Muhongo

CUF yamvaa Prof. Muhongo

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,342

BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF), limemvaa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kumtaka aueleze umma wa Watanzania sababu za kukatika umeme, hususan katika Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema wakati umefika kwa umma kujua ukweli kuhusu kile kinachotokea na si vinginevyo.

Alisema baraza hilo limemtaka waziri huyo kutoa ufafanuzi kutokana na kauli zake za awali za kusisitiza hakutakuwa na mgawo wa nishati hiyo muhimu, lakini taifa linashuhudia mgawo wa kimya kimya kila kukicha.

"Pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo kuwaeleza Watanzania kuwa hakutakuwa na mgawo na kwamba mgawo kwa sasa itakuwa ndoto, bado maeneo mengi ya nchi yetu ikiwemo Jiji la Dar es Salaam hali ya umeme si ya kuridhisha hata kidogo.

"CUF inamtaka Waziri wa Nishati na Madini kuwaeleza Watanzania nini tatizo la msingi juu ya suala la kuendelea kwa mgawo wa umeme kinyemela," alisema Prof. Lipumba.


Aidha, alisema CUF inapinga mpango wa TANESCO kuongeza bei ya umeme na badala yake kuitaka serikali kuona umuhimu wa kuwa na mpango wa uhakika wa kuhakikisha tatizo la umeme linakwisha na Watanzania wengi wananufaika na huduma kulingana na gharama zinazoendana na hali za maisha yao.

Akizungumzia suala la michango kwa wanafunzi wanaoanza shule za msingi nchini, Prof. Lipumba alisema licha ya serikali kutangaza utoaji wa elimu ya msingi bure, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la michango na kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati suala hilo, kuhakikisha kuwa amri ya kutowachangisha wazazi michango hiyo inasimamiwa kwa vitendo.


[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
CUF yamvaa Prof. Muhongo

na Shehe Semtawa
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
 
Akili za kuambiwa changanyeni na zenu,Kama Muhongo aliwaambia hakutakuwa na mgawo leo basi nawakumbusheni kwamba Mhe.Rais Kikwete alisema mgao wa umeme mwisho 2015...kama ni mchambuzi wa mambo utagundua alilenga nini wala huhitaji kuita press conference kuuliza hilo.Anyway najua CUF mlizimwa sasa sijui ndo mmewaka au mpo likizo kwani wenzenu CHADEMA wanawaka kila kona!
 
Back
Top Bottom