CUF Yamalizeni na Hamad Rashid Arudi

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
Kwa maneno machache kabisa ili kuenzi siasa za Tata Mandela napendekeza CuF wamsamehe Hamad Rashid na arufishiwe uwanachama wake ili kujenga uimara uchaguzi ujao.
Ni mgongano wa kimawazo tu ndio ulo sababisha yeye kutimuliwa siamini kuwa ni msaliti.
HAMad Rashid ni nguzo muhimu sana bungeni na ni mtu asie na jazba katika kujenga hoja na amekikitetea chama chake kwa uwedi mkubwa katika majukwaa na midahalo mbali mbali. Naweza kusema hakuna mtu mahiri katika CUF anaye mshinda Rashid kuisimamia CUF
Nakumbuka mdahalo wake na mbowe ITV namna alivo simama imara kupangua masuali yote kwa ufasaha mkubwa sana
Maalim seif najua unapita huku jamii forum kama hupitii basi wakupe ujumbe ya kwamba lililopita si mdwele tugange ya mbele.Rashid mmetoka mbali sana mlikua pamoja katika kkundi la vijana mliokua mkipinga msimamo ya Ccm kuhusu muungano ,mlifukuzwa Ccm nyote pamoja na pia mlipata vipigo pamoja
Onesha ukomavu wa kisiasa kama mandela alivo wasemehe maadui zake waliomtesa na kumdhalilisha na kuua watu wake na kusambaratisha familia yake. Wewe mwenyewe umufungwa na kuteswa na Ccm umedhalilishwa lakini umekubali kusamehe na kufanyakazi nao tena ukiwa chini ya Ukuu wao. Vipi ikushinde kuanzisha upatanishi na nduguyo mloteswa pamoja ?
Mtafute muungee Man to Man myamalize
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
Hivi kumbe huyu alifukuzwa uanachama .mbona CUF haina demokrasia hii

Sio kuhusi democrasia matatizo ya vyama vyote hivi ni maslahi kulinda maslahi ya kibinafsi kama ilivo kwa cdm mambo ya uchaguzi na ruzuku na yeye alitaka Maalim aachie ukatibu ili watu wengine wagombee kama kina Zitto.
Ndio maana namwambia Seif Sharif be a Man na amwite wayamalize na kea hilo Cuf itapanda chati sana
Waondoe kinyongo
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,133
1,225
Sio kuhusi democrasia matatizo ya vyama vyote hivi ni maslahi kulinda maslahi ya kibinafsi kama ilivo kwa cdm mambo ya uchaguzi na ruzuku na yeye alitaka Maalim aachie ukatibu ili watu wengine wagombee kama kina Zitto.
Ndio maana namwambia Seif Sharif be a Man na amwite wayamalize na kea hilo Cuf itapanda chati sana
Waondoe kinyongo
Kwani CUF imeshuka chati?
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,121
2,000
anayesamehewa ni yule aliyekiri makosa yake , akatubu na kuomba msamaha , sasa huyu badala ya kufanya haya akakimbilia mahakamani ! ambapo sasa amekuwa MBUNGE WA JIMBO JIPYA LA UCHAGUZI LA KISUTU KWA TIKETI YA ADC , mwacheni achinjiwe baharini .
 

Royals

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,446
1,500
woote mmekosea. huyu anachukua nafasi ya makamu mwenyekiti chadema.
 

Mr. Mpevu

Senior Member
Oct 26, 2012
138
250
kwa kweli usilolijua ni usiku wa kiza. Mngelijua nini kiko nyuma ya mgogoro huu wa Hamad Rashid na CUF usingesema hayo uyasemayo ya msamaha. Siasa ni mchezo mchafu kama inavyosemwa na hao wanasiasa wenyewe.
 

Mzee Wa Sumu

JF-Expert Member
Apr 17, 2013
643
0
Nukuu makamo m.kiti cuf mzee machano alisema ktk mkutano manzese ukishatoka ktk cuf hurudi hamad aende ktk chama chake cha adc au amfuate pinda swaiba wake machano alifungwa uhaini na hamad kutoka jela mkapa kamteua mbunge hamad hujiulizi hupati jibu hapo
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
Nukuu makamo m.kiti cuf mzee machano alisema ktk mkutano manzese ukishatoka ktk cuf hurudi hamad aende ktk chama chake cha adc au amfuate pinda swaiba wake machano alifungwa uhaini na hamad kutoka jela mkapa kamteua mbunge hamad hujiulizi hupati jibu hapo

Mkuu kama mandela alisamehe so inawezrkana
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
Cuf na hamad Rashid biashara imekwisha, nyie malizaneni Zitto.

Kama cuf iko hivo basi mtaendelea kuambulia umakamu wa rais mpaka Seif azekee nusu ikulu na yeye madam anafungiwa na kufunguliwa milango ya gari kashafika mtabaki kupiga kelele tu
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,750
2,000
Habari za kuaminika hamad wawili wamekutana na kuna uwezekano mkubwa hamad rashid akarudishiwa kadi ya chama na kuwa mgimbea mwenza
 

albuluushiy

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
1,365
2,000
Habari za kuaminika hamad wawili wamekutana na kuna uwezekano mkubwa hamad rashid akarudishiwa kadi ya chama na kuwa mgimbea mwenza

ndugu yangu maana kwa kweli we undugu yangu maana ni wa jazira mwenzangu ila nakuomba hili suala la hamad rashid ulichukulie very sensitive coz sote tunatamani hamad rashid arudi kundini so ukisema wamekutana una uhakiki gn?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom