CUF yajitoa rasmi UKAWA, 2020 kusimamisha mgombea wa Urais

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
982
723
Baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kusimamisha wagombea udiwani kwenye Kata 14 kati ya 20 katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Januari 22,2017 Tanzania Bara na Baraza Kuu la Uongozi Taifa kukataa kusimamisha wagombea na kuiachia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusimamisha katika kata zote kwa madai ya chama chake kuwa na mgogoro wa viongozi.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma CUF anayetambuliwa na Lipumba, amesema kuwa kwa sasa shughuli zao zimejikita kukijenga chama hicho na si UKAWA kwa kuwa dhamira ya chama hicho ni kushika dola mwaka 2020.

Kambaya ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi huu, ambapo ametaja sababu ya vyama vya upinzani kushindwa katika uchaguzi huo, ni vyama hivyo kuishiwa nguvu pamoja na kushindwa kutetea ajenda ya ufisadi kwa madai kuwa vinakumbatia mafisadi.

Kambaya hakuishia hapo, amesema kuwa kwa sasa kila chama kinawajibu wa kujijenga huku akidai kuwa matokeo mazuri katika uchaguzi Mkuu wa 2015 ya vyama vinavyounda UKAWA hayakutokana na nguvu wala ushawishi wa umoja huo kupitia Edward Lowassa aliyekuwa Mgombea wa Chadema kwa mwamvuli wa umoja huo, bali yalitokana na nguvu za vyama hivyo.

“Kila chama kinahitaji kijijenge, uchaguzi uliopita hatukushinda sababu ya Lowassa. Uchaguzi huu umedhihirisha hilo sababu alipita katika kata zote lakini hawakushinda. 2015 tulishinda uchaguzi sababu ya nguvu za vyama vyetu,” amesema na kuongeza.

“2020 huenda kusiwepo UKAWA sababu ulilenga kutetea katiba itakua ajabu kutumia umoja huo ambao lengo lake ni tofauti, labda utafutwe umoja mwingine na jina lingine.”

Aidha, Kambaya amemtuhumu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sheriff Hamad na wenzake kuwa wanatumia rasilimali za chama hicho kuijenga Chadema kwa mgongo wa UKAWA.

“Sasa kuna CUF inayofanya kazi Bara na inayofanya kazi Zanzibar, Katibu Mkuu na kundi lake lengo lao ni kuiua CUF Bara na ndiyo maana baadhi ya wabunge na viongozi wa CUF walisimama katika majukwaa kuwanadi wagombea wa Chadema ilhali katika maeneo husika kulikuwa na wagombea wa CUF,” amesema.

Ameongeza kuwa “Tatizo kwetu sio UKAWA, tatizo kwetu ni CUF, Ukawa utafuata baadae. UKAWA ni maridhiano baada ya kukijenga chama chetu.

Chanzo: Modewjiblog
 
Msemaji wa kafu ya lipumba hana tofauti na harakaharaka msemaji wa ccm tofauti ni majina tu
 
Hapa suluhisho ni maalim na mbowe na mbatia waunde chama kimoja kitakachounganisha vyama vyote vya upinzani ikiwezekana mpaka ACT hapo tuone kambaya atavuna nini 2020.

Hawa kina maalim wakiendelea kumchekea lipumba 2020 CUF itazikwa rasmi bara maana upinzani hauwezi kushinda ukigawanyika

Time will tell
 
Maamuzi madogo ya kuthibitisha kujiudhuru kwa Lipumba wakati suala la kujiudhuru kwake likiwa la moto limewaghalimu na litawaghalimu CUF na UKAWA milele.

' for many events, roughly 80% of the effects come from 20% of the causes.' Pareto principle inatafuna upinzani.

Umoja huu ungekuwa na Maono ungeiona 2017+ mwaka 2015 siku lipumba anaondoka na kukubali resignation yake kipindi hichohicho.
 
Lipumba na genge lake wajue kabisa hawatakaa wapate diwani wala mbunge hata mmoja kuanzia huku bara hadi Pemba. labda wa kuteuliwa (kuteuliwa na CCM of course - who else?).
 
Maamuzi madogo ya kuthibitisha kujiudhuru kwa Lipumba wakati suala la kujiudhuru kwake likiwa la moto limewaghalimu na litawaghalimu CUF na UKAWA milele.

' for many events, roughly 80% of the effects come from 20% of the causes.' Pareto principle inatafuna upinzani.

Umoja huu ungekuwa na Maono ungeiona 2017+ mwaka 2015 siku lipumba anaondoka na kukubali resignation yake kipindi hichohicho.
Emenena mkuu
 
Ni kweli kabisa.CUF walimuamini sana Lipumba bila kujua,walitakiwa wamvue uanachama siku ile ile.Haya mengine yangekuwa historia
 
Back
Top Bottom