CUF yajichanganya dhana ya Muungano

CUF yajichanganya dhana ya Muungano

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Na Alex Manonga.

Bila shaka baadhi mlipata fursa ya kutazama kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na kituo cha televison cha Star TV. Yalizungumzwa masuala mengi na yenye tija lakini nitapenda kugusia suala la Muungano.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF ndugu Julius Mtatiro akijibu swali la mtazamaji mmoja kupitia mtandao wa Jamii Forums aliyetaka kujua kama CUF kinaunga mkono hoja ya mkataba au la. Ndugu Mtatiro alibabaika sana katika maelezo yake na katika kubabaika huko aliongeza mashaka zaidi juu ya nini hasa sera ya chama chake kuhusu Muungano. Mwisho akasema chama chake kinaunga mkono serikali tatu na kiujanjanja akajaribu kuitetea dhana ya mkataba kama vile ni haja ya makubaliano hivi ya namna ya kuendesha hizi serikali tatu na mwisho katika namna inayoonesha kumuogopa Katibu Mkuu wake ambaye moja kwa moja ametangaza hadharani tena kwenye jukwaa la kisiasa kuunga mkono mkataba akatupia mzigo kwa viongozi wa juu labda watalisemea zaidi.

Katika maelezo ya Mtatiro nimepata mambo mawili; moja, kwamba Mtatiro binafsi haamini na hakubaliani na hoja ya mkataba lakini anashindwa kusema hadharani na Pili, kwamba CUF kama chama hawajakubaliana au hawakubaliani juu ya jambo hili. Kwa mujibu wa watetezi wa mkataba, Zanzibar inapaswa kuwa na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa ikiashiria vivyo hivyo kwa Tanganyika. Ukishakuwa na Serikali ya Zanzibar na Tanganyika zenye mamlaka kamili utahitaji serikali ya tatu ya Muungano ya kazi gani na itayatoa wapi mamlaka yake wakati kila nchi ina mamlaka yake kamili mikononi mwake? Huhitaji kuwa Albert Einstein kujua kuwa hawa wanataka kuvunja Muungano. Kimsingi watetezi wa mkataba wanataka kuvunja Muungano lakini wameamua kupitia njia yenye kona nyingi kama sehemu ya kuhadaa wananchi hasa wasiotaka Muungano uvunjike.

Nadhani ni muhimu CUF kikatolea ufafanuzi juu ya sera yake ya Muungano la sivyo itaonekana kuna vyama viwili ndani ya kimoja, kimoja kikitaka serikali tatu na kingine mkataba. Kutokuwa na sera inayoeleweka kutawachanganya watanzania na mwisho wakiacha kuwachagua mtalalamika kura zenu kuibwa au tumekosa kura kwa sababu pale wanaishi watu wengi kutoka bara!

Namuunga mkono Zitto kuhusu mantiki ya Muungano. Kwamba tunaweza tusiwe na kitu kizima kama jiwe la kulishika mkononi na kusema hiki au huu ndio faida ya Muungano. Lakini ile heshima tulioujenga kwa Afrika kutofungwa na mipaka ya kufikirika ya kikoloni ni kitu kizito sana. Ni jambo la ajabu sana kwamba tunaheshimu sana hivi vinchi vya kikoloni ( call them Bismarck states), Tanganyika na Zanzibar kuliko nchi iliyoundwa na waafrika wenyewe( Tanzania). Pia nakubaliana naye kwamba ukiruhusu sehemu moja ya nchi kujimega unahalalisha mmomonyoko endelevu maana hakutakuwa na hoja ya kuwazuia wengine wasijitenge.

Nafikiri ifike mahali kujadili suala la kuvuruga Muungano iwe ni mwiko kama ilivyo mwiko kwa watoto kujadili kuvunja ndoa ya baba na mama yao eti kwa kuwa walikosea taratibu za kuchumbiana!

Nawatakia mwaka 2013 wenye baraka tele!
 
Mkuu maneno mazito sana haya! Unaweza kwenda hatua moja mbele zaidi na kufunguka kama ilivyotabia ya African American
Zanzibar United Front ( ZUF) ilianzishwa na maalim na wenzake na baadeye walibadili jina kwa sababu sheria hairuhusi chama cha upande mmoja wakaita Civic United Front. Cuf ni ya maalim atamuachia Jussa wakina Hamad wasahau
 
Last edited by a moderator:
Mm binafsi nimesikiliza lakn sijaona kama amejichanganya! Ameenda straight to the point wao wana options mbili moja ni muungano wa mkataba na pili ni muungano wa serikari tatu! Sasa wapi amejichanganya!
 
Ina maana hawajaamua option ipi wauchukue? Ukahaba wa kisera!
 
...Kwa nini wasijitenge? [!] Kama Sudan Kusini (waliyokuwa ndani ya Sudan) waliweza, na Rais Kikwete alihudhuria kujitenga kwao, Zanzibar wana nini? Kama iliwezekana kwa Elitrea kutoka Ethiopia, Zanzibar isijitenge ina nini? Na kama leo Somalia kuna Somalia na Puntiland, Zanzibar isjitenge kwa nini?

Kama kuna hoja; nadhani waulizwe Wazanzibari na si Wazanzibara! Tatizo letu (wengi) ni kudhani kwamba "muungano" wa Nyerere na Karume ni "jambo takatifu" na kamwe pasiwepo na mawazo kinyume na mawazo ya Mwalimu Nyerere...huu utakuwa nu ujinga na hata Mwalimu Nyerere alikataa watu kuwa wajinga (na wapumbavu) soma Tujisahihishe (1962, ukurasa wa 5) iliandikwa:
"....Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache hawatakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo ya wazi wazi."

Wanaoweza kuamua hatma ya Zanzibar ni Wazanzibari si Wazanzibara! Kama hivyo ndivyo, Wazanzibari wapewe haki hiyo; na kwa sasa wanaoweza kuzungumza juu ya nini wanataka ni wananchi wa Zanzibar. CUF, kwa asili, ni chama kilichochokua "masalia" ya wapinga muungano tangu historia ya kufukuzwa kwa Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake kutoka CCM. Hakuna shaka yoyote kwamba Mwalimu Nyerere hakutaka mtu yeyote apinge "muungano" aliyouasisi kwa sababu alizozijua yeye (na sehemu ndogo) Abeid Aman Karume.

Tazama, Mtatiro (Julius) si Mzanzibari isipokuwa ni Mzanzibara! Kwa jinsi hiyo, huwezi kumuuliza msimamo wa CUF juu ya mfumo wa mungano wanaoutaka CUF - Zanzibar. Hili ni sawa na kuwauliza CCM juu ya aina ya muungano wao - kwao CCM ni muungano wa serikali mbili (kama hivi ulivyo)...mbona sijaona sera ya vyama vingine juu ya muungano zaidi ya CCM na CUF? Hili linafahamika kwa kuwa siasa za visiwani ni CCM dhidi ya CUF (huu ni ukweli) na kama historia huandikwa; basi wanaoweza kuanikwa juu ya harakai za Zanzibar dhidi ya muungano lazima aandikwe Maalim Seif Sharif Hamad (na wenzake) waliyofukuzwa CCM na kuanzisha harakati zao nje ya CCM na mwaka 1992 walipopewa fursa ya kuanzisha vyama vingi walikuwa tayari wana agenda ya kisiasa juu ya mustakabali wa Zanzibar.

Tazama, hata mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 (Toleo la 2010) yamechochewa na "mtazamo" wa kuifanya Zanzibar kuwa "nchi ndani ya muungano" jambo ambalo Wazanzibara (na Watanganyika) walichelewa kuona ni kwa jinsi gani asilimia 66 (66%) ya Wazanzibari waliunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kutumia Katiba ya Zanzibar ya 1984 (RE 2010) mbayo imetoa nafasi kwa mfumo huo wa kisiasa kuwapo Zanzibar. Kwa hili la muungano; hakuna mwenye mamlaka (mandate) ya kuamua juu ya mfumo unaofaa (kwa Zanzibar) isipokuwa Wazanzibari wenyewe kwa uwezo wao kikatiba.

Kulazimisha mawazo ya mtu kuwa ndio sehemu ya mawazo ya watu wengine utakuwa ni "udikteta" na kamwe demokrasia haitaacha kutukanwa na kufanyiwa mzaha. Wapo wanaodai kwamba wao ni wana demokrasia na wanadai kupigania demokrasia na hata kudai kwamba watakufa wakitetea demokrasia...huu ni wakati wake wa kukomaa kidemokrasia! Waachwe Wazanzibari waamue hatma yao; Wazanzibara tubaki kuwa wasindikizaji, kinyuma chake, na sisi (Wazanzibara na Watanganyika) tudai nchi yetu iliyozamishwa kwenye MUUNGANO na kisha kupoteza utambulisho wake!
 
Zanzibar United Front ( ZUF) ilianzishwa na maalim na wenzake na baadeye walibadili jina kwa sababu sheria hairuhusi chama cha upande mmoja wakaita Civic United Front. Cuf ni ya maalim atamuachia Jussa wakina Hamad wasahau

Umesikia kama jana zaidi ya wanachama 50 waliokua ADC wamerejesha wakati kulipofanyika mkutano wa CUF Tanga!
 
Tatizo ni UELEWA tu hakuna jengine! Sisi wazanzibari tunavyofahamu na ndivyo ilivyo Sera ya CUF ni mfumo wa Serikali 3 na wakati Maalim anaposimama katika majukwaa na kuzungumzia kuunga mkono Muungano wa mkataba anazungumza yeye kama Maalim Seif kwa niaba yake binafsi na sio kwamba anaisemea CUF. Hata ukifuatilia mikutano yake utaona 'Hansard' zinajieleza wazi "mimi binafsi ni muumini muungano wa mkataba.." na wala sio "sisi (CUF) tumeamua kubadili msimamo na kutaka Muungano wa mkataba.".
 
Na Alex Manonga.

Nafikiri ifike mahali kujadili suala la kuvuruga Muungano iwe ni mwiko kama ilivyo mwiko kwa watoto kujadili kuvunja ndoa ya baba na mama yao eti kwa kuwa walikosea taratibu za kuchumbiana!

Nawatakia mwaka 2013 wenye baraka tele!

Mohamed Mtoi ni mwana chadema lakini ananishangaza na kunichekesha sana. Wakati anasema CUF wanajichanganya, na yeye anarudia hayo hayo ya kujichanganya. Mtoi ni kiongozi wa vijana ndani ya CDM kwa hiyo inastaajabisha kuwa na yeye anaposema kujadili suala la muungano iwe marufuku! Unajua sera ya CDM kuhusu muungano? Na unajua msimamo wa naibu katibu wako mkuu juu ya muungano? Kama ukikuta mitazamo miwili iko sawa una haki ya kuilaumu CUF. Lakini kamani tofauti basi anza kulaumu CDM kwanza kwa vile na wenyewe hawana msimamo juu ya ajenda ya muungano.

Kwa CUF ukisema serikali tatu na mkataba it is one and the same. Tofauti ni hiyo serikali ya tatu itakuwaje tu. Hamna mkanganyiko itakuwa zinakuchanganya tu.
 
Tatizo ni UELEWA tu hakuna jengine! Sisi wazanzibari tunavyofahamu na ndivyo ilivyo Sera ya CUF ni mfumo wa Serikali 3 na wakati Maalim anaposimama katika majukwaa na kuzungumzia kuunga mkono Muungano wa mkataba anazungumza yeye kama Maalim Seif kwa niaba yake binafsi na sio kwamba anaisemea CUF. Hata ukifuatilia mikutano yake utaona 'Hansard' zinajieleza wazi "mimi binafsi ni muumini muungano wa mkataba.." na wala sio "sisi (CUF) tumeamua kubadili msimamo na kutaka Muungano wa mkataba.".

Matamanio ya maalim seif tangu aanzishe cuf ni kutawala zanzibar hiyo ni sababu mpaka sasa yeye ni mgombea pekee wa cuf. Msimamo wake hata kama haupo kwenye hansard ni wa chama. Wanachama 50 ni kumtisha hamad rashid
 
Tatizo ni UELEWA tu hakuna jengine! Sisi wazanzibari tunavyofahamu na ndivyo ilivyo Sera ya CUF ni mfumo wa Serikali 3 na wakati Maalim anaposimama katika majukwaa na kuzungumzia kuunga mkono Muungano wa mkataba anazungumza yeye kama Maalim Seif kwa niaba yake binafsi na sio kwamba anaisemea CUF. Hata ukifuatilia mikutano yake utaona 'Hansard' zinajieleza wazi "mimi binafsi ni muumini muungano wa mkataba.." na wala sio "sisi (CUF) tumeamua kubadili msimamo na kutaka Muungano wa mkataba.".
CUF serikali tatu, akisimama Maalim Seif yeye ni muumini wa mkataba? Wewe ni muumini wa nini?
 
Back
Top Bottom