CUF wapinga Uteuzi wa Prof. Muhongo

CUF wapinga Uteuzi wa Prof. Muhongo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,162
Reaction score
11,229
JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) imesema wanasikitishwa na uteuzi wa baraza la mawaziri lililotajwa juzi na Rais John Magufuli na kudai kuwa, katika baraza hilo wamerudishwa wale mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

Pia imesema katika baraza hilo hakuna uteuzi ambao umewiana hasa katika suala la usawa wa kijinsia na wala haukuzingataia Muungano uliokuwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Hamidu Bobali amesema wanashangaa kuwaona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Harson Mwakyembe kuwepo tena.

Amesema, Waziri Muhongo alikuwa anatuhumiwa na suala la Escrow na akajiuzulu halafu Magufuli amemrudisha tena kitu ambacho kinawakosesha amani.

Inatusikitisha sana kitendo cha Rais wetu kumteua tena Waziri Muhongo kurudi tena wizarani hapo wakati alikuwa na kashfa kubwa ya escrow lakini amerudishwa tena inaonyesha Magufuli pia pamoja na kusifiwa juu ya utendaji wake hayuko makini,?amesema Bobali.

Pamoja na Muhongo pia Waziri Mwakyembe alikuwa katika wizara ambayo sasa hivi inakubwa na matatizo makubwa ya kupitisha makontena na wakati alikuwa waziri katika wizara hiyo, hilo lilitosha kwa Magufuli kufanya upembuzi wa Mawaziri. Hao wote hawakufaa tena kuridi kuwa mawaziri,? amesema.

Ameongeza kuwa, wanasikitishwa sana kwani ile kasi ambayo Magufuli alianza nayo wanaiona inakufa siku si nyingi kwa kuwarudia tena mawaziri hao mizigo.

Wananchi tunasikitika sana kwa kuwa tulimuamini Rais Magufuli lakini imani hiyo inakaribia kukatika kutokana na kurudishwa kwa mawaziri hawa na kusababisha kasi kupungua,?ameeleza

Aidha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo hakuwahi kupatikana na hiyo ya Escrow kwani alijiuzulu mwenyewe. Kwa kuhofia kupatikana na hatia.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro uliokuwepo Zanzibar na kusema kuwa Baraza la vijana wa chama hicho kwa kushirikiana na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba Wananchi (Ukawa) wameandaa mkutano juu ya kuzungumzia mgogoro huo.

Tunafurahishwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya viongozi kwetu wa huko Zanzibar lakini baraza letu limeandaa mkutano huo ili kuzungumzia suala hili,?amesema Bobali

Hata hivyo Bobali amesema wanamuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala la Zanzibar kwani kutokufikia kikomo kunasababisha mambo mengi kurudi nyuma ikiwa moja na uchumi kushuka.

Jumuiya ya vijana inawatahadharisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha mara moja kauli chafi na vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na wanachama hao kwani vinaweza kuamsha hasira za vijana wa CUF Zanzibar,? amesema Bobali.
 
Hawa watu hawajiulizi ilikuwaje wakamuunga mkono Lowassa aliyejiuzulu kwa tuhuma kama hizohizo, tena kwa nafasi ya urais?? Halafu wanakumbuka kuwa Alli Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzulu kabla ya kuwa rais?? BTW wanajua the other side of Muhongo??
 
Ukawa ebu jifunzeni kutunza kumbukumbu.Miezi miwili iliyopita mlikuwa mnamnadi mtu aliyejiuzuru Uwaziri Mkuu kwa kashfa ambayo hadi sasa madhara yake yanalitafuna Taifa,awe Rais wa JMT.Au ndio nyani halioni Ku......le?
 
Ni lini CUF wamemtambua Rais Magufuli mpaka wanaanza kukosoa uteuzi wa Baraza lake la Mawaziri?

Hizi siasa za kinafiki na kilaghai hazitakiwi nchini.
 
Hawajitambui hao.ukiwauliza makosa ya muhongo ninini utaona watakavyojiumauma midomo. By the way wao siwalimchagua lowasa. Watulie tuli.

Muhongo ndiye waziri sahihi wa ile wizara ama wengine ni wababaishaji.

Yaani mtu yeyote wa ukawa au aliyekuwa shabiki anayeweza kumnyoshea kidole muhongo basi huyo mtu mtindio wake wa ubongo haupo sawa kwani anamjua lowasa ni nani lakini alimshabikia na kumuona kuwa anafaa kuwa rais wake na hakuona kama hilo ni tatizo sasa leo anaibuka na Mzalendo anayepinga wababaishaji
 
Kama hawakumpinga Lowassa kuwa mgombea kupitia umoja ambao na wao ni members bora wakae kimya tu.Waache unafiki.
 
Hawa watu hawajiulizi ilikuwaje wakamuunga mkono Lowassa aliyejiuzulu kwa tuhuma kama hizohizo, tena kwa nafasi ya urais?? Halafu wanakumbuka kuwa Alli Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzulu kabla ya kuwa rais?? BTW wanajua the other side of Muhongo??

Ukawa ebu jifunzeni kutunza kumbukumbu.Miezi miwili iliyopita mlikuwa mnamnadi mtu aliyejiuzuru Uwaziri Mkuu kwa kashfa ambayo hadi sasa madhara yake yanalitafuna Taifa,awe Rais wa JMT.Au ndio nyani halioni Ku......le?

hapa ndio panadhihirisha pasi na shaka yeyote kuwa rais mstahafu B. W. Mkapa kuwa alikuwa sahihi
Cc Lizaboni, FaizaFoxy na MsemajiUkweli
 
Last edited by a moderator:
Hawa watu hawajiulizi ilikuwaje wakamuunga mkono Lowassa aliyejiuzulu kwa tuhuma kama hizohizo, tena kwa nafasi ya urais?? Halafu wanakumbuka kuwa Alli Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzulu kabla ya kuwa rais?? BTW wanajua the other side of Muhongo??
Wajinga tu
 
ccm ni ile ile,ccm mbele kwa mbele,watanzania mtaisoma no
mbati huwezi kusukuma gari ukiwa ndani ya gari ni sayansi ndogo tu nanukuu
 
Hawa watu hawajiulizi ilikuwaje wakamuunga mkono Lowassa aliyejiuzulu kwa tuhuma kama hizohizo, tena kwa nafasi ya urais?? Halafu wanakumbuka kuwa Alli Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzulu kabla ya kuwa rais?? BTW wanajua the other side of Muhongo??

Malofa katika ubora wao.
 
Khaa!! Kasomeni katiba kisha mrudi hapa. Kudadadeki zenu :mvutaji:
 
Hoja hii weng wataihusianisha na Lowasa tu mana hakuna namna nyngne.Nionavyo mm hakuna mwny nia ya dhati ya kusaidia kuondoa ufisadi mana kila mtu anafnya makosa ya kuwakumbatia hao hao
 
Lowasa alijiuzulu Uwazi mkuu na hakuwa anagombea cheo hicho tena bali Urais, Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa mambo ya ndani na alivyorudi hakugombea hiyo nafasi bali Urais. Huyu Muhongo alijiuzulu Uwaziri wa Nishati na Madini na karudi nafasi hiyo tena na ndiyo maana watu wanalalanika. Angepewa Kilimo au nyingine tofauti na aliyojiuzulu watu wasingelalamika.
 
JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) imesema wanasikitishwa na uteuzi wa baraza la mawaziri lililotajwa juzi na Rais John Magufuli na kudai kuwa, katika baraza hilo wamerudishwa wale mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

Pia imesema katika baraza hilo hakuna uteuzi ambao umewiana hasa katika suala la usawa wa kijinsia na wala haukuzingataia Muungano uliokuwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Hamidu Bobali amesema wanashangaa kuwaona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Harson Mwakyembe kuwepo tena.

Amesema, Waziri Muhongo alikuwa anatuhumiwa na suala la Escrow na akajiuzulu halafu Magufuli amemrudisha tena kitu ambacho kinawakosesha amani.

Inatusikitisha sana kitendo cha Rais wetu kumteua tena Waziri Muhongo kurudi tena wizarani hapo wakati alikuwa na kashfa kubwa ya escrow lakini amerudishwa tena inaonyesha Magufuli pia pamoja na kusifiwa juu ya utendaji wake hayuko makini,?amesema Bobali.

Pamoja na Muhongo pia Waziri Mwakyembe alikuwa katika wizara ambayo sasa hivi inakubwa na matatizo makubwa ya kupitisha makontena na wakati alikuwa waziri katika wizara hiyo, hilo lilitosha kwa Magufuli kufanya upembuzi wa Mawaziri. Hao wote hawakufaa tena kuridi kuwa mawaziri,? amesema.

Ameongeza kuwa, wanasikitishwa sana kwani ile kasi ambayo Magufuli alianza nayo wanaiona inakufa siku si nyingi kwa kuwarudia tena mawaziri hao mizigo.

Wananchi tunasikitika sana kwa kuwa tulimuamini Rais Magufuli lakini imani hiyo inakaribia kukatika kutokana na kurudishwa kwa mawaziri hawa na kusababisha kasi kupungua,?ameeleza

Aidha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo hakuwahi kupatikana na hiyo ya Escrow kwani alijiuzulu mwenyewe. Kwa kuhofia kupatikana na hatia.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro uliokuwepo Zanzibar na kusema kuwa Baraza la vijana wa chama hicho kwa kushirikiana na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba Wananchi (Ukawa) wameandaa mkutano juu ya kuzungumzia mgogoro huo.

Tunafurahishwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya viongozi kwetu wa huko Zanzibar lakini baraza letu limeandaa mkutano huo ili kuzungumzia suala hili,?amesema Bobali

Hata hivyo Bobali amesema wanamuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala la Zanzibar kwani kutokufikia kikomo kunasababisha mambo mengi kurudi nyuma ikiwa moja na uchumi kushuka.

Jumuiya ya vijana inawatahadharisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha mara moja kauli chafi na vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na wanachama hao kwani vinaweza kuamsha hasira za vijana wa CUF Zanzibar,? amesema Bobali.

Yani hizi ndio siasa za majitaka kabisa, muda wote walikaa kimya kama wamemwagiwa maji, wakijifariji kuwa eti Magufuli alikuwa anatekeleza sera za UKAWA,ameteuliwa Nape, Muhongo tayari nongwa zimeanza !! hizo si ndio sera za UKAWA kaeni kimya.alafu mbona nyie wakati mnamchagua Lowasa kuwa mgombea wenu hakuna aliyewagusa kwani nyie ni nani hasa eh? nyie muwe na haki ya kumteua mtuhumiwa wa Richmond wengine hawana haki ya kuteua watuhumiwa wa Escrow!
 
Lowasa alijiuzulu Uwazi mkuu na hakuwa anagombea cheo hicho tena bali Urais, Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa mambo ya ndani na alivyorudi hakugombea hiyo nafasi bali Urais. Huyu Muhongo alijiuzulu Uwaziri wa Nishati na Madini na karudi nafasi hiyo tena na ndiyo maana watu wanalalanika. Angepewa Kilimo au nyingine tofauti na aliyojiuzulu watu wasingelalamika.
Kwa nn apelekwe kilimo wakati aliisimamia wizara hii vizuri sana. Acheni unafiki Muhongo kichwa na tunahitaji vichwa nchi hii. Mna katabia kakutaka kuua vichwa vya nchi hii. Asante Magufuli kwa kutokubali siasa chafu za media ambazo kila ck zinataka tanzania iwe chini ya miguu yao. Mfyuuuuuiu
 
Hawajitambui hao.ukiwauliza makosa ya muhongo ninini utaona watakavyojiumauma midomo. By the way wao siwalimchagua lowasa. Watulie tuli.

Muhongo ndiye waziri sahihi wa ile wizara ama wengine ni wababaishaji.

Yaani mtu yeyote wa ukawa au aliyekuwa shabiki anayeweza kumnyoshea kidole muhongo basi huyo mtu mtindio wake wa ubongo haupo sawa kwani anamjua lowasa ni nani lakini alimshabikia na kumuona kuwa anafaa kuwa rais wake na hakuona kama hilo ni tatizo sasa leo anaibuka na Mzalendo anayepinga wababaishaji

Mkuu umesema point lakini hapa kajifunze kiswahili ,nanunukuu"...basi huyo mtu mtindio wake wa ubongo haupo sawa.." mwisho wa kunukuuu!
 
Back
Top Bottom