CUF wanastahili kugombea majimbo mengi zaidi 2020

Babu Kijana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
589
Reaction score
278
Katika UKAWA CUF wamedhihirisha kuwa bado wapo ngangari kutoyumba kufanya mabadiliko, huku bara wamejitahidi kuchukua majimbo mengi kwa uwiano na walivyogombea ndani ya UKAWA.

Nafikiri 2020 waongezewe idadi kubwa ya majimbo. CDM wamejitahidi pia lakini na tofauti ya matarajio ya wengi hasa kwa kupoteza majimbo mengi hususani kanda ya ziwa.

UKAWA tujipange kuangalia 2020.
 
Cuf walipewa majimbo mengi yenye uhakika wa kushinda...pia chadema imepoteza majimbo mengi kanda ya ziwa kutokana na siasa za kikabila...ccm wamefanya siasa chafu sana kanda ya ziwa
 
niliandika humu kampeni za kikabila ,nilitegemea ukawa waitishe pree na kupinga jambo hili, pia nilitegemea wapinge udhalilishaji wa mgombea wao hasa kanda ya ziwa nadhani walikuwa too much passive wakaonekana hawana haja ya kusikilizwa ccm kuona hivyo wakaendelea na udhalilishaji ambao ulimbomoa lowassa na kumjenga magufuli -katika maeneo ya wasiokuwa na elimu mambo ya kijinga yanaweza kumsaidia mgombea
 
cuf wamevamia majimbo mengi ya cdm kama huko tabora,singida hata dsm-hata hivyo cuf wengi walidai wameonewa ,lakini wajiulize matunda ya umoja wameyeona? tufikirie namna ya kuboresha sio mivutano kama ile ya kina lipumba-kauli ya lipumba iliwanyima CDM kura za wana -cuf na kuchochea wana-cuf kukataa kufuata makubaliano ya ukawa.
 
hata NCCR INGEPEWA VITI VINGI SEHEM MBALIMBALI NAAMIN WANGESHINDA WALAU VITI 3...4 hivi . sasa huyu mbatia kakubalia kupewa majimbo sita.. , kwa waliosoma probability wanajua unapoongeza sample space !! pia namba of event inaongeza
 
niliandika humu kampeni za kikabila ,nilitegemea ukawa waitishe pree na kupinga jambo hili, pia nilitegemea wapinge udhalilishaji wa mgombea wao hasa kanda ya ziwa nadhani walikuwa too much passive wakaonekana hawana haja ya kusikilizwa ccm kuona hivyo wakaendelea na udhalilishaji ambao ulimbomoa lowassa na kumjenga magufuli -katika maeneo ya wasiokuwa na elimu mambo ya kijinga yanaweza kumsaidia mgombea

Vipi kanda ya kaskazini?
 
CUF wameporwa mbagala
waende mahakamani
hadi Lipumba anatamani tena kurudi uenyekiti
 
Nafikiri ni vema tu aombe radhi wanacuf na wanaukawa arudi kushiriki kujenga chama, nafikiri atakuwa ameona matunda ya umoja huu. Kupata takribani wabunge 7 bara peke yake ni mafanikio makubwa
 
hata NCCR INGEPEWA VITI VINGI SEHEM MBALIMBALI NAAMIN WANGESHINDA WALAU VITI 3...4 hivi . sasa huyu mbatia kakubalia kupewa majimbo sita.. , kwa waliosoma probability wanajua unapoongeza sample space !! pia namba of event inaongeza
Sifahamu elimu na umri wako lakini kugombea maeneo mengi si kushhinda hii si probability ya bahati na sibu panataka uwezo na kukubalika kwa chama pia resources kuna maeneo wamepewa NCCR hata kampeni wameshindwa kufanya-hebu angalia ACT nao walijigamba sana kuwa wameweka wagombea kila pahala zaidi ya CHADEMA yaani sifa ni kuweka wagombea wengi ona majibu yake
 
sasa mantiki ya UKAWA iko wapi apo
 
Katika UKAWA CUF wamedhihirisha kuwa bado wapo ngangari kutoyumba kufanya mabadiliko, huku bara wamejitahidi kuchukua majimbo mengi kwa uwiano na walivyogombea ndani ya UKAWA.

Nafikiri 2020 waongezewe idadi kubwa ya majimbo. CDM wamejitahidi pia lakini na tofauti ya matarajio ya wengi hasa kwa kupoteza majimbo mengi hususani kanda ya ziwa.

UKAWA tujipange kuangalia 2020.

Ishukuriwe UKAWA bila hivyo wangeanguka zaidi....aliekuwa anawadanganya kipindi kile kuwa wajitoe UKAWA wangechemka...naujue jambo 1 majimbo hawagawani kama vitumbua lazima wapige kazi kuhamasisha chama....usidhani Chadema wamejipendelea waliwekeza kwenye Op tofauti zakujenga chama...naushukuriwe Uongoz wa CDM kukubali umoja lkn hata wangesimama wenyewe CDM wangepasua pengine zaidi ya sasa.....
 
Usisahau pia investment ya lowasa hapo na upepo wake wa kisiasa
 
hata NCCR INGEPEWA VITI VINGI SEHEM MBALIMBALI NAAMIN WANGESHINDA WALAU VITI 3...4 hivi . sasa huyu mbatia kakubalia kupewa majimbo sita.. , kwa waliosoma probability wanajua unapoongeza sample space !! pia namba of event inaongeza

Mkuu UKAWA haikuundwa kugawana majimbo....Vyama viliachiana sehemu za kugombea kutokana na kukubalika kwake watu kama NCCR hawakuwekeza sana kwenye kujenga chama so walikuwa hawafahamiki sehemu nyingi Ukiacha Kigoma ambako siasa za kule zimeiua zaidi
 
Cuf walipewa majimbo mengi yenye uhakika wa kushinda...pia chadema imepoteza majimbo mengi kanda ya ziwa kutokana na siasa za kikabila...ccm wamefanya siasa chafu sana kanda ya ziwa

Apo umenena ndugu uchaguzi wa mwaka huu ulitawaliwa na ukanda.
 
sasa mantiki ya UKAWA iko wapi apo

Mkuu inaonekana kumbe hukujua muungano ule ulihusu nini.....!! kila chama ilitakiwa kifanye kazi sio kutembelea NYOTA ya mwingine au ulielewa chadema waache OP wakahamasishe watu wachague NCCR wao nichama kina uongoz wake so Namna gani kushinda Jimbo uongozi wa chama ndio kz yake
 
hata NCCR INGEPEWA VITI VINGI SEHEM MBALIMBALI NAAMIN WANGESHINDA WALAU VITI 3...4 hivi . sasa huyu mbatia kakubalia kupewa majimbo sita.. , kwa waliosoma probability wanajua unapoongeza sample space !! pia namba of event inaongeza

Akili zako zimeathiriwa na push-ups za jukwaani.ACT waliosimamisha wagomebea nchi nzima wamepata viti vingapi?
 
Nafikiri ni vema tu aombe radhi wanacuf na wanaukawa arudi kushiriki kujenga chama, nafikiri atakuwa ameona matunda ya umoja huu. Kupata takribani wabunge 7 bara peke yake ni mafanikio makubwa

Bara CUF ina wabunge 10 wa kuchaguliwa.Mtwara 2,Lindi 4,Dar 2,Tanga mjini 1 na Tabora 1.Pia fisiemu kwa kushirikiana na mawakala wao wote wamevuruga jumbo la Mbagala ambalo CUF iliwagaragaza vibaya ccm.
 
Cuf walipewa majimbo mengi yenye uhakika wa kushinda...pia chadema imepoteza majimbo mengi kanda ya ziwa kutokana na siasa za kikabila...ccm wamefanya siasa chafu sana kanda ya ziwa

kama CHADEMA walivyofanya kampeni chafu mikoa ya kilimanjaro na Arusha, achilia mbali kampeni za udini mulizozipiga makanisani mwote humu
 
Back
Top Bottom