CUF wanamlea Lipumba

DhulRah

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
251
218
Kinachotokea CUF ni matunda ya chama hicho kumlea sana Lipumba. Kitendo cha Lipumba kulazimisha kurudi tena kwenye kiti baada ya kujiuzulu mwenyewe kwa hiyari yake ni matokeo ya kumlea yeye pamoja na mtandao wake, walipaswa kuchukua hatua mapema, kumtafuta mwenyekiti mwingine lakini kuchelewa kwao kumempa nafasi ya kurudi tena.

Suala la kujitangazia kumuondoa katibu mkuu Maalim Seif vilevile ni moja ya sababu ya kumlea sana huyu mtu. Hapo mbeleni watajikuta chama kimeshakufa bwana yule ameshakiua.

VIONGOZI WA CUF CHUKUENI HATUA MAPEMA LIPUMBA ANAUA CHAMA CHENU.
 
Kinachotokea CUF ni matunda ya chama hicho kumlea sana Lipumba.
Kitendo cha Lipumba kulazimisha kurudi tena kwenye kiti baada ya kujiuzulu mwenyewe kwa hiyari yake ni matokeo ya kumlea yeye pamoja na mtandao wake, walipaswa kuchukua hatua mapema, kumtafuta mwenyekiti mwingine lakini kuchelewa kwao kumempa nafasi ya kurudi tena.
Suala la kujitangazia kumuondoa katibu mkuu Maalim Seif vilevile ni moja ya sababu ya kumlea sana huyu mtu.
Hapo mbeleni watajikuta chama kimeshakufa bwana yule ameshakiua.
VIONGOZI WA CUF CHUKUENI HATUA MAPEMA LIPUMBA ANAUA CHAMA CHENU.
Seif interest yake ni kujitangazia karibuni atakuwa rais wa Zanzibar, anaota mchana ! Haoni kama anaiua CUF !!
 
Kwa vile Lipumba-vu anataka kuua chama wana-CUF nao wanapaswa kumwuua mapema! Wamwulize Bashite kule alikokatoa kale kamjamaa kenye Pistol kwa Nape!
 
Alivunja ofisi na kuiteka huku analindwa na polisi.

Hazina walimwibia ruzuku huku wakimsaidia kufungua a/c kinyume na utaratibu.

Mikutano yake inalindwa na polisi huku vyama vingine na wanasiasa wakiambiwa hakuna kufanya mikutano hadi 2020.

Mara kwa mara yupo magogoni anadhauriana na mabosi zake,hao ndio wanamlea.

Kufutwa kwa Seif ni kuzima jitihada za kimataifa kuingilia uhuni uliofanyika ili Shein atawale,wanamfukuza ili nchi zilizopinga ubaradhuli wa Jecha zione Seif hatakiwi ili madai yafe kibudu!!
 
Back
Top Bottom