Kuna sehemu nyingine mamluki wanatumika. Mfano mtaa wa Madale Kata ya wazo, Dar.... kuna mgombea wa CUF ameamua kugombea kivyake baada ya vikao vya ushirikiano kushindikana ikiwamo kuleta wananchama ili wammchague mgombea mwenye nguvu. Huyu wa CUF alileta wananchame wake lakini Chadema wakakshinda, hivyo kwa mujibu wa makubaliano ya UKAWA ilitakiwa huyu wa Chadema asimame..lkn badala yake huyu wa CUF naye akaenda kuchukua fomu na kusimama. Watu walipofuatilia ni kwanini ameng'ang'ania sana wakagundua kuwa mdogo wa huyo wa CUF anagombea kupitia CCM.. hivyo kulikuwa kunatengenezwa mazingira ya kumpa ushindi huyu mgombea wa CCM. Sasa kwa mazingira hayo unaweza kusema nini kama siyo mamluki.