CUF wambebesha msalaba Msekwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,781

Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtupia lawama Makamu Mwenyekiti wa CCM (bara), Bw. Pius Msekwa kuwa endapo damu itamwagika katika uchaguzi mkdogo wa
Jimbo la Igunga ndiye atakuwa amesababisha.

Meneja Kampeni wa chama hicho Jimbo la Igunga, Bw. Antony Kayange akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika kijiji cha Ncheli, Kata Sungwizi, alisema kitendo cha Bw. Msekwa kutangaza kuwa CCM itashinda katika jimbo hilo anataka damu imwagike.

Bw. Mayange alisema CCM haina chake kwa sababu imekuwa ikitaka
wananchi wa Igunga wachague mbunge wa chama hicho lakini akichaguliwa haonekani tena mpaka uchaguzi mwingine uje, huku akiacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa shida zilizokithiri.

Bw. Pius Msekwa alikaririwa akitamba kwenye vyombo vya habari kuwa pamoja ya matukio ya hapa na pale yanayofanywa na vyama vya upinzani, bado CCM itashinda katika uchaguzi wa mbunge utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu.

Kampeni za chama hicho zilizofanyika juzi katika Tarafa ya Simbo
alikozaliwa na kusoma Bw. Mahona, watu waliohudhuria kumsikiliza walimtaka asiige tabia za wabunge waliopita wa CCM pindi wanapochaguliwa hukimbilia Dar es Salaam wao wakibaki yatima na hawana sehemu ya kupeleka matatizo yao.

“Nimedhamiria kuokoa maisha ya ndugu zangu wa Igunga, ndiyo maana mwaka jana nilibaki peke yangu nikiomba kura zenu kwa baiskeli. Kati ya wagombea 13 waliochukua fomu za Ubunge nikapambana na mbunge aliyejiuzulu CCM hivi karibuni, Bw. Rostam Aziz na nikashinda vishawishi vyake vya kutaka nijitoe nikang’angana hadi mwisho nikashika nafasi ya pili nikipata kura 11,000,” alisema Bw. Mahona.

Kampeni za CUF zilitarajiwa kuendelea jana katika vijiji 96 vya Jimbo la Igunga ambalo wananchi wake wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ya safi ya kunywa na kunywesha mifugo yao.

“Huyu Pius Msekwa anatangaza CCM itachukua jimbo hili yaani wasukuma na wanyamwezi wote hatuwezi kudanganywa kama walivyozoea kufanya wanavyotaka,” alisema Bw. Mahona.

Mikakati ya kampeni

Akizungumzian kampeni za uchaguzi wa Igunga, Naibu katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro alisema wamejipanga vizuri na kuongeza timu kufikia 6 na kufanya mikutano 36 kwa siku katika kata 26 za Igunga.

Alisema baada wabunge sita wa Zanzibar kuwasili wengine 10 wanatarajia kuwasili leo, wengine 15 Alhamisi, na Ijumaa
wataongezeka watano na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Bw. Mtatiro alisema timu hiyo inaongeza mikutano kufikia 45 kwa siku na kutamba kuwa chama chake kiko tayari kupiga kampeni ya chini kwa chini, juu kwa juu na miguu kwa miguu.

Alisema vyama vingine vikileta helkopta moja, CUF nayo inafanya hivyo hivyo, vikileta tatu na hata kumi nacho kitafanya hivyo mpaka jimbo hilo libaki kwa chama hicho.
 

Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,821
1,914
si propaganda za siasa kusema mgombea wetu lazima ashinde lakini kutokana na historia inaweza kutufundisha kwamba amepre empty matokeo yaliyo chakachuliwa either way
 

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,115
14,389
Si vibaya ku-fantasize (kuota ndoto za mchana),
inasaidia kupunguza maumivu na mihemko...
 

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,773
801
Mbona CUF wanajaza wabunge wa taifa la zanzibar huko. Kwani ni ruksa kupeleka mamluki wa nchi tofauti katika huo uchaguzi???
 

thinka

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
334
142
wabunge ni wa tanzania sio wanzanziba kwa hyo angalia unachokisema kwanza umamluki umetoka wap.au umeshndwa kutofautisha kat ya tanganyika na tanzania ndugu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom