CUF waibana ZEC Zanzibar

CUF waibana ZEC Zanzibar

Pistol

Senior Member
Joined
Oct 13, 2015
Posts
194
Reaction score
86
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kama Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wana ushahidi wa kuhujumiwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, waonyeshe hadharani wananchi na dunia ipate kufahamu ukweli wake.

Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alipokuwa akizungumzia hatua ya Zec kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai ya kubaini vitendo vya udanganyifu.?Inasikitisha kuona tangu uchaguzi kufutwa matokeo Oktoba 28, mwaka huu, Mwenyekiti wa tume, Jecha Salim Jecha, ameshindwa kujitokeza hadharani kuonyesha vielelezo na ushahidi wa kuharibika kwa uchaguzi huo," alisema na kuongeza.

"Tumeishia kuambiwa jumla jumla tu uchaguzi kumefanyika udanganyifu bila ya kuonyeshwa vielelezo na ushahidi wa kuhalibika."Shehe alisema tangu kufanyika uchaguzi huo Oktoba 25, mwaka huu, mpaka sasa hakuna mtendaji yoyote wa ZEC aliyefikishwa katika chombo cha sheria kwa kushiriki kuharibu uchaguzi na kusababisha hasara kwa serikali.

Aidha, alisema kama kulikuwa na kura nyingi kuliko idadi ya watu waliosajiliwa katika Daftari la Wapiga, Zec walitakiwa kutaja vituo hivyo na kura zilizoongezeka badala ya kueleza bila ya kuonyesha ushahidi wake.

Alisema kuwa CUF itahakikisha uchaguzi wa marudio haufanyiki Zanzibar na badala yake ZEC wakamilishe kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Alisema pamoja na kuwapo vyama 14 vilivyosimamisha wagombea wa urais wa Zanzibar, lakini vyama vyenye uwakilishi mkubwa wa watu ni CCM na CUF visiwani humo.

Shehe alisema kama uchaguzi kulitokea kasoro haukupaswa kufutwa wote na badala yake ZEC walitakiwa kufanya uhakiki katika maeneo yenye kasoro na kurekebisha.


ZEC YANENA
Mkurugenzi wa Zec, Salum Kassim Ali, alisema uchaguzi wa marudio utafanyika Zanzibar na kwamba kwa sasa taratibu za kufanikisha uchaguzi huo zinaendelea kufanyika.
"Bado ni mapema kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio, lakini wananchi waendelee kuwa na subira baada ya taratibu kukamilika watatangaziwa ili wafahamu na kujitayarisha na uchaguzi huo," alisema.

CCM YAJIBU
Kwa upande wake, Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kimesema uchaguzi huo utafanyika hata kama CUF hawatashiriki.Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CCM Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema suala la chama cha siasa kushiriki au kutoshiriki uchaguzi ni la hiyari.
Alisema vyama vyenye usajiliwa wa kudumu vipo 22 lakini ni 14 tu ndiyo vilisimamisha wagombea wa nafasi mbali mbali ikiwamo urais katika uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.
Alisema CCM kwa kutambua ukweli kuwa matokeo ya uchaguzi wa awali yamefutwa rasmi, imeanza kufanya maandalizi mazito ya kuingia katika uchaguzi wa marudio.

CHANZO:NIPASHE
 
Znz hakuna haja yakua namfumo wavyama vingi anae sema Uchaguzi znz ulidiwe kwakua ccm wameshindwa ni ni maana yademoccorai kama haku.bai wasubiri miujiza yaharingumu kiuchumi.loo amakweli uanafiki huuo mpakalini HUKO znz
 
ZEC mtangazeni Maalim Seif kuwa ni msshindi, kwanini mnajidhalilisha namna iyo jamani..???
aaaahhggrrrhh
 
...ccm wamejitoa akili zote, yani wamevurugwa wakavurugika, hayana aibu kabisa!
 
Katika kosa ambalo CCM na Tanzania watajuta maisha yao ni kurejea uchaguzi Zanzibar (chini ya mamlaka ya Tume yao).

Huo ndio utakuwa mwanzo wa kupatikana kwa Zanzibar huru na kuvunjika kwa muungano. Mark my words
 
Katika kosa ambalo CCM na Tanzania watajuta maisha yao ni kurejea uchaguzi Zanzibar (chini ya mamlaka ya Tume yao).

Huo ndio utakuwa mwanzo wa kupatikana kwa Zanzibar huru na kuvunjika kwa muungano. Mark my words

Haya nayo ni MANENO! Mwenye masikio na asikie!!
 
Nikiambiwa nitathmini hali halisi inayoendelea zanzibar kisha nitowe maana ya DEMOCRACY na DICTATOR SHIP mm nitashindwa kutofautisha.
 
Cuf na Maalim ...wakiamua kweli kweli hakuna uchaguzi haufanyiki.
mfano pemba wote 95% wakitaa haufanyiki.
Na unguja cuf siku ya uchaguzi wakiitisha mkutano mkubwa ..hakutakua na uchaguzi...Ccm wakubali tu kushindwa wamtangaze Maalim
 
Hakika kwa sababu zilizotolewa za kufuta uchaguzi, sidhani kama ZEC hii ina moral authority ya kuandaa uchaguzi mwinhine!
 
Hakika kwa sababu zilizotolewa za kufuta uchaguzi, sidhani kama ZEC hii ina moral authority ya kuandaa uchaguzi mwinhine!

Mpaka tarehe ya leo jecha yupo mafichoni hatujui atarudi lini.
 
Ninahasira na c.c.m!

Asili yetu waTz ni waswahili na wanafki . Swala la Zanzibar linaonyesha asili yetu!! Tunataka majirani zetu wamalize tofauti zao kwa dialogue wakati kwetu ni kiyume.

Tofauti ya Dr Shein na Laurence Bagbo ni kitu gani umeshindwa uchaguzi unang'ang'ania ofisini kumuongoza nani ???????????????!!. This is what we call USWAHILI
 
Back
Top Bottom