CUF UDSM yatoa pongezi kwa ajili ya uchaguzi wa Lindi

Sep 29, 2016
34
83
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)

JUMUIYA YA VIJANA (JUVICUF)

CUF VYUO VIKUU TAWI LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI-UDSM)

PONGEZI NYINGI KWA WANALINDI, CUF NA UKAWA KWA UJUMLA

CUF Chama Cha Wananchi tawi la Mlimani Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam tunayofuraha kubwa juu ya taarifa ya ushindi wa Chama Chetu katika uchaguzi mdogo wa marudio wa serikali ya mitaa uliofanyika machi 12 mwaka huu 2017.

Katika uchaguzi huo ulihusisha mitaa 7 na vyama shiriki ni CCM na CUF, katika uchaguzi huo chama Chetu kimefanikiwa kushinda mitaa yote 7 dhidi ya mitaa 0 iliyochukuliwa na CCM.

Tunajua kazi haikuwa rahisi kwetu kushinda hasa ukizingatia chama chetu kipo kwenye dimbwi kubwa la mgogoro ambao kwa kiasi kikubwa Sisi tawi la Mlimani tunakili kuwa mtu anyeitwa LIPUMBA anatumia nguvu kubwa sana kuhakikisha CUF haipati mafanikio kama alivyoagizwa kuifanya Kazi hiyo na Chama Chake Cha CCM.

Hivyo umoja na mshikamano wa wanalindi wote na kwa uzalendo mliouonesha kuwa CUF ni taasisi imara na mmekilinda chama kwa nguvu zote na kwenye mazingira magumu.

Tawi la Mlimani kwa juhudi zenu wanacuf wa Lindi tunawapa pongezi kubwa sana kwa kuhakikisha CUF taasisi inashinda uchaguzi huo.

CUF tawi la Mlimani pia linawapongeza wanachama, wadau na watu mbalimbali waliojitoa kwa muda, pesa na mali nyingine kuhakikisha kuwa wanasapoti kampeni za uchaguzi na hatimaye kushinda mitaa yote Saba.

Pia CUF tawi la Mlimani linawapongeza wanalindi wote bila kujali itikadi zao kwa kukichagua na kuwachagua viongozi wanaotokana na chama chetu ili waweze kuwaongoza Kwa kuwawakilisha na kusimamia maendeleo ndani ya mitaa yenu na kwa maamuzi yenu yameweza kukipa heshima kubwa chama chetu na tunawaomba muendelee kukiunga mkono chama chetu na pia tunawataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa ufanisi kama mnavyoagizwa na wananchi bila kujali itikadi zao za vyama kwani maendeleo hayana chama.

Vilevile tunakazia kwa kuwapa pongezi zaidi viongozi wa CUF wote wa Lindi na ngazi ya Taifa na JUVICUF kwa juhudi zao kubwa walizozifanya kuhakikisha chama kinashinda.

Mwisho kabisa tawi letu linawashukuru wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kwa ushirikiano wenu kwani tunajua na kutambua wafuasi wa CHADEMA, NCCR na NLD pasi na mashaka yoyote walikiunga mkono chama chetu kwa namna moja ama nyingine na tunawaomba tuendeleze umoja wetu ili kupata mafanikio zaidi.

CUF TAASISI IMARA

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliono CUF tawi la Mlimani

cufmlimani@gmail.com

0715428849
HAMISI KAPALILA
Afisa Habari na Mawasiliano tawi la CUF Mlimani

HAKI SAWA KWA WOTE
 
Back
Top Bottom