CUF sasa wamiliki migodi minane ya madini Tanga

CUF sasa wamiliki migodi minane ya madini Tanga

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
HABARI
[h=1][/h]
Na Hussein Semdoe, Handeni

Posted Jumatano,Januari16 2013 saa 21:52 PM

KWA UFUPI
Alisema wanaimiliki kihalali huku akionyesha vibali, hatua iliyolenga kujaribu kujisafisha, kufuatia kurushiwa tuhuma na Mlezi wa ADC Kanda ya Kaskazini, Hassan Doyo, aliyejiunga na chama hicho baada ya kutimuliwa CUF.

CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga kimewatahadharisha wananchi kuepuka kuwaunga mkono watu au viongozi wanaohamahama na kuanzisha vyama vya siasa, kikidai wanataka kujinufaisha binafsi.

“Acheni kuwaunga mkono watu wanaoanzisha vyama vipya, haiwezekani kwa mfano mtu umekaa CUF karibu miaka 20, leo unaanzisha chama kipya eti unahimiza watu wakufuate, haiwezekani,” alisema Katibu wa CUF Wilaya ya Handeni, Masoud Mjaila na kuongeza:
“Kwani hao watu umewachukua ‘msukule’ wakufuate kila unakotaka kwenda… Hapana, wakataeni.”

Mjaila alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wilayani hapa juzi, uliokuwa ukilenga kuweka mambo sawa, baada ya wiki iliyopita Chama cha ADC kukishambulia kwa kukituhumu kuanzisha migodi ya madini wilayani humo isiyokuwa na kibali.

Katika mkutano huo, Mjaila alikiri wana kampuni inayomiliki migodi minane ya madini mbalimbali Kijiji cha Sezakofi, Kata ya Ndolwa.

Alisema wanaimiliki kihalali huku akionyesha vibali, hatua iliyolenga kujaribu kujisafisha, kufuatia kurushiwa tuhuma na Mlezi wa ADC Kanda ya Kaskazini, Hassan Doyo, aliyejiunga na chama hicho baada ya kutimuliwa CUF.

“Wananchi msikubali kuburuzwa, hiki chama chenu cha CUF kina miaka 20 tangu kuanzishwa, hapa Handeni kina miaka 15, lakini mnaona hali ilivyo, ndiyo hivi karibuni sasa na sisi tupo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Mjaila na kuongeza:
“Sasa hawa ADC wameanza jana, leo wanataka waungwe mkono, hapana! Hawa wanatafuta masilahi yao maana huku CUF walifukuzwa.

“Eti wanasema migodi ile ya madini haina vibali, siyo kweli kwani serikali iko wapi, tumechangia zaidi ya Sh3.5 milioni, kusaidia miradi mbalimbali ya Serikali ya Kijiji cha Sezakofi.”

Alisema wanatambua vijembe hivyo vinatokana na fitina zilizojaa viongozi wa ADC, hawataki CUF wapate maendeleo.
Aliwashauri nao kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujipatia maendeleo badala ya malumbano majukwaani.

Katika mkutano huo, CUF kilitangaza kutoa msaada wa shuka 20 zenye thamani ya Sh180,000 hospitali ya wilaya hiyo.

Pia, walitoa sabuni zenye thamani ya Sh150,000.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa, Jumaa Magogo, alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo wanauziwa uji.

Magogo alisema kitendo hicho siyo cha kiungwana na kwamba, kinafanywa na mawakala waliopewa kazi ya kutoa huduma hiyo na halmashauri ya wilaya.

Kweli KATIBA inaruhusu VYAMA VYA KISIASA kumiliki NJIA kuu za KIUCHUMI?? Sasa Kama CAF yafanya HIVYO CCM si ITAZOA KILA KITU kabla ya 2015???

Kwahiyo na Sababu ya kupata kazi kwenye HIYO MIGUDI utalazimika kuwa Mwanachama wa CUF???

Kweli Jakaya Kikwete anatumaliza kwa hayo MADARAJA ya MIKOPO!!!
 
Mifumo ya Siasa za Afrika ni za ajabu kwelikweli!. Na Kazi za Wanasiasa (Wabunge, Rais, Watendaji wa Vyama, n.k) pamoja na Taasisi/Vyama vyao sijuhi kama vinafahamika na wao pamoja na Jamii?! Tumebadili Ubunge kuwa kazi ya kugawa hisani badala ya kuwawakilisha wananchi kwenye kutunga, kurekebisha sheria na kuisimamia serikali ili rasilimali za nchi yao ndizo zitumike vema katika kuwaletea maendeleo. Sasa tunasonga mbele kugeuza vyama vya siasa kuwa Mashirika ya Watoa Hisani! Swali la msingi; hizo hisani zinazalishwaje au zinatoka wapi na zinalipwaje?
..Katika mkutano huo, CUF kilitangaza kutoa msaada wa shuka 20 zenye thamani ya Sh180,000 hospitali ya wilaya hiyo.Pia, walitoa sabuni zenye thamani ya Sh150,000....
V/S
CCM+Kampeni.png

​
 
Kweli KATIBA inaruhusu VYAMA VYA KISIASA kumiliki NJIA kuu za KIUCHUMI?? Sasa Kama CAF yafanya HIVYO CCM si ITAZOA KILA KITU kabla ya 2015???

Kwahiyo na Sababu ya kupata kazi kwenye HIYO MIGUDI utalazimika kuwa Mwanachama wa CUF???

Kweli Jakaya Kikwete anatumaliza kwa hayo MADARAJA ya MIKOPO!!!
ccm wanamiliki viwanja vya mpira kila mkoa,majengo ya kupangisha ya kumwaga tu.......kwa hiyo sioni tatizo na hiyo itavisaidia vyama kuondokana na utegemezi wa ruzuku
 
CUF wanamiliki kihalali vitegauchumi vya walivyo vitafuta kama chama bali CCM imejimilikisha Mali na vitegauchumi mbalimbali vya uma na kuvitumia kwa manufaa ya chama. Mfano majengo, kumbi na viwanja vya mpira.
 
Hatua hiyo tunaipongeza kama ni kweli, lakini isijekuwa ni miradi ya watu wachache ndani ya Chama
 
ccm wanamiliki viwanja vya mpira kila mkoa,majengo ya kupangisha ya kumwaga tu.......kwa hiyo sioni tatizo na hiyo itavisaidia vyama kuondokana na utegemezi wa ruzuku

HIVYO VIWANJA vya MIPIRA wananchi kwa UJUMLA walikatwa kodi KUVIJENGA hivyo SIO MALI ya CCM; ni kwasababu tu CCM iko MADARAKANI waking'atuka utaona kuna SHERIA vitarudishwa kwa WANANCHI

Nadhani Unakumbuka KANU ilipodondoka... KASARANI ikarudi kwa Wananchi; KENYATTA CONFRENCE CENTER ikarudi kwenye SERIKALI; Gazeti la STANDARD likafa kama hapa tuna UHURU na MZALENDO...

Majengo waliyoyabeba bila kulipia yalichukuliwa... KANU sasa hivi ni JINA TUUUU... VINGI VILIKUWA vya VIONGOZI

Kwahiyo CCM vyote walivyonavyo hawakuvipata KIUHALALI vitarudi MIKONONI mwa WANANCHI
 
Yaani hawa CUF kumbe wana utajiri wote huo ila wanashindwa kuendesha V4C yao nchi nzima!!!!!!
Inaelekea hawako serious katika siasa, baada ya kufunga ndoa na ccm wameridhika na maisha.
 
Hivi madini hayo yangegundulika znz na Chadema ndiyo wamiliki hiyo migodi wapemba wangekubali kweli? Inabidi watuheshimu sana na waache kuchoma makanisa.
 
HIVYO VIWANJA vya MIPIRA wananchi kwa UJUMLA walikatwa kodi KUVIJENGA hivyo SIO MALI ya CCM; ni kwasababu tu CCM iko MADARAKANI waking'atuka utaona kuna SHERIA vitarudishwa kwa WANANCHI

Nadhani Unakumbuka KANU ilipodondoka... KASARANI ikarudi kwa Wananchi; KENYATTA CONFRENCE CENTER ikarudi kwenye SERIKALI; Gazeti la STANDARD likafa kama hapa tuna UHURU na MZALENDO...

Majengo waliyoyabeba bila kulipia yalichukuliwa... KANU sasa hivi ni JINA TUUUU... VINGI VILIKUWA vya VIONGOZI

Kwahiyo CCM vyote walivyonavyo hawakuvipata KIUHALALI vitarudi MIKONONI mwa WANANCHI
Kuhusu umiliki wahizo mali za ccm naungana na wewe kwamba kiuhalisia ni mali ya wananchi wote lakini pointi inabaki palepale kuna umuhimu wa vyama vya siasa kuwa na vitega uchumi ili kuondokana na utegemezi wa ruzuku mwisho wa siku vyama vinakuwa dhaifu kiuchumi na hivyo kushindwa kuendesha harakati za kisiasa
 
Generally political parties exist on donations from the public and from corporations or wealthy people, supposedly in the name of helping the country, but often for what they hope to get from the officials or party that they donate to... And not owning MINES or Industries...

Unajua POLITICAL PARTY kazi yake ni kutunga SHERIA na kusaidia NCHI KUENDELEA kisiasa kibishara na kiuchumi sasa wakianza kumiliki njia kuu za UCHUMI nani atakaa bungeni kutunga SHERIA au kilinda SHERIA za NCHI???? HILO NI KOSA KUBWA KWELI.... SIJUI NCHI YETU INAKWENDA WAPI...

Political parties are funded by contributions from

  • party members and other individuals,

  • organizations which share their political ideas or who stand to benefit from their activities or

  • governmental public funding
 
the contents of the above paragraph withoutprejudice is admitted.
 
Jamani huu ni muda wa kujiuliza kabla hatujasahau masuala ya kampuni ya Deep green ya CCM na Meremeta yaliyoleta wizi mtakatifu katika historia yetu ya vyama vingi nchini! Tunaanza kushuhudia chama cha siasa cha CUF kinachojipambanua kwa siasa za kinazi za Zanzibar kujitenga kikianza kumiliki vitalu vya uchimbaji dhahabu huko Tanga huku kikinyemelea vitalu vya uchimbaji wa gesi huko kusini! Cha kustaajabisha chama hichi kinatumia sintofahamu ya wenyeji wa huko katika kuwarubuni wananchi wao kukataa ujenzi wa bomba lagesi kupitia viongozi wao wa kidini misikitini. Je kwa mwenendo huu, ni haki kunyamaza kimya wakati uhuru wetu na utaifa wetu ukimumunyika kwa sababu tu ya uroho wa madaraka ya wale wanaofahamika kuwa vinara wa kuigawa hii nchi? kuanzia Zanzibar mpaka sasa Pwani huku wakijitwalia vitalu vya uchimbaji madini na mafuta kama vile kampuni ya biashara? uhalali wa vyama vya siasa kujihusisha na biashara ya rasilimali za madini bara huku wakikemea ubadhirifu katika sekta hiyohiyo unatoka wapi? mbona wasimiliki vitalu Zanzibar? Naomba tutafakari hili...
 
Kama hutaki watz wenzetu wamiliki vitalu sasa wewe unataka nani amiliki? Kama wamepata kihalali kuna tatizo gani. Sheria haizuii vyama vya siasa kufanya biashara.
 
Kama hutaki watz wenzetu wamiliki vitalu sasa wewe unataka nani amiliki? Kama wamepata kihalali kuna tatizo gani. Sheria haizuii vyama vya siasa kufanya biashara.
Utanzania unakuja kwenye umiliki wa rasirimali za Bara tu ila si za Zanzibar sio! Jussa si alipinga masuala ya gesi na mafuta kuwa ya Muungano ila haya ya rasilimali za Tanga, Mtwara na Lindi yupo kimya...! na tangu lini chama cha siasa kikafanya biashara ya utafutaji dhahabu?
 
Back
Top Bottom