Cuf na Lipumba siwasomi

REBEL

Senior Member
Dec 15, 2010
166
64
Utangulizi.
Leo nataka kuzungumzia Chama kilichokuwa na nguvu sana miaka iliyopita(sana sana miaka ya 1995-2000) nacho si kingine bali ni CUF.CUF Kilikuwa chama chenye nguvu sana na kilichopendwa na watanzania wote bila kujali rangi,dini wala kabila la watu.Wakati ule kilikuwa ngangari sana katika medani za siasa za Tanzania chini ya uongozi makini wa Prof.Lipumba na Maalim Seif.

Siasa ya sasa na CUF
Miaka ya sasa CUF imekosa mvuto kabisa kwa jamii ya Tanzania.Mimi nadhani sababu kubwa imechangiwa na viongozi wao kuongea mambo ambayo hayana mvuto kwa watanzania wa sasa.mosi,Mara nyingi nimekuwa nikiangalia Prof.Lipumba katika mahojiano au hotuba zake amekuwa akimsifia sana kikwete kama vile yeye sio mwenyekiti wa chama cha upinzani.na mara nyingine wamekuwa kama ni wasemaji wa CCM katika mahojihano mengi.Pili, kila mtu anajua watu wanaotoa kauli tata kama Jussa na yule mkuu wa itikadi wa cuf ambazo simejaa udini na ubaguzi kwa watu wa bara na kuonyesha waziwazi chuki kwa baba wa taifa(sitaliongelea hili maana linaitaji maada nyingine).
Swali:mnadhani CUF inaweza kufanikiwa Tanzania hii ya leo kwa watu kama hao?
jibu ni rahisi tu hapana.
Cuf wanaitaji kubadilika kulingana na siasa za sasa.
Inabidi ibadilike kama inataka kushindana katika siasa za sasa ambazo ni za ushindani.na wajue watu wa Tanzania ni waelewa wa mambo wasiodanganyika kwa siasa za kipropaganda na waache kuwa na mahaba na kikwete(yeye sio mwenyekiti wao).Na Lipumba hana mvuto tena hawape watu wengine waongoze chama katika itikadi zinazoeleweka.Maana CCM siku hizi inakiona Cuf kama kivuli tu!
 
Back
Top Bottom