CUF: Msajili wa vyama vya siasa usikubali kutumika

CUF: Msajili wa vyama vya siasa usikubali kutumika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

"MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA USIKUBALI KUTUMIKA KUKIYUMBISHA"

Imetolewa leo Tarehe -15/9/2016,
Na, WAABUNGE WA CHAMA CHA WANANCHI-CUF, DODOMA.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi wabunge wa THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi) tunapenda kutumia fursa hii kumnasihi Msajiri wa vyama vya siasa nchini Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi kutokubali kutumika kukiyumbisha chama chetu cha CUF kutokana na baadhi ya wanachama wenye nia ovu dhidi ya CUF wakishirikiana na vyombo vya dola na serikali ya CCM kutaka kuitumia ofisi yake kwa madhumuni hayo.

Ndugu waandishi wa habari,
Kama tunavyofahamu, mwaka jana tarehe 5 Agosti, aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahimu Lipumba kwa hiyari yake mwenyewe alijiuzuru uenyekiti wa CUF Taifa kwa kuutangazia umma wa watanzania pale Peacock Hotel na kumuandikia rasmi Katibu Mkuu wa CUF juu ya uamuzi huo na baadaye akaelekea nchini Rwanda kwa kazi aliyodai kuwa za utafiti wa kiuchumi ili aje kuisaidia serikali ijayo ambayo kwa vyovyote alitegemea kuwa itakuwa ni ya CCM.

Chama cha CUF na wagombea wake wote nchi nzima tuliendelea na kampeni bila msaada wala ushawishi wa Prof Lipumba na baada ya uchaguzi chama chetu kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287, kuongoza Manispaa mbili na Halmashauri za wilaya tatu. Pia kwa ushirikiano na vyama rafiki vya UKAWA tumeweza kupata viongozi katika manispaa mbili za Jiji la Dar es Salaam pamoja na kuongoza jiji lenyewe.

Baada ya chama kupita katika wakati mgumu chini ya uongozi wa mpito na kupata mafanikio makubwa bila Prof. Lipumba, Baraza kuu la Uongozi Taifa katika kikao chake cha tarehe 2-3 April, 2016 liliamua kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa kujaza nafasi wazi za uongozi ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.

Maandalizi ya Kikao cha Mkutano Mkuu yalikamilika na mkutano huo kufanyika Ubungo Plaza (Blue Pearl Hotel) tarehe 21/8/2015. Mkutano Mkuu Maalum huo ulikuwa na ajenda mbili, ajenda ya kwanza ilikuwa ni kukamilisha matakwa ya ibara ya 117 (2) ya Katiba ya CUF inayoongelea mamlaka ya mkutano mkuu kukubali kujiuzulu kwa kiongozi ambaye amechaguliwa na au kuteuliwa na ngazi husika.

Wajumbe 476 sawa na asilimia 70 ya wajumbe wote waliohudhuria mkutano mkuu huo walithibitisha na kukubali kujiuzulu kwa Prof Ibrahimu Lipumba na ajenda ya kwanza ikakamilika.

Katika hali isiyotarajiwa na bila mualiko rasmi Prof Lipumba aliingia kwa nguvu ndani ya ukumbi wa mkutano na kusababisha kuzuka kwa vurugu kubwa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wachache waliokuwa wanamuunga mkono. Hata hivyo vurugu hizo zilidhibitiwa na mkutano ukarejea na kuendelea kwa amani na ajenda kwanza ikajadiliwa na kufanyiwa maamuzi.

Kikao kiliporejea baada ya mapumziko ya mchana kiliendelea na ajenda ya pili ya kujaza nafasi wazi za viongozi ikiwemo ya Mwenyekiti wa chama Taifa. Ghafla wakati kamati ya uchaguzi ya ndani ya chama ikianza majukumu yake kundi la vijana wahuni lililokodiwa kuja kufanya vurugu kwa ajili ya kumsaidia Prof Lipumba lilivamia ukumbi na kusababisha vurugu kubwa hali iliyopelekea mwenyekiti wa mkutano kuuahirisha rasmi mkutano huo bila ya kukamilisha ajenda ya pili.

Vurugu hizo zimekisababishia Chama hasara kubwa ya takribani Shilingi milioni 600 za Kitanzania na uharibifu wa mali za hotel kiasi cha shilingi milioni 8.7. Hali hii inadhihirisha wazi kuwa Prof Lipumba hakuwa na nia njema na alidhamiria kuvuruga mustakbali wa Chama.

Baraza Kuu la Uongozi la CUF Taifa lililokutana, kwa mujibu wa Katiba, tarehe 28/8/2016 lilifanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama wanachama kadhaa akiwemo Prof Lipumba na Magdalena Sakaya (Naibu Katibu Mkuu Bara) na kumvua uanachama Mhe. Shashu Lugeye baada ya kupewa nafasi ya kujitetea na kusikilizwa. Wanachama waliosimamishwa wameshaandikiwa barua za kujulishwa juu ya uamuzi huo ambao pia unawapa nafasi ya kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CUF.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi wabunge tunaotokana na chama cha CUF katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaunga mkono hatua ya Baraza kuu la uongozi Taifa kuwachukulia hatua za kinidhamu wanachama wote waliohusika na vitendo vinavyokiuka katiba ya chama chetu, malengo yake na utamaduni wake.

Baada ya hatua hizo za Baraza Kuu la uongozi la Taifa ambazo kwa kweli bado zinaendelea, tulipata taarifa kuwa Prof. Lipumba na wenzake walipeleka malalamiko yao kwa Msajili wa vyama vya siasa, lakini pia tumemshuhudia akiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari akijitangaza kuwa yeye ndiye ‘mwenyekiti halali’ wa CUF na kwamba anasubiria tu barua ya Msajili wa vyama vya siasa ili kuthibitishiwa uenyekiti wake.

Prof Lipumba anafanya haya huku akitambua kuwa Baraza Kuu lililokutana tarehe 28 Agosti, 2016 likiwa na akidi halali pande zote za muungano, lilikwishateua kamati ya Uongozi wa Chama Taifa ambayo inapaswa kufanya na kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Mwenyekiti Taifa kwa mujibu wa katiba yetu.

Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena Prof. Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF, kwa sasa CUF inaongozwa na Kamati ya Uongozi ya CUF Taifa chini ya Mheshimiwa Julius Sunday Mtatiro. Haya yote yamefanywa kwa mujibu wa katiba ya CUF na vikao halali vya CUF.

Hata hivyo, tumepata taarifa kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika serikalini kuwa kuna njama zinazopangwa na washindani wetu wa kisiasa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyombo vya ulinzi na usalama na serikali ya CCM kutaka kuitumia ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kumtangaza Prof Ibrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF. Dhumuni la yote hayo ni kutaka kukiyumbisha chama chetu na kutupandikizia mgogoro usiopaswa kuwepo.

Kama kitendo hicho kikifanyika kitakuwa kinyume kabisa na katiba, kanuni na taratibu za chama chetu, lakini kitakuwa kinyume na sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 ambayo haitoi mamlaka yoyote kwa Msajili wa vyama vya siasa kukipangia chama cha siasa viongozi wake.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi kama wabunge na wawakilishi wa wananchi, tunatoa tahadhari kwa Msajili wa vyama vya siasa na wale wote wanaotaka kutumika kukiingiza chama chetu cha CUF katika mgogoro usiopaswa kuwepo na kurudisha nyuma jitihada za kudai haki na demokrasia ndani ya nchi yetu, kuacha njama hizo mara moja kwa sababu tumekwishazibaini na kwa gharama yoyote tuko tayari kukilinda chama chetu na kushirikiana na uongozi halali uliopo dhidi ya maadui wa ndani na nje. Tunawahakikishia watanzania kwamba maadui hawa hawatafanikiwa kutuyumbisha.

Tunao uhakika kuwa Chama chetu kimefuata taratibu zote za kikatiba kushughulikia suala hili na kwamba katiba ya CUF haitoi nafasi kwa kiongozi aliyejiuzuru kwa hiyari yake mwenyewe kutengua maamuzi yake ya kujiuzulu. Mamlaka iliyomchagua kwa mujibu wa ibara ya 117(2) ya Katiba ya CUF imekamilisha wajibu wake katika Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika Blue Pearl hotel tarehe 21/8/2016.

Tunashangazwa ni katiba ipi ya CUF ambayo vyombo vya ulinzi na usalama, CCM na serikali yake vinataka kuitumia ili kumuuzia Msajili kesi ya kumrejesha Prof Lipumba madarakani? Tunamtahadharisha Msajili wa vyama vya siasa atakapotoa maoni yake kuhusu malalamiko yoyote yaliyopelekwa kwake asikubali kujivunjia heshima yake kubwa akiwa Jaji aliyehudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa vyovyote vile maoni na ushauri wa Msajili juu ya jambo hili hayapaswi kwenda kinyuma na katiba ya CUF, Sheria ya vyama vya siasa na kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa nchini. Katika kile kinachoonekana kuwa Msajili anaweza kushiriki katika njama hizo ovu, tayari Prof. Lipumba na timu ya watu wachache wanaomuunga mkono wameanza maandalizi mbalimbali ya kuchapisha fulana za kumpokea katika Ofisi Kuu ya CUF muda wowote kuanzia sasa na kinachosubiriwa ni tangazo la Msajiri wa vyama vya siasa kama ambavyo Prof. Lipumba amekuwa akitangaza kwenye vyombo vya habari.

Mpango wa kuendelea kumlinda Lipumba (kama ambavyo Polisi walikubali kutumika na kumlinda yeye na makundi ya vijana waliovamia na kuufanya mkutano mkuu maalumu wa Agosti 21 uahirishwe bila kumaliza ajenda ya pili kwa sababu za kiusalama) unasukwa kwa njama za juu na tunazo taarifa kuwa wanaandaliwa watu watakaovamia na kuiteka Ofisi Kuu ya CUF Buguruni, kufanya vurugu na kumsimika Prof. Lipumba kwenye nafasi ya uenyekiti na baadaye kusaidiwa na serikali ya CCM kuzunguka nchi nzima kufanya vikao vya ndani ili kujaribu kuimaliza CUF. Njama zote hizi tunazijua.

Sisi wabunge wa CUF ambao ni wawakilishi wa wananchi tutasimama imara kukilinda na kukitetea chama chetu dhidi ya njama zote hizo. Tutaendelea kupambana na yeyote ambaye ataonekana anataka kutumiwa kukivuruga chama na hatutakubali kuyumbishwa. Tunatambua umuhimu wa kuheshimu katiba za vyama na kuheshimu maamuzi halali ya vikao halali vya vyama vya siasa.

Kwa vyovyote vile hatutegemei kuwa Msajili wa vyama vya siasa atakubali kutumika katika mkakati huu uliojaa uovu. Pamoja na kumheshimu sana, tunatumia fursa hii kumtahadharisha kwamba CUF iko macho, inajua yanayoendelea kila pembe ya nchi na tuko tayari kuyakabili.

Ndugu waandishi wa habari,
Tunatumia fursa hii pia kumshauri Prof. Lipumba na kumjulisha kuwa tunamheshimu sana na aliyokitendea chama hiki yanatosha. Haiwezekani Prof. Lipumba huyu huyu tumjuaye na ambaye huko nyuma amewahi kusimamia maamuzi ya Baraza Kuu na mikutano mikuu kadhaa ya CUF, leo aanze kuzunguka huku na kule kupinga maamuzi ya mikutano hiyo.

Ni Prof. Lipumba huyu huyu ndiye alisimamia vikao vya Baraza Kuu vilivyopitia madai na tuhuma kwa baadhi ya viongozi wa chama na akasimamia maamuzi ya hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi hao. Mmoja wa viongozi waliowahi kuchukuliwa hatua kali mtakumbuka ni Ndugu. Chief Lutayosa Yemba.

Hiyo ina maana kuwa katiba ya CUF inayo mamlaka juu ya wanachama wote akiwemo yeye Lipumba. Kwa sababu hivi sasa ameshasimamishwa uanachama ni vema atoe ushirikiano kwa chama katika hatua zinazofuata za kusikiliza utetezi wake na kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya chama. Chama cha CUF ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini na kamwe haitakubali kuyumba wala kuyumbishwa kwa namna yeyote ile.

Tunatoa wito kwa wanachama wenzetu wote na viongozi kwa ujumla kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki na tuelekeze nguvu zetu katika kukiimarisha zaidi chama chetu ili kwa kushirikiana na vyama rafiki ndani ya UKAWA tuweze kupigania haki na demokrasia inayoonekanwa kutaka kubanwa na utawala wa serikali ya awamu hii ya tano.

"HAKI SAWA KWA WOTE"
IMETOLEWA NA WABUNGE WA CUF LEO TAREHE 15 SEPT 2016.

RIZIKI SHAHARI MNGWALI -
KIONGOZI WA WABUNGE WA CUF

JUMA KOMBO HAMAD - KATIBU WA WABUNGE WA CUF.
 
Lipumba ataaibika vibaya sana ! Huyu ni profesa wa namna gani ?

Mkuu Mutungi kuwa makini sana na kutumika , aibu yote itakuelemea , fanya utafiti , cuf haijawahi kushindwa na wasaliti , yuko wapi mapalala ?
 
THE CIVIC UNITED FRONT

(CUF – Chama Cha Wananchi)





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

"MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA USIKUBALI KUTUMIKA KUKIYUMBISHA"

Imetolewa leo Tarehe -15/9/2016,
Na, WAABUNGE WA CHAMA CHA WANANCHI-CUF, DODOMA.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi wabunge wa THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi) tunapenda kutumia fursa hii kumnasihi Msajiri wa vyama vya siasa nchini Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi kutokubali kutumika kukiyumbisha chama chetu cha CUF kutokana na baadhi ya wanachama wenye nia ovu dhidi ya CUF wakishirikiana na vyombo vya dola na serikali ya CCM kutaka kuitumia ofisi yake kwa madhumuni hayo.

Ndugu waandishi wa habari,
Kama tunavyofahamu, mwaka jana tarehe 5 Agosti, aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahimu Lipumba kwa hiyari yake mwenyewe alijiuzuru uenyekiti wa CUF Taifa kwa kuutangazia umma wa watanzania pale Peacock Hotel na kumuandikia rasmi Katibu Mkuu wa CUF juu ya uamuzi huo na baadaye akaelekea nchini Rwanda kwa kazi aliyodai kuwa za utafiti wa kiuchumi ili aje kuisaidia serikali ijayo ambayo kwa vyovyote alitegemea kuwa itakuwa ni ya CCM.

Chama cha CUF na wagombea wake wote nchi nzima tuliendelea na kampeni bila msaada wala ushawishi wa Prof Lipumba na baada ya uchaguzi chama chetu kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287, kuongoza Manispaa mbili na Halmashauri za wilaya tatu. Pia kwa ushirikiano na vyama rafiki vya UKAWA tumeweza kupata viongozi katika manispaa mbili za Jiji la Dar es Salaam pamoja na kuongoza jiji lenyewe.

Baada ya chama kupita katika wakati mgumu chini ya uongozi wa mpito na kupata mafanikio makubwa bila Prof. Lipumba, Baraza kuu la Uongozi Taifa katika kikao chake cha tarehe 2-3 April, 2016 liliamua kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa kujaza nafasi wazi za uongozi ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.

Maandalizi ya Kikao cha Mkutano Mkuu yalikamilika na mkutano huo kufanyika Ubungo Plaza (Blue Pearl Hotel) tarehe 21/8/2015. Mkutano Mkuu Maalum huo ulikuwa na ajenda mbili, ajenda ya kwanza ilikuwa ni kukamilisha matakwa ya ibara ya 117 (2) ya Katiba ya CUF inayoongelea mamlaka ya mkutano mkuu kukubali kujiuzulu kwa kiongozi ambaye amechaguliwa na au kuteuliwa na ngazi husika. Wajumbe 476 sawa na asilimia 70 ya wajumbe wote waliohudhuria mkutano mkuu huo walithibitisha na kukubali kujiuzulu kwa Prof Ibrahimu Lipumba na ajenda ya kwanza ikakamilika.

Katika hali isiyotarajiwa na bila mualiko rasmi Prof Lipumba aliingia kwa nguvu ndani ya ukumbi wa mkutano na kusababisha kuzuka kwa vurugu kubwa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wachache waliokuwa wanamuunga mkono. Hata hivyo vurugu hizo zilidhibitiwa na mkutano ukarejea na kuendelea kwa amani na ajenda kwanza ikajadiliwa na kufanyiwa maamuzi.

Kikao kiliporejea baada ya mapumziko ya mchana kiliendelea na ajenda ya pili ya kujaza nafasi wazi za viongozi ikiwemo ya Mwenyekiti wa chama Taifa. Ghafla wakati kamati ya uchaguzi ya ndani ya chama ikianza majukumu yake kundi la vijana wahuni lililokodiwa kuja kufanya vurugu kwa ajili ya kumsaidia Prof Lipumba lilivamia ukumbi na kusababisha vurugu kubwa hali iliyopelekea mwenyekiti wa mkutano kuuahirisha rasmi mkutano huo bila ya kukamilisha ajenda ya pili.

Vurugu hizo zimekisababishia Chama hasara kubwa ya takribani Shilingi milioni 600 za Kitanzania na uharibifu wa mali za hotel kiasi cha shilingi milioni 8.7. Hali hii inadhihirisha wazi kuwa Prof Lipumba hakuwa na nia njema na alidhamiria kuvuruga mustakbali wa Chama.

Baraza Kuu la Uongozi la CUF Taifa lililokutana, kwa mujibu wa Katiba, tarehe 28/8/2016 lilifanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama wanachama kadhaa akiwemo Prof Lipumba na Magdalena Sakaya (Naibu Katibu Mkuu Bara) na kumvua uanachama Mhe. Shashu Lugeye baada ya kupewa nafasi ya kujitetea na kusikilizwa. Wanachama waliosimamishwa wameshaandikiwa barua za kujulishwa juu ya uamuzi huo ambao pia unawapa nafasi ya kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CUF.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi wabunge tunaotokana na chama cha CUF katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaunga mkono hatua ya Baraza kuu la uongozi Taifa kuwachukulia hatua za kinidhamu wanachama wote waliohusika na vitendo vinavyokiuka katiba ya chama chetu, malengo yake na utamaduni wake. Baada ya hatua hizo za Baraza Kuu la uongozi la Taifa ambazo kwa kweli bado zinaendelea, tulipata taarifa kuwa Prof. Lipumba na wenzake walipeleka malalamiko yao kwa Msajili wa vyama vya siasa, lakini pia tumemshuhudia akiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari akijitangaza kuwa yeye ndiye ‘mwenyekiti halali’ wa CUF na kwamba anasubiria tu barua ya Msajili wa vyama vya siasa ili kuthibitishiwa uenyekiti wake.

Prof Lipumba anafanya haya huku akitambua kuwa Baraza Kuu lililokutana tarehe 28 Agosti, 2016 likiwa na akidi halali pande zote za muungano, lilikwishateua kamati ya Uongozi wa Chama Taifa ambayo inapaswa kufanya na kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Mwenyekiti Taifa kwa mujibu wa katiba yetu. Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena Prof. Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF, kwa sasa CUF inaongozwa na Kamati ya Uongozi ya CUF Taifa chini ya Mheshimiwa Julius Sunday Mtatiro. Haya yote yamefanywa kwa mujibu wa katiba ya CUF na vikao halali vya CUF.

Hata hivyo, tumepata taarifa kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika serikalini kuwa kuna njama zinazopangwa na washindani wetu wa kisiasa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyombo vya ulinzi na usalama na serikali ya CCM kutaka kuitumia ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kumtangaza Prof Ibrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF. Dhumuni la yote hayo ni kutaka kukiyumbisha chama chetu na kutupandikizia mgogoro usiopaswa kuwepo. Kama kitendo hicho kikifanyika kitakuwa kinyume kabisa na katiba, kanuni na taratibu za chama chetu, lakini kitakuwa kinyume na sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 ambayo haitoi mamlaka yoyote kwa Msajili wa vyama vya siasa kukipangia chama cha siasa viongozi wake.

Ndugu waandishi wa habari,
Sisi kama wabunge na wawakilishi wa wananchi, tunatoa tahadhari kwa Msajili wa vyama vya siasa na wale wote wanaotaka kutumika kukiingiza chama chetu cha CUF katika mgogoro usiopaswa kuwepo na kurudisha nyuma jitihada za kudai haki na demokrasia ndani ya nchi yetu, kuacha njama hizo mara moja kwa sababu tumekwishazibaini na kwa gharama yoyote tuko tayari kukilinda chama chetu na kushirikiana na uongozi halali uliopo dhidi ya maadui wa ndani na nje. Tunawahakikishia watanzania kwamba maadui hawa hawatafanikiwa kutuyumbisha.

Tunao uhakika kuwa Chama chetu kimefuata taratibu zote za kikatiba kushughulikia suala hili na kwamba katiba ya CUF haitoi nafasi kwa kiongozi aliyejiuzuru kwa hiyari yake mwenyewe kutengua maamuzi yake ya kujiuzulu. Mamlaka iliyomchagua kwa mujibu wa ibara ya 117(2) ya Katiba ya CUF imekamilisha wajibu wake katika Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika Blue Pearl hotel tarehe 21/8/2016.

Tunashangazwa ni katiba ipi ya CUF ambayo vyombo vya ulinzi na usalama, CCM na serikali yake vinataka kuitumia ili kumuuzia Msajili kesi ya kumrejesha Prof Lipumba madarakani? Tunamtahadharisha Msajili wa vyama vya siasa atakapotoa maoni yake kuhusu malalamiko yoyote yaliyopelekwa kwake asikubali kujivunjia heshima yake kubwa akiwa Jaji aliyehudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa vyovyote vile maoni na ushauri wa Msajili juu ya jambo hili hayapaswi kwenda kinyuma na katiba ya CUF, Sheria ya vyama vya siasa na kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa nchini. Katika kile kinachoonekana kuwa Msajili anaweza kushiriki katika njama hizo ovu, tayari Prof. Lipumba na timu ya watu wachache wanaomuunga mkono wameanza maandalizi mbalimbali ya kuchapisha fulana za kumpokea katika Ofisi Kuu ya CUF muda wowote kuanzia sasa na kinachosubiriwa ni tangazo la Msajiri wa vyama vya siasa kama ambavyo Prof. Lipumba amekuwa akitangaza kwenye vyombo vya habari.

Mpango wa kuendelea kumlinda Lipumba (kama ambavyo Polisi walikubali kutumika na kumlinda yeye na makundi ya vijana waliovamia na kuufanya mkutano mkuu maalumu wa Agosti 21 uahirishwe bila kumaliza ajenda ya pili kwa sababu za kiusalama) unasukwa kwa njama za juu na tunazo taarifa kuwa wanaandaliwa watu watakaovamia na kuiteka Ofisi Kuu ya CUF Buguruni, kufanya vurugu na kumsimika Prof. Lipumba kwenye nafasi ya uenyekiti na baadaye kusaidiwa na serikali ya CCM kuzunguka nchi nzima kufanya vikao vya ndani ili kujaribu kuimaliza CUF. Njama zote hizi tunazijua.

Sisi wabunge wa CUF ambao ni wawakilishi wa wananchi tutasimama imara kukilinda na kukitetea chama chetu dhidi ya njama zote hizo. Tutaendelea kupambana na yeyote ambaye ataonekana anataka kutumiwa kukivuruga chama na hatutakubali kuyumbishwa. Tunatambua umuhimu wa kuheshimu katiba za vyama na kuheshimu maamuzi halali ya vikao halali vya vyama vya siasa. Kwa vyovyote vile hatutegemei kuwa Msajili wa vyama vya siasa atakubali kutumika katika mkakati huu uliojaa uovu. Pamoja na kumheshimu sana, tunatumia fursa hii kumtahadharisha kwamba CUF iko macho, inajua yanayoendelea kila pembe ya nchi na tuko tayari kuyakabili.

Ndugu waandishi wa habari,
Tunatumia fursa hii pia kumshauri Prof. Lipumba na kumjulisha kuwa tunamheshimu sana na aliyokitendea chama hiki yanatosha. Haiwezekani Prof. Lipumba huyu huyu tumjuaye na ambaye huko nyuma amewahi kusimamia maamuzi ya Baraza Kuu na mikutano mikuu kadhaa ya CUF, leo aanze kuzunguka huku na kule kupinga maamuzi ya mikutano hiyo.

Ni Prof. Lipumba huyu huyu ndiye alisimamia vikao vya Baraza Kuu vilivyopitia madai na tuhuma kwa baadhi ya viongozi wa chama na akasimamia maamuzi ya hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi hao. Mmoja wa viongozi waliowahi kuchukuliwa hatua kali mtakumbuka ni Ndugu. Chief Lutayosa Yemba. Hiyo ina maana kuwa katiba ya CUF inayo mamlaka juu ya wanachama wote akiwemo yeye Lipumba. Kwa sababu hivi sasa ameshasimamishwa uanachama ni vema atoe ushirikiano kwa chama katika hatua zinazofuata za kusikiliza utetezi wake na kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya chama. Chama cha CUF ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini na kamwe haitakubali kuyumba wala kuyumbishwa kwa namna yeyote ile.

Tunatoa wito kwa wanachama wenzetu wote na viongozi kwa ujumla kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki na tuelekeze nguvu zetu katika kukiimarisha zaidi chama chetu ili kwa kushirikiana na vyama rafiki ndani ya UKAWA tuweze kupigania haki na demokrasia inayoonekanwa kutaka kubanwa na utawala wa serikali ya awamu hii ya tano.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

IMETOLEWA NA WABUNGE WA CUF LEO TAREHE 15 SEPT 2016.

RIZIKI SHAHARI MNGWALI -
KIONGOZI WA WABUNGE WA CUF

JUMA KOMBO HAMAD - KATIBU WA WABUNGE WA CUF.
Hahaaa...ccm wametuma tena bundi mwingine.

----- TRUMPLIZATION-----
 
kuna kitu gani Lipumba amekisahau Cuf?
Hivi nyie wana demokrasia wa kweli mbona mnamuhujumu profesa lipumba hadharani? Tutawapuuza kama mlivyopuuzwa na wananchi 2015. CHADEMA wamenunua hii kesi kama ya kwao kwa sababu za hujuma tuuh hadharani mnadiriki kuwawekea hadi walinzi wa kuwalinda kwenye mkutano wao na kununua wanachama feki kuja kuhujumu hali halisi na MTU wa watu profesa mtahukumiwa hadi siku ya mwisho naandika haya nikiwa naona machungu mnayoyafanya mnastaili ata kulaaniwa
 
Huyu profesa mbona anafanya wasomi wadharaulike kazi ya kufanya utafiti Rwanda kwani waliokutuma ni cuf au nenda kwa waliokutuma kazi ya utafiti Rwanda cuf una nafasi tena kwani ulivyorudi Rwanda si ulikutana naye mwambie tu akupe kazi kama mwenzako wa kiraracha
 
Dah....safari hii naona mafisadi wameingia tena choo cha kike.....[emoji4]
 
lipumba akimaliza kuivuruga cuf ndio atapewa kazi ya ushauri
 
Lipumba sasa atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa BAKWATA.
 
Haya ndio maajabu ya siasa za Bongo,
Chadema leo hii wamekuwa wa kuleta habari za Cuf na kuwa watetezi wa CUF hasa Maalim na Mtatiro wakati huo huo Ccm wamekuwa watetezi wa Prof. Lipumba.
Mwisho wa siku haki itasimama sehemu yake ni suala la muda tu.
 
Sarakasi zote hizi za CCM na washirika wake ni kutaka LIPUMBA arejee CUF kwa lazima.
 
Haya ndio maajabu ya siasa za Bongo,
Chadema leo hii wamekuwa wa kuleta habari za Cuf na kuwa watetezi wa CUF hasa Maalim na Mtatiro wakati huo huo Ccm wamekuwa watetezi wa Prof. Lipumba.
Mwisho wa siku haki itasimama sehemu yake ni suala la muda tu.
CHADEMA wana kila sababu ya kufanya hivyo. Kwa nia njema kabisa!
 
Haya ndio maajabu ya siasa za Bongo,
Chadema leo hii wamekuwa wa kuleta habari za Cuf na kuwa watetezi wa CUF hasa Maalim na Mtatiro wakati huo huo Ccm wamekuwa watetezi wa Prof. Lipumba.
Mwisho wa siku haki itasimama sehemu yake ni suala la muda tu.
Maajabu mengine ni CCM kuwa watetezi wa Lipumba kwa kutaka kushirikiana na Msajili wa vyama
 
Taarifa kaiandika Mtatiro kawapa wabunge waisome
Mtatiro ni expert kwenye riwaya zisizo na meno kama hizo
Mtatiro amenusa kushindwa,kkatiba ya cuf inataka mtu yoyote anaekalia kiti cha uenyeketi wa muda kuendesha kikao chochote kile,atoke kwenye baraza kuu
Sefu kampa Mtatiro uenyekiti wa muda wa kikao cha kimagumashi kilichomtimua lipumba huku akijua mtatiro si mjumbe wa baraza kuu
Kwa hiyo kikao kile ni batili,maamuzi batili
Kiitishwe kikao kipya na kura za siri zipigwe kama katiba inavyotaka
 
Back
Top Bottom