CUF kuiteketeza CCM Mikoa ya Kusini.

CUF kuiteketeza CCM Mikoa ya Kusini.

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Prof. Lipumba kunguruma Mtwara
NA MARIAM MAREGESI

9th October 2014

headline_bullet.jpg
Aandaliwa mapokezi makubwa

Ibrahim%20Lipumba-October9-2014.jpg

Prof, Ibrahim Lipumba.

Baada ya serikali kutangaza kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi kwa takribani mwaka mmoja, Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Mtwara, kinafanya maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho, Prof, Ibrahim Lipumba, ambaye atafanya mikutano ya hadhara miwili mjini Mtwara.

Kiongozi huyo ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi, anatarajiwa kuwasili Mtwara mjini Oktoba 13, mwaka huu.

Akizungumza na NIPASHE katika ofisi za CUF mjini Mtwara, Katibu wa chama hicho mkoani humo, Said Kulaga, alisema anaandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali polisi cha mapokezi ya kiongozi huyo.

“Mwenyekiti (Lipumba) yupo katika mkoa wetu kwa ziara ya kikazi, tunaishukuru serikali kufungua mikutano, naandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali kwa OCD cha kumpokea Mwenyekiti wetu, naamini tutakubaliwa kwa sababu tamko limetoka ” alisema na kuongeza:

“Tutakuwa na mapokezi makubwa ya pikipiki, magari, bajaji pamoja na magari na yatakayoanzia Ghalani Mikindani saa 2:00 asubuhi na baadaye atazindua ofisi ya chama mkoa.”

Alisema baada ya uzinduzi huo, Prof Lipumba atazindua matawi matatu ya chama hicho kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano wa adhara Ghalani Mikindani.

Kulaga, alisema siku ya pili ya ziara yake, Prof. Lipumba atakuwa na mkutano na viongozi wa CUF wa wilaya, jumuiya za kata na matawi yote ya chama hicho, na kisha atahutubia wananchi wa Mtwara mjini katika uwanja wa Mashujaa.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakali, alisema: “Sina neno juu ya tamko hilo maana tayari serikali imetangaza kuruhusu mikutano na hakuna serikali mbili,” alisema na kuongeza:

“Mimi nitakupa maneno, lakini nimeazima ya Baba wa Taifa, ‘uhuru wa kujitawala bila demokrasia ni udikiteta, lakini uhuru bila nidhamu ni fujo

Alisema kuruhusiwa kwa mikutano hiyo isiwe mwanzo wa fujo, matusi na kejeli na kuonya kuwa endapo mtu atajihusisha na uvunjaji wa amani na kuleta vurugu sheria itachukua mkondo wake.

walibana sana,lkn nilijua iko siku wataachia....
kiko wapi..
lipumba kazi ni kwako hakikisha ccm wanaisha kusini
 
2015 utapata jawabu ,subiri kwanza tuipapatue katiba ya Chama Cha Mabepari.

Mtaipapatua kwa lipi ikiwa chopa 3 ziliwapa kata 3??

kwa watu wapi ambao hatujawahi sikia porojo na ulaghai wao?

mmekwisha kazi nyie...
 
CUF nacho ni chama cha kuongelea hadi jf

jina la zitto kambwe linatosha kupambana na CUF
 
..tatizo la watu wangu wa kusini ni umasikini.
Umesababishwa na Chama kilichopo madarakani ,ubepari wao sasa umetupia jicho kwenye machimbo ya gesi ,mkiendeleza kupokea vikofia vya manjano na shuka za kijani ,watawadidimiza kabisa ,vuzi kuendelea kuikataa CCM'mtafanikiwa.
 
Prof. Lipumba kunguruma Mtwara
NA MARIAM MAREGESI

9th October 2014

headline_bullet.jpg
Aandaliwa mapokezi makubwa

Ibrahim%20Lipumba-October9-2014.jpg

Prof, Ibrahim Lipumba.

Baada ya serikali kutangaza kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi kwa takribani mwaka mmoja, Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Mtwara, kinafanya maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho, Prof, Ibrahim Lipumba, ambaye atafanya mikutano ya hadhara miwili mjini Mtwara.

Kiongozi huyo ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi, anatarajiwa kuwasili Mtwara mjini Oktoba 13, mwaka huu.

Akizungumza na NIPASHE katika ofisi za CUF mjini Mtwara, Katibu wa chama hicho mkoani humo, Said Kulaga, alisema anaandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali polisi cha mapokezi ya kiongozi huyo.

“Mwenyekiti (Lipumba) yupo katika mkoa wetu kwa ziara ya kikazi, tunaishukuru serikali kufungua mikutano, naandaa barua kwa ajili ya kuomba kibali kwa OCD cha kumpokea Mwenyekiti wetu, naamini tutakubaliwa kwa sababu tamko limetoka ” alisema na kuongeza:

“Tutakuwa na mapokezi makubwa ya pikipiki, magari, bajaji pamoja na magari na yatakayoanzia Ghalani Mikindani saa 2:00 asubuhi na baadaye atazindua ofisi ya chama mkoa.”

Alisema baada ya uzinduzi huo, Prof Lipumba atazindua matawi matatu ya chama hicho kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano wa adhara Ghalani Mikindani.

Kulaga, alisema siku ya pili ya ziara yake, Prof. Lipumba atakuwa na mkutano na viongozi wa CUF wa wilaya, jumuiya za kata na matawi yote ya chama hicho, na kisha atahutubia wananchi wa Mtwara mjini katika uwanja wa Mashujaa.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakali, alisema: “Sina neno juu ya tamko hilo maana tayari serikali imetangaza kuruhusu mikutano na hakuna serikali mbili,” alisema na kuongeza:

“Mimi nitakupa maneno, lakini nimeazima ya Baba wa Taifa, ‘uhuru wa kujitawala bila demokrasia ni udikiteta, lakini uhuru bila nidhamu ni fujo

Alisema kuruhusiwa kwa mikutano hiyo isiwe mwanzo wa fujo, matusi na kejeli na kuonya kuwa endapo mtu atajihusisha na uvunjaji wa amani na kuleta vurugu sheria itachukua mkondo wake.

haya bwana.
 
..tatizo la watu wangu wa kusini ni umasikini.
Na huko kwa "matajiri" mbona CCM imesambaa?? Watu wa hili jukwaa ni watu wa hovyo sana... kila siku wao hoja yao ni kwamba kusini na mikoa ya pwani ndio wachawi wa mabadiliko wakati huko bara kuna mikoa majimbo na kata zote zipo CCM na hawasemi! Kuna wapuuzi wanashindwa kabisa kufahamu kwamba wakati Lindi kuna wabunge wawili wa upinzani, Morogoro, Dodoma, Tabora, Ruvuma (naitaja hii coz' wengi wanapotaja kusini wanamaanisha Lindi na Mtwara); kote huko hakuna mbunge hata mmoja kutoka upinzani! Ukienda Iringa na Singida, kuna mbunge mmoja tu kutoka kila mkoa... lakini bado watu nongwa dhidi ya watu wa pwani na kusini haziwaashi... wanaona aibu kusema bayana kwamba hata bibi, babu, mama na baba zao ndio wanaoifanya CCM kuendelea kuwa madarakani!!!

Nitarudi neno hili kila siku! Hata kama kura zote za mikoa ya kusini na pwani zikaenda CCM bado mikoa ya bara peke yake inatosha kuindoa CCM madarakani... kwanza huku pwani population ni ndogo sana as compared to bara... my homeland, mkoa mzima haufiki hata watu milioni moja....

Narudia, wanaoiweka CCM madarakani sio watu wa kusini wala watu wa Pwani bali ni watu wa bara! Watu wa Mwanza na Shinyanga peke yake wanaweza kuwa sawa au wengi zaidi ya watu wote wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga!
 
kusini wana akili sana naona wamewaamsha hata wasukuma siku moja wataona umuhimu wa kudai zahabu ya kanda ya iwanufaishe wana kanda ya ziwa, tatizo la wasukuma kila kitu nduhu tabu hata kama mtu anapingu mkononi wao poa tu wana msemo usemao maguzu masese, eti nguvu zipo tu haziishi hawa jamaa inabidi wabadirike sana, angalia sasa eti wazungu wanasema hawatoi pesa mpaka masuala ya IPTL yawaridhishe kwanza ndio watatoa, hapa unaona jinsi gani serikali ya ccm ilivyo oudated rais kila siku anazunguka kwa wazungu na wanamsifia sasa wanambania, magufuli nae anamuambia rais unatakiwa kutembea zaidi kwa hao wazungu kwani ndio wanaofanikisha mipango mingi ya nchi hii katika ujenzi, sasa je mbona sasa wamezuia fedha za kuchangia bajeti yetu? ccm hamna mawazo mbada mwakani out tumechoka na mipango yanu isiyotekelezeka.
 
Back
Top Bottom