CUF Kuishtaki Serikali ICC?? Patamu hapo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Kuishtaki Serikali ICC?? Patamu hapo!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Dec 30, 2010.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  CUF watishia kwenda ICC Send to a friend Wednesday, 29 December 2010 20:52 0diggsdigg

  Sadick Mtulya na Elias Sichalwe CHAMA cha Wananchi (CUF) kimetishia kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuwashitaki viongozi wa Serikali kutokana na kile kinachodai kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini.

  CUF wanalalamikia polisi kuwakamata wafuasi wake 40 kwa tuhuma za kushiriki maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi kwa lengo la kuwasilisha rasimu sifuri ya Katiba kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.
  Maandamano hayo yalifanyika wakati kukiwa na marufuku ya Jeshi la Polisi inayozuia kutofanyika kwake na polisi hao kuyaita kuwa ni batili kutokana na kufanyika bila kibali chao.

  Jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria wa CUF, Salim Bimani aliliambia Mwananchi kuwa “Kama polisi wataendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu, CUF ipo tayari kulifikisha suala hili ICC kuwashtaki viongozi wa nchi kwa ukiukwaji huo’’.

  Kwa mujibu wa Bimani, polisi hawakuwa na mamlaka ya kuwakamata waandamanaji hao kutokana na ukweli kwamba maandamano ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi.

  Alisema katika maandamano hayo, watu 40 walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa na wengine kuachiwa huru muda mfupi baadaye.
  "Hadi saa 6:00 mchana wanachama 40 waliokamatwa, lakini wamachama 36 waliachiwa baadaye hivyo ninavyozungumza hapa bado kuna watu wanne wako mahabusu,"alisema Bimani.

  Bimani alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kuvidhibiti vyombo vya usalama kwa kuwa vingi, vinafanya kazi kinyume na taratibu na vinakiuka haki za binadamu. Awali akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro alisema rasimu ya katiba iliyowasilishwa jana wizarani ina sura 16 na ibara 131.

  “Rasimu hiyo ya Katiba imeandaliwa na wadau mbalimbali ikiwamo kunakiliwa kutoka kwenye katiba zaidi ya 30 za nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika na Ulaya,’’ alisema Mtatiro. Kwa mujibu wa Mtatiro, Sura ya tano, ibara ya 32 ya rasimu hiyo inahusu uwepo wa Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ambaye atakuwa mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

  Juzi majira ya saa 2:00 asubuhi polisi wenye silaha walifika ofisi za CUF kudhibiti maandamano ambapo waliwatangazia wananchi hali ya hatari na kuwataka wajifungie majumbani mwao huku wakifyatua risasi za moto na kurusha mabomo kuwatawanya.

  Mara baada ya tangazo hilo, wananchi walianza kukusanyika kwa wingi nje ya makao makuu ya chama hicho wakiwa na mabango mikononi na vitambaa vilivyoandikwa ujumbe mbalimbali wa kudai katiba mpya. Baada ya hapo, magari hayo ya polisi yaliyokuwa yamesheheni askari wenye silaha nzito za moto na mabomu ya kutolea machozi, yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika makutano ya barabara ya Uhuru na barabara ndogo inayoingilia Makao Makuu ya CUF eneo la Rozana.

  Baadaye waandamanaji walianza maandamano na walipofika Rozana, magari ya polisi yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika kituo cha mabasi cha Buguruni Malapa, ambako gari maalumu la kumwaga maji ya kuwasha maarufu kama deraya, lilikuwa limeegeshwa.

  Baada ya kuona hivyo waandamanaji walijipa moyo na kuona labda polisi wanawaogopa na hivyo kuingia moja kwa moja katika Barabara Kuu ya Uhuru kuelekea mjini. Lakini, walipofika Malapa, walikumbana na kizuizi cha magari ya polisi zaidi ya sita ya FFU na deraya nyingine. Hapo ilikuwa kama mchezo wa kuigiza baina ya FFU na waandamanaji, baada ya kila upande kumtunishia msuli mwingine. Wakati polisi wakiwataka wanachama hao wasalimu amri na kusitisha maandamano yao, wanachama hao wanajibu "Kuandamana ni haki yetu kikatiba.

  " Wakiwa wanatunishiana misuli katika kituo cha mabasi cha Malapa, gari moja la FFU lilikaa katikati ya barabara na dereva wake alitangaza tena “Tafadhali hili gari usilipite, ukilipita hili gari unatafuta shari.” Lakini pamoja na tangazo hilo, wanachama hao waliendelea kulipita gari hilo na mkuu wa operesheni ya polisi hao akaruhusu gari la maji ya kuwasha kuanza kuwarushia maji.

  Wakati hayo yakiendelea, daladala na magari yote yanayotoka na kwenda Buguruni yalikuwa yamezuia kupita na kupaki pembeni ama kwa amri au kwa hofu yao wenyewe. Baada ya kuona kizuizi hicho waandamanaji hao waliamua kuingia mitaani na kwenda kuibukia katika mitaa ya Amana na Ilala Boma na kuendelea na safari ya kuelekea wizarani. Wakati huo polisi walikuwa wameachwa Malapa.

  Polisi hao walisituka kwamba maandamano yanaendelea wakati waandamanaji hao walipokuwa tayari wamefika eneo la Karume na Mchikichini. Maandamano yalipofika kati ya mitaa ya Ilala Boma na Karume, polisi hao ambao walikuwa tayari wameshajawa na hasira kwa mchezo wa sinema waliokuwa wakichezewa na waandamanaji, waliamua kufyatua risasi za moto kuwatawanya.

  Pia mabomu kadhaa ya kutoa machozi yalilipuliwa katika mitaa hiyo jambo ambalo lilisababisha waandamanaji hao kuanza kupoteza mwelekeo huku baadhi ya viongozi wao, wakifanikiwa kupita kwa gari la chama lenye bendera. Baadaye maandamano hayo yalifanikiwa kufika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria ambako viongozi wa CUF walikabidhi rasimu yao ya katiba. Mwisho


  Source: Mwananchi
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kila Mtanzania mpenda HAKI tuwaunge mkono CUF kwa dhati sana tena sana katika hili.

  Vyama vya ushindani vile vya kweli tu tuungane katika kudai haki ya (i) kujumuika pamoja, (ii) kutoa maoni na kuonyesha hisia, (iii) kuchagua na kutokuchagua bila kuadhibiwa (iv) haki ya wananchi wa kawaida kuunda katiba mpya watakavyo na mambo kama hayo.

  CHADEMA tusibaki nyuma katika kuwaunga mkono CUF juu ya hili jambo.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wabaki nyuma kwani wapo ,maana nasikia wameshagawika makundi ,tunasubiri siku na saa tu lakini Chadema kwa mida hii tulio nayo si shwari tena ,imegawika mapande kama manne.
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Tujulishe nani aliyegawa Chadeama mapande manne?
  Evidence pls.
  Au ndio ushabiki tena?
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA tunapohimiza umoja katika jambo kamwe haina maana ya kwamba kuna watu watakua hawafahamu undani wa CUF. Wakati mwingine busara hututaka kuvumiliana ili tuweze kufika pamoja.

  Hivyo basi, nikikumegea japo ka kipande tu, sitosema yote hapa, ni afadhali ya wao kugawanjika mapande manne ya KUFIKIRIKA kuliko CUF ambayo ukienda Zanzibar ni Serikali na ukirudi bara ni wapinzani. Huyu ni nyoka wa ajabu mwenye vichwa viwili kila upande.

  Tena ni mara mia ya CUF na CCM waliounganishwa pamoja na kamba ya UFISADI na kula kusaza pamoja huku walalahoi tukilia.

  Hoja nyingine upewe majibu sahihi???
   
 6. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF waislamu, humu hatuungi mkono waislamu
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Uislamu na Ukristo baadaye, mimi natetea hoja basi. CUF kwa madai yao kufungua kesi kwa POLICE BRUTALITY is a matter in good direction that need not be trivialised the way Mwiba may have loved to look at the whole issue here.

  Mimi nawaunga mkono katika jema na kuwaponda vile vile kama hali halisi inatusukuma huko. Na kwa mstari huo hata CHADEMA haiwezi ikapona.
   
Loading...