CUF,CHADEMA wapinga majimbo kupunguzwa Zanzibar

CUF,CHADEMA wapinga majimbo kupunguzwa Zanzibar

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,434
Reaction score
6,356
Omar%20Ali%20Shehe,-SEPTE,MBER11--2014.jpg

Omar Ali Shehe

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakiko tayari kuona majimbo ya uchaguzi yanapunguzwa Zanzibar kwa kisingizio cha idadi ndogo ya watu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alisema siyo kweli kuwa baadhi ya majimbo yakiwamo Magogoni na Chambani Kisiwani Pemba kuwa na idadi ndogo ya watu kwani suala hilo linahitaji utafiti zaidi.

“Idadi ndogo ya wananchi isiwe kigezo cha Tume ya Uchaguzi kupunguza majimbo, mbona Tanzania bara kuna Jimbo la Mafia ambalo lina wakaazi 13,000 na linafahamika kama jimbo?” alihoji Omar.

Alisema ni vyema tume hiyo kufuata katiba na sheria, hivyo ipo haja ya kuongeza majimbo na siyo kupunguza majimbo.

Alisema kuwa endapo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itapunguza majimbo haitokuwa na uadilifu na upo uwezekano mkubwa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kutokuwa huru na wa haki.

“CUF inahisi tume haina nia njema katika zoezi hilo, kama tume hiyo itaamua kupunguza majimbo hasa ya Pemba,” alisema.

Afisa Habari na Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Dadi Kombo Maalim, alisema Chadema hakijashawishika na upunguzaji au uongezaji wa majimbo kwani wanahisi majimbo 50 yaliopo yanatosheleza.

Alisema bado wana mashaka na ZEC katika utaratibu wa ugawaji wa majimbo, hivyo ipo haja kwa tume hiyo kuepukana na mizozo isiyokuwa ya lazima.

“Fedha zinazotumika katika ukusanyaji wa maoni kuhusu mgawanyo wa majimbo ni fedha za wananchi, hivyo fedha hizo zisifanyiwe ubadhirifu,” alisema Dadi.

Licha ya mtazamo huo wa vyama vya siasa, ZEC ilisema bado haijaamua kupunguza au kuongeza majimbo na sasa ipo katika utaratibu wa kukusanya na kuchambua maoni yaliowasilishwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salum Jecha, alisema tume yake itafikia maamuzi kutokana na mapendekezo ya wadau na kuwataka wananchi wasubiri maamuzi ya tume.


Chanzo: Nipashe
 
....njama ya ccm hiyo,lengo ni kupata theluthi 2 ktk baraza la wawakilishi na kuongeza idadi ya vilaza ktk bunde la muungano
 
Ata wakichanganya majimbo uko wanakoyahamishia story ni ile ile tu ccm haikubaliki tena.
 
hapa ndo ninapowapendea ccm. kule wilaya ya hai walipoona hawana chao kwa mbowe wakaamua kugawa wilaya/majimbo ili yawe mawili na sasa wilaya ya siha ipo chini ya ccm. na huko pemba walipoona uwezekano wa ccm kujiongezea majimbo haupo wakaamua kuyagawa kwa kuangalia ni sehemu gani wanakubalika zaidi, lakini wapemba ni watata. hata kule ambako walihisi watapata kura wakatoswa. sasa wanakuja na singo ya kuyaunganisha. hii kama sio laana ni nini kwa haya manyang'au? EWE MWENYEZI MUNGU TUJAALIE TUYAONE MAMBO KATIKA UHALISIA WAKE.
 
Back
Top Bottom