Na Otilia Paulinus
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepunguza gharama za vipimo vya matibabu kwa wagonjwa wa rufaa.
Vipimo vilivyopunguzwa gharama hospitalini hapo ni vipimo vya aina mbili; ambavyo ni MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, vipimo vilivyopunguzwa gharama ni kiitwacho MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.
Lengo la kupunguza gharama hizo, Aligaesha alisema ni kuwafanya wagonjwa waweze kumudu gharama za vipimo hivyo na kuanza matibabu mapema.
Awali kipimo cha MRI kilikuwa kinagharimu Sh 350, 000, lakini sasa kimeshuka hadi 100,000 na kile cha CT Scan kilikuwa kinagharimu Sh 170,000 na sasa kitakuwa kikigharimu Sh 50,000 kwa wagonjwa watakaokuwa wamepata rufaa ya kutibiwa hapa Muhimbili wakitokea Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Kimsingi punguzo hili limeanza tangu mwezi uliopita na hili limekuja baada ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutaka kuifanya Muhimbili kuwa Hospitali Maalum ya kutoa vipimo vikubwa ambavyo hapo awali havikuwapo.
. .
cr@p!!!CCM OYEEEE....!
Natoa pongezi zangu za dhati kwa serikali ya CCM chini ya makamanda KIKWETE,MUKAMA,NAPE et al kwa kuwezesha yote hayo
this is a good news kwetu... what we need to struggle now ni kuboresha customer service and equipment maintenance and repair... BTW, huu ni ule msaada wa ABBOTT au ni pesa za wananchi ndizo zilinunua mashine?CT scan inagharimu sh 300,000/- katika hospitali za Private kama Regency, Aghakan. na kwa sasa Muhimbili ni sh 50,000/-
MRI inapatikana Muhimbili na Aga Khan tu kwa Tanzania.
Aga Khan sh. 500,000/- Muhimbili Sh. 100,000/-
Punguzo sawa, je huduma itapatikana? Au ndo yaleyale ukifika unaambiwa machine ina matatizo inabidi usubiri wiki mbili au nenda Regency! Na tatizo la mgonjwa ambaye nature ya tatizo lake tu haihitaji CT wala MRI, na akiambiwa anaona kakataliwa.Muhimbili yapunguza gharama za vipimo
Hili punguzo limeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Muhimbili na MOI
umeanza kuniudhi kwa kuleta siasa hapa... hii effort imekuja baada ya kuona mamashine yanakua white elephant mkuuSERIKALI YA CCM ISIPOSEMA......wapo watakaodaka hoja na kusema uwongo....NA UWONGO UKISEMWA MARA NYINGI HUGEUKA UKWELI
Foleni haikwepeki mkubwa, mashine ni moja ya serikali, ipo muhimbili, Dsm population about 5million, Tanzania population about 40million.Punguzo sawa, je huduma itapatikana? Au ndo yaleyale ukifika unaambiwa machine ina matatizo inabidi usubiri wiki mbili au nenda Regency! Na tatizo la mgonjwa ambaye nature ya tatizo lake tu haihitaji CT wala MRI, na akiambiwa anaona kakataliwa.
Tusubiri kuona foleni itakavyokuwa ndefu!
Kwa pressha ya wagonjwa Mashine tangu iwe installed inapiga kazi 24/7! No breather!duh bonge la nafuu ila kwa wengine ni mzigo bado inatakiwa ifanyike buree kwa wasio na uwezo!Kingine nacho hofia hapo isije kufanyika hujuma ya kuharibu hizo mashine ili kule private wapate nao kazi duh wewe unatoa huduma laki 5!sio mchezo
With the current punguzo all NHIF clients irrespective of their insuarance category (green/brown/etc) have CT and MRI services at their disposalbima ya NHIF au za maofisini hazilipi hivi vipimo na wazazi na wazazi wa wazazi wetu wanatumia hivi vipimo and they can not affort
jee ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kutoa sh 100 000?
Wewe na mimi tunaweza kulipa 100,000 for MRI lakini hatuna uwezo wa kulipa 350,000/- ya awali.
Kwa watakaoshindwa kulipa hata hicho kiwango kuna idara maalum ya msamaha inayoshughulikia matibabu yao ikijumuisha vipimo, dawa, consultations hata chakula na ikibidi nauli na escort ya kurudi Urambo nyumbani alikotoka.