Crossroads: Ex wa mke wangu wanaendelea kuwa karibu na wife hadi sasa

Willy Wills

Member
Dec 8, 2018
22
174
Hello guys!

Kama unasoma ujumbe huu naomba nikushukuru kwa kupoteza muda wa kusoma nyuzi zingine na kujua ni kipi hasa ninahitaji unishauri. Nitaanzia mbali kidogo ili upate mtiririko mzuri wa matukio na nitajaribu kuweka kila detail ya msingi ili ukiweza kunishauri, unishauri vyema. Yawezekana niko desperate kiasi cha kuonekana kuwa nauliza ushauri kwa ajabu ambalo ni la kawaida katika jamii.

Mimi ni mwanaume wa miaka 31 ni mzaliwa na mkazi wa mkoa wa DSM. Nimeoa na mke wangu ana mtoto mmoja. Ni mtumishi wa umma katika 'ofisi kuu' ya Nchi yetu.

Ilipoanzia...

Miaka mi4 iliyopita nilifahamiana na binti mmoja(wife) yeye akiwa ni mtumishi katika ofisi moja ya 'uchunguzi' HQ. Frankly nilimoenda sana at glance na hadi leo nikiri ninampenda sana, sina hakika kama niko tayari kumpoteza. Nikaanza kumfuatilia na kugundua yuko kwenye relation na jamaa mmoja ambaye ni mwanafunzi wa law SAUT mwanza, na binti alikua deadly in love with the guy ambaye wamekaa for almost 3 years back then since wakiwa High school.

Jamaa anatoka mkoa mmoja na binti(lake zone). Hivyo nikaona ugumu ulipo kumpata. Nikaendelea na hustle za kumfuatilia ili nijue vita ikoje, nikichukua advantage kuwa binti niko naye Dar na jamaa yuko huko mwanza. Nikaja gundua pia jamaa angalau twice per month huwa anakuja Dar kwa binti na alikua akifikia nyumbani kwa binti ambapo wanaishi na sista yake.

Pia nikaja gundua financially jamaa hakua vibaya sana (though hakunizidi) kwani mzee wake alikua ni 'kigogo' wa council moja huko kusini, na alikua akisimamia projects kadhaa za ujenzi za mzee wake hapo Mwanza, pia alikua na mkopo chuoni. sources ziliniambia jamaa alikua akimpiga tafu binti kwa issues nyingi kama house rent kidogo, issues mbili tatu za kimaisha.
Nikagundua pia binti alikua akimumini sana jamaa, ingawa jamaa alikua ni player wa siri sana na mtu wa pombe sana, nilihisi kushindwa pambano.

2015 March nipata info kuwa jamaa ameenda weekend kuspend Uganda na ameondoka na rafiki yake na madem wawili bila kumuambia binti.

Nikafanya makeke taarifa zikamfikia binti. Hapa binti akaanza kuloose trust na jamaa. To me ilikua ni point tatu. Aliporudi Uganda jamaa akaja Dar, kisha binti akagundua messages za mapenzi na dem mmoja wa jamaa. Sikujua what happened next.

Few days later nikapata taarifa binti yuko frastruated na anaumwa baada ya kugundua nasty things za jamaa yake. I took advantage na nikawa close na binti nikamcare sana. Siku moja tuko naye jamaa kapiga dem akamjibu dry kuwa yuko namimi hawezi ongea na simu. I told myself that im about to win, nikawa close na binti finally nikamtia mimba na punde nikatangaza ndoa, binti aka convert kufuata dini yangu and we married. from then hakua binti tena bali wife and she gave me baby girl.

Thanks God shem zangu hawakua na shida na Mimi wala mama mkwe wangu 2015-2017 things were cool na nilijiridhisha kuwa binti hakua na mawasiliano na binti.

Bahati mbaya tuliingia kwenye quarrels kadhaa baada ya kunigundua red handed mara kadhaa kuwa nina mcheat. We peacefully solved shida zetu.

But I started kunote tofauti fulani fulani. Wife hakutaka tena nishike simu yake on ground kuwa mimi sitaki ashike yangu. Mwaka huu mwanzoni nikakuta namba fulani imempigia, nikampigia na nikapokelewa na mwanaume, nikamwambia mpigie fulani (wife) alikua anakutafuta, jamaa akanijibu yeye anayo namba yangu kwanini asinipigie mwenyewe. Nikakata simu.

Baada ya wiki kadhaa, nikaona namba ya jamaa imeweka d.p picha ya wife kilichonistua ni kuwa that pic sikuwahi iona..it was like my wife selfied herself and sent a pic straight to the guy. Nikachat na jamaa na kumtumia picha za wife zingine na kumuambia... weka na hizo profile., but hakunijibu chochote cha kumfanya nione kuwa wako naye kimahusiano. Jamaa alikua smart sana kwenye majibu yake akiavoid kuwa caught, nikampigia simu wife kumlalamikia kuwa kwanini mtu anaweka picha zako dp. Wife akaniambia mimi ndio nina makosa zaidi na kama ningekua namuheshimu nisingemtumia picha zake zingine.

Nikawa mpole, I deleted those pic i sent to the guy.

Some few minutes dp ya jamaa ikabadilishwa na kuwekwa pic ya dem mwingine. Namba nikainote kuicheck mpesa ina jina la kike. Nikachukua jukumu la kutrace msgs za jamaa using my position, sikuona kitu cha maana chochote zaidi ya salam. Na kuna mgs za kushukuru wife ametumiwa pesa na jamaa. Nothing shocking I noticed. Baada ya kama mwezj ile namba haikuwa hewani tena.

Shida kubwa ikaja hapa miezi kama miwili imepita.....

As u all know public offices zinahamia dom, na mimi niko huku almost 4 months now. Nilichokuja gundua wife ananicheat. Na ananicheat kwa mtu mmoja tu, naye ni yule yule jamaa yake aliyemuacha na mimi kumuoa.

kama wiki 3 zilizopita, jamaa yangu alinitaarifu kuwa shem nimemuona lodge fulani magomeni kwa nje its like anampigia simu mtu, bahati mbaya hakujua kinachoendela sababu alikua kwenye shughuli za kiofisi. Kumpigia simu wife kumuuliza alipo, akajibu yuko ofisini. Nikamuuliza informer wangu pale ofisini kwake, akanijibu yeye hayupo ingawa gari yake ipo. i took it easy. Siku 4 baadae nikarudi Dar, sikunotice shida yoyote kwa wife. nikaka kama wiki 1 pale dar nikifanya upelelezi wangu pale lodge aliyofikia.

Nikipata msaada wa binti mmoja nikaonyeshwa Cctv footage ya ile hotel. Niliumia sana niliyoyaona. wife amefika pale mara tatu. Ya kwanza ndio ile aliyoonwa na jamaa yangu, second one ilikua saa 11 asubuhi na kutoka saa 3. Nikajiuliza ina maana siku hiyo hakwenda kazini. nikafuatilia na kugundua siku hiyo alitoka nyumbani saa 11 na kisha kureport kazini saa 3.

What hurted me the most ni mara ya tatu. Hii ilitokea a day before, nami nikiwepo. Siku hii nakumbuka nilimuaga wife naenda town kurekebisha gari by saa 10 jioni nitakua nimerudi, mida hiyo ni saa 6. Nikiwa garage wife alinipigia sim kuwa atatoka for almost 2 hours ana issue kazini, nikamuambia poa.

Footage ilinionyesha kuwa aliingia pale saa 7 na ilimuonyesha akitoka saa 9 na robo. alitoka akiwa anasindikizwa na jamaa kavaa vest na boxer tu kutoka floor ya 3 hadi ground floor na jamaa akarudi. Siku hii kilichonishangaza wife alitumia uber. Bila shaka nikathibitisha wife ananicheat, na ananicheat kwa mtu ambaye yule yule niliyemdhania miaka mingi.

But nature i dont take quick judgement. Nilijipa muda wa kutafakari na kujua how deep wako na huyo jamaa this time around.

Nikafanikisha kupata namba ya jamaa. kwanza imesajiliwa kwa jina la kike.

Nikagundua wana chat zaidi whatsapp hii sikuweza kung'amua kipi ni kipi. Ikabidi nicheck text messages. niliyoyakuta, hurted me the most.

1. wife na jamaa walikua wakikumbushiana ni jinsi gani walivyokua wana enjoy sex. Kila mmoja akimsifia mwenzake kuwa yuko vizuri. Lakini wife ndiye aliyekua akimsifia zaidi jamaa kuwa ni mwanume pekee anayemjua vyema na kipi cha kufanya kuwa the guy knows how to satisfy a woman. This pained me much

2. Walikuwa wanazungumzia sexual fantasies zao. kila mmoja akimwambia kipi wanatamani wafanyiane. hapa paliniumiza sana, kwani wife alimuambia jamaa wakikutana atampa vyote anavyotamani na ambavyo hawakuvifanya. Wife pia amemuambia jamaa they have to arrange for threesome na jamaa amekua tasked atafute dem ambaye anamuona anafaa and they guy promised to work on it.

3. Wife na jamaa wanasaidiana mambo mengi hasa financially, mfano jamaa alimuongezea wife 1 M ya kununua kiwanja huko kwao, pia jamaa alimnunulia sim wife, ambayo nilijua kwa kazi yake wife simu kununua sio issue kubwa. na vitu vidogo vidogo vingi jamaa anafinance wife. Pia maza wake na wife jamaa ana msupport sana as wanaishi the same town. wife anakiri kwa jamaa kuwa yeye ndiye mwanaume pekee ambaye yuko free sana kumuambia chochote na akamsikiliza.

4. Hakuna point hata moja niliyonote kuwa walishawahi kunizunguzmia, hilj linanipa shida sana. je wife hajamwambia jamaa kuwa hajaolewa? au jamaa

Guys, nimenote mengine sana, ingawa naamini kuwa mengi zaidi yapo kwenye whatsapp. nikiwa na wife, i never doubted wala openly noticing kuwa ananicheat, sim yake yuko free nayo muda mwingi na usiku hata nikiwa naye haipigiwi. Mimi ni as a man i know how hard it is to cheat na kuficha, hivyo I trusted wife 100%.

I deeply seek a wise advice from you guys on basisi kuwa siko tayari kumuacha wife, najua kiasi gani ninavyompenda, I believe she loves me, na she respects me sana, anaihandle family yangu vizuri na mtoto also family businesses.

Ninachoomba kujua ni kuwa nitafanya vipi ili aachane na jamaa, huu ndio mtihani mkubwa kwani it seems wife ni sex addicts kwa jamaa, mwezi huu ana likizo ya kwenda kwao, na jajamaa yuko the same town wife ndiyo kwao, je nimzuie asiende? Niko njia panda.

Sijamuambia wife chochote na hajanotice chochote kuwa najua nini kinaendelea. Thanks guys kwa time yenu, nitashukuru kupata ushauri wenu. Na ninaahidi kuufanyia kazi.

NOTE: KULINDA HESHIMA YANGU, KAZI YANGU I HAD TO COME WITH THIS ID
 
Wewe ulianza mwenzio kamalizia

Alichobugi n mwanamke hashindani na mwanaume,

Huna cha kufanya hapo yataka mke akubali mwenyewe waachane na s kushurutishwa zaidi

Alikukubali sababu alikua desperate na stress za kua single zikimtafuna

Maybe ushirikishe wazazi sasa au muitane wenyewe muambiane mwisho wa siku mshindane kuleteana maradhi tofauti tofauti

Akikataa kwa amani achana naye hapo mlipofika ni pabaya na kukubali threesome smh!!
 
Duh! Hiyo ngoma nzito!

Nilicho-notice wife unam-feel kichizi hutaki kumpoteza, something very difficult to be guaranteed.

Ushauri wangu:

1. Tafuta weekend moja toka na wife zungumzieni mustakabali wa mapenzi/ndoa yenu, kila mmoja awe huru kwa mwingine, kiri kufahamu kinachoendelea katikati yao (sijui itakua na madhara kiasi gani kumwambie namna umepata hizo taarifa).

Kila mmoja akiri makosa yake kea mwenzie, akiwa tayari kuendelea muendelea na muanze upya, no cheating.

2. Andaa moyo wako in case hayuko tayari muendelea, let it go.

I humbly submit!
 
Hakuna kitu kinachoma kama ukute sms ya wife anamsifia Jamaa kama anamgegeda vizuri na kwamba hajawahi toshelezwa kiasi hicho na Mwanaume yoyote!

Usipotuliza Akili unaweza jikuta unatafuta vumbi la Congo hivi hivi

Yaani unapoteza confidence kwenye sex kabisa

Pole sana kaka
 
Nimeshavuta embassy now i can say something!

Ni vyema tuanzie kwenye msingi wa tatizo lenyewe.

Ni dhahiri kuwa huyo mkeo alikua anampenda sana huyo ex wake, na wewe ulimuoa kipindi akiwa desperate naye akakubali. So alifanya maamuzi bila kuwa huru. Jambo la Pili ni kuwa wife baada ya kuwa na amani na mfumo mwingine wa maisha yawezekana kuwa akagundua wewe humfikishi kimapenzi, na ikachagizwa zaidi na wewe kuwa na michepuko hivyo ndipo nae akaamua kutafuta alipopaacha kama kumwaga mboga. (kwa ujuzi wangu mdogo wa saikolojia na naona iko hivyo).

Ushauri: Jaribu sana kwanza wewe uache michepuko yako na jaribu kuonyesha kuwa uko faithful ili upate moral authority ya kuanza kumbana.

Pili jitahidi utengeze ukaribu naye sana, sababu inaelekea wife wako wamekaa muda mrefu tangu utoto na jamaa hivyo wamezoeana sana. Ukiwa na ukaribu naye atatengeneza mazingira ya kuwa huru sana kwako. kama ulivyosema jamaa anamuhudumia vitu vidogo vidogo na yuko huru zaidi kwa jamaa kuliko wewe.

Mwisho tengeneza mkakati maalum wa kudeal na jamaa. mface umchane wazi kuwa aachane na mkeo.
 
Willy Wills,
Mkuu kwanza pole. Ushauri wangu ni mfupi sana lakini umejaa uhalisia 100%. Wife wako anampenda huyo jamaa na hilo huwezi kulibadilisha hata kama utampa ulimwengu huu tunaoishi na vyote vilivyomo. Moyo wa mtu ukipenda hakuna utakachoweza kukifanya ukaubadilisha huo upendo. So cha kufanya ongea tu na wife ili ajue kuwa unajua kinachoendelea.

Akishajua kuwa unaujua mchezo mzima ataogopa. Nasema ataogopa tu, kwa hiyo anaweza kumuacha huyo jamaa on the grounds za kuogopa tu na si kwamba upendo kwa huyo jamaa utakwisha. Conclusion, hiyo njia ya kumuogopesha ikishindikana basi hakuna cha zaidi utakachokifanya ili kuwatenganisha "wawili wapendanao". Ukimpenda mtu na yeye akawa anakupenda kuachana haiwezekani. Kifo tu ndio kitakachowaachanisha.
 
Inshu yako itakuwa rahisi kuisolve endapo kama shemeji atakubari kubadilika, mwambie kistarabu kuwa usaliti wake umeshaufahamu, namkumbushe athari zausaliti nakama wewe ndio ulianza kumcheat nimuda sasa muhafaka wawewe kumuomba msamaha nakama atakuwa muelewa basi mfungue ukurasa mpya maana naamini huyo jamaa hana cha kupoteza kwa huyo mke wako ila wewe unacho chakupoteza kwanza nindoa yako ya imani yako na vilevile status yako katika Jamii na mwisho kabisa ni mustakabali wa chalii yenu.
 
Pole sana Mkuu

Hapo nadhani tunza hizo evidence vizuri kisha umuite wife mzungumze taratibu nini tatizo!

Na je yupo tayari kuendelea au vipi?( hapa jipange maana jibu lolote unaweza lipata inaonekana Jamaa yake yupo vizuri na ameridhika kweli kweli)

Ingawa nawewe Mkuu jiulize nini hasa tatizo mpaka wife amebadilika kiasi hicho wakati zamani alikupenda!( tatua chanzo usitatue matokeo)

Kila la kheri Mkuu Ulimwaga ugali wife amemwaga mboga akazima Na moto kabisa
 
Kiukweli ndoa yenu ni changa na imekutana na kesi kubwa sana.

Utakuja kugundua baadae sana kwamba it is not reconcilable, utakuwa ushapoteza focus sana.

1. Wife anampenda jamaa
2. Mama mzazi wa wife anamkubali jamaa
3. Jamaa atakuwa ni rafiki mzuri sana kwa wife wako

So, hiyo ndoa itakutesa sana, anza kujiandaa kukaa pembeni, 31 ni mapema sana kuharibu maisha yako kwa stress za ndoa.
 
pole sana ndio changamoto zenyewe hapo cha msingi n kumwambia ukwel as long unazo evdenc na yeye atatoa msimamo wake.....na ww kuwa mtu wa msimamo.... mapenz n ufala sana let her go
Honestly ni ufala sana. Wife aliteswa sana baada ya kugundua jamaa anamcheat na kumdump, the moment naanza naye relation alikua ameugua sana baada ya maumivu ya kulia sana takribani wiki nzima alilazwa. I saved her from that situation. I used a lot of money kumrudisha katika hali ya kawaida. Leo the guy aliyemtesa ndio ananicheat naye. I never cried lakini wa mara ya kwanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom