Critical analysis: Taarifa ya polisi kuhusu jinsi alivyouawa muuza magazeti Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Critical analysis: Taarifa ya polisi kuhusu jinsi alivyouawa muuza magazeti Morogoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Aug 31, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  mchezo ulianza kwa vyombo vya habari kuripoti.Kisha akaja waziri wa mambo ya ndani.Kisha akaja kingozi wa vijana wa ccm.Taarifa zilikuwa risasi ndizo zilitumika, hadi kwa majeruhi.na waandishi waliokuwepo walindika na kuhoji watu waliokuwepo pale.

  Hadi hapo watuhumiwa walikuwa ni hawa na suala halikuwa ni silaha gani imetumika:=
  1.CCM
  2Polisi.
  3.CDM.

  Kisha polisi wanakuja na tangazo lao.Kuwa kifo kilisababishwa na kitu chenye ncha kali.Kama attempt ya kubadili mitazamo na guessworks za raia,

  1.CCM.
  2.CDM.

  Wakati polisi wanajaribu ondoa uwepo wa risasi,ili baadaye wajiondoe katika mauaji na baadaya kuwabana CDM, swali linakuja.Je wataweza jitoa salama?Na nani anafanikiwa jiweka in perfect place.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mr. Critical analyser, kuondolewa risasi kunaiondoa vipi polisi kwenye list ya watuhumiwa?

  CCM imeingia vipi kwenye list ya watuhumiwa?
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kwa vile silaha nyingie kama mikuki,mundu,visu watasema hawatumii katika riots.CCM walitangaza mtuhumiwa kabla ya polisi.

  Unakaribishwa weka mtazamo wako
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Jamani hili ni swala la common sense, Raia hawez kuuawa bila watu wengine kumuona huyo mtu.

  Common sense:
  kwa mujibu ya watu walikuwepo eneo marehemu alikuwa akisoma magazeti ubaoni kwahyo muuza magazeti ndiye angekuwa mtu wa kwanza kumuona muuaji kama angekuwa raia wa kawaida ni chombo cha mbali tu ndio kinaweza kuua bila wausika kumuona muuaji.

  Ulinzi wa polisi.

  Pamoja na polisi kuwepo eneo hilo ni raia ndio waliojotolea kumpeleka marehemu hospitalini, jiulize kwanini wananchi
  walikuwepo hawakutaka kuwaita polisi kuwasaidia huku wakijua kuwa wao ndio wanausika na usalama wa raia?? sababu pekee ni kwamba wananchi walichajua kuwa polisi ndio wauaji na ndio sababu ya raia kutowashirikisha polisi hao na badala yake wakaamua kumpeleka marehemu hospitali bila kuwashirikisha polisi.

  CCM inausikaje??
  Wiki mbili zilizopita gazeti la mwananchi na nipashe lilimripoti Nape akitabiri kuwa chadema itafanya fujo morogoro
  jiulize Nape alipata wapi taarifa kuwa CHADEMA itafanya fujo ili hali mikutano ya CHADEMA ilikuwa inaendelea na hakuna mtu wala nyenyere aliyekufa kwa ajili ya kuwepo kwa mkutano wa CHADEMA?? zingatia jinsi jeshi la polisi linavyotumiwa
  na CCM.

  Kwanini wanaondoa risasi??
  Kwa sababu ukishaondoa risasi unakaribisha mazingira ya kuwa marehemu anaweza kuwa ameuawa na mtu yeyote yule nia ni kuwachanganya wananchi. Ukibakiza risasi pekee maana yake umeshawamata polisi na kosa la mauaji kwa sababu ni wao pekee ndio waliobeba risasi siku hiyo.

  Muuaji anafahamika ni CCM kwa sababu polisi wanafanya haya wanayoyafanya kutokana na shinikizo kubwa wanalopata kutoka kwa viongozi wa CCM kumbuka wanye hofu kubwa ya kupoteza power ni CCM na si polisi kwahiyo hii ni kama kesi ya mtu aliyekodi mtu kuua kwa niaba yake naye pia anahusika asilimia 100% kwani bila ushawishi wake mauaji hayo yasingetokea.
   
 5. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  hivi risasi haina ncha kali?....kama risai ilimparaza marehemu basi ina chana nyama ....ikiingia mwilini inakotoka inafumua!!!!! NCha kali could be anything from a bullet to a knife....Wametumia neno hili ili kupunguza jaziba za wananchi, wanaharakati nk...kwani mtu akisema umekaa vibaya ndo kusema huku kaa uchi????
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Basically Hata issue ya Ncha Kali si ya kupuuzia kwani kuna Vijana wengi wa Magamba wanasafirishwa kutoka Dar Kwenda kwenye Hiyo Mikutano na sijui mission yao!! Ila wakikamatwa wanadai ni wanunuzi wa Mazao Vijijini!!!
   
 7. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ile ilikua Risasi halisi na ndio maana kuna majeruhi wa risasi, sasa inakuaje hakuuawa kwa Risasi? CCM ikishirikiana na Polisi wameenda kuongea na hatimae kuchakachua riport ya madaktari wa Morogoro. Ili kujitoa na ndio maana waliwasiliana na ndugu wa marehemu ili kuusafirisha mwili.

  "Siku zote muovu wa karibu yako pindi akikufanyia uovu hua karibu zaidi ili kujua kila hatua uipitiayo katika kipindi kigumu alichosababisha"
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ili kuchambua kiyakinifu tukio hili, ni muhimu pia kuangalia majeruhi hasa wale wawili waliojeruhiwa vibaya na risasi. Ikumbukwe kwamba mmoja wa majeruhi aliyepigwa risasi mguuni alikuwa ni mpita njia na baiskeli yake, hivyo alikuwa mbali na hekaheka hizo.

  Kama risasi ingempata kichwani basi angeweza kufariki na tukapewa hadithi kama hii ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali. Pia kutabiriwa kwa fujo hizi na Ndugu Nape hakuwezi kumuondoa kwenye hii hatia.

  Tunashangaa kwanini hadi sasa polisi haijamuhoji ingali alikwisha sema na maafa yametokea licha ya wengine kujeruhiwa. Je, ni nani hasa aliyesababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani?

  Ni lazima umma tueleweshwe ni vipi siasa zinatumiwa kutuhatarishia maisha yetu tena hata wale tusio washabiki wa chama chochote.
   
 9. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Nimeupenda sana mchanganuo wa Politiki #4. Nina hakika FBI wangeweza kusaidiana naye kama wangepewa kazi ya kupeleleza kesi ya Ulimboka!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mwache nape mkuu mimi namsamehe kama mwenyekiti wake dhaifu!
   
 11. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Yaani watu wa falsafa pale UDSM wakiona hii mada watamshangaa sana mtoa mada.

  Kama mtu alikua anafuatilia kwa makini swala la kuuwawa kwa binadamu mwenzetu kule morogoro hawezi kumwelewa mtoa mada na politiki. Nimshukuru ze marcopolo kwa kuuliza swali la msingi.

  Risasi ni risasi hata palipopigwa risasi pa kioshwa namna gani pado itajulikana tu kuwa ni risasi. Kumbuka risasi ina kemikali isyopotea maana huingia kwenye damu ambapo ukipima damu tu au chembe za kwenye moyo utagundua ni risasi ama la. Pili CCM hawakutaja aliyemuuwa ni CHADEMA bali CHADEMA kutotii sheria ndiyo chanzo cha yote. Eti aliyoko karibu ndiye anayeweza kutambua aliyempiga??? Tambua wakati wa sokomoko hilo kila mtu alikua anakimbia kivyake wengine wanarusha mawe, wengine chupa na wengine nondo au aina nyingine za silaha za ujima ambavyo ndivyo vilimkumba mwenzetu. Niliuliza swali la msingi siku chache zilizopita lakini nikapingwa vikali na matusi juu.

  Tuache ushabiki wa vyama, tuache kutafuta umaarufu kupitia damu za wenzetu, tuache kuvunja sheria kwa madai ya kutaka kuonesha tunahonewa.
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha kesi ya Singida.........kwamba wale vijana waliokamatwa wote walikuwa wafanyabiashara wa Dar na wote walikuwa wanachama wa CCM............what a coincidence...!!
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hii unayozungumzia hapa kwenye Red ni yale yaliyotokea Morogoro au unaota?
  Hapo kwenye Bold, upo tayari kutoa ushahidi? au pia unaota kama mwanzo.
   
 14. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Yale yale ya magamba akili ndogo kutaka kutawala akili kubwa,kwa pumba kama hizi mzee hata ukitukanwa ni poa tu tena ungestahili hata kupigwa mawe haiwezekani mkawa mnatetea huu uuaji wa poloccmagamba halafu wakuache....tafakari ww gamba polis wanatumka.
   
 15. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  MKUU HATA HII NI NCHA KALI.....
  [​IMG]
  Polisi hawawezi kulikwepa hili.....wao waseme yote lakini ukweli nikua Polisi wamehusika na unyama huu
   
 16. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu tambua kuwa uoga wako ndio umaskini wako...na waswahili walishasema kuwa "mjusi ukimfukuza sana hugeuka kuwa nyoka kinachotokea sasa ni matokeo ya ukandamzwaji wa haki yanayofanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM imefika mahali wananchi nao wametambua haki zao ndipo linapokuja suala la liwalo naliwe.
  Unaposema CHADEMA kutotii sheria ndiyo chanzo cha yote unasahau kuwa polisi kukandamiza sheria ndo wanaweza kuwa chanzo cha yote hayo.
  TAFAKARI
   
 17. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Je unaweza kuitenganisha ccm na serikali yake? Je unaweza kuitenganisha serikali na Polisi?
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapana,serikali na polisi havitengani,,,,maana polisi ni chombo cha serikali,na ipo kuilinda serikali
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna swali najiuliza,sijawah kupata MAJIBU,,,,mauaji haya yanayofanywa na polisi wakat yakifanyika VIONGOZ WAANDAMIZ WA CHADEMA HUWA HAWAPO AU????ARUSHA WAMEULIWA WATU WA 5,MORO MMOJA,SINGIDA MMOJA,,,,
  SASA KWA KESI YA ARUSHA NA MORO ZAFANANA,JE POLISI HUWA HAWAWAIN HAWA VIONGOZ,,,,(SIMAANISH NAO WAUAWE)
  NAOMBA JIBU
   
 20. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,886
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 180
  Hivi siku hizi Nape amekuwa mtabiri wa alama za nyakati..ama mie nimelala bado?!
   
Loading...