Cristiano Ronaldo ni somo kwa vijana

manchoso

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
1,606
2,055
Nilikuwa namuangalia Cristiano Ronaldo katika mechi ya kufuzu Russia2018 kati ya Ureno na Uswiswi na ukweli ni kuwa anaelekea katika kumalizia maisha yake ya soka,huyu wa leo sio yule niliemzoea aliekua na kasi isiyomithilika, anaoneka kuchoka na kasi kupungua labda huu msimu/msimu ujao unaweza ukawa msimu wa mwisho wa kumuona akiwa juu katika ubora wake.
lakini nachotaka kusema kueleza hapa vijana tuna mengi ya kujifunza kutoka katika maisha ya Cristiano Ronaldo.

SOKA
Sahau kuhusu Messi,Zidane,R.de lima,Baggio,Gaucho,Rivaldo, Pele wala Maradona.Cristiano ndie mchezaji bora zaidi ambae nimebahatika kumuona sababu hao niowataja juu naamini walizaliwa na vipaji vyao ila ronaldo ni (self made) amejitengeneza mwenyewe kutokana na juhudi kujituma na kujiamini

Raul Gonzalez alipata kusema ipo siku alimuona Messi akikimbia na mpira na ule mpira ukaonekana kama vile umegandishwa na gundi mguuni kwake,ni kweli sababu Messi amezaliwa na kipaji ni raha kumuangalia ila Cristiano ni mtu wa kutumia nguvu kasi na mviziaji mzuri sana. Ronaldo hakuwa na kipaji kama mawinga Lopez,Ginola, Overmars,Duff, Robben.Figo au Quaresma n.k lakini amewapita wote hao kwa mafanikio sababu ya kujtuma na kuishi kwa malengo

Wayne Rooney katika kitabu chake ''my decade in the premier league''
cristiano-ronaldo-553-and-wayne-rooney-receiving-awards-in-2008-2009.jpg

Anamzungumzia Ronaldo kama ''mtu mmoja bishoo mno na ana kioo karibu na kiti cha kubadilishia nguo old traford na kabla ya mechi au mazoezi ni lazima ajiangalie na kujiweka vizuri nywele zake kabla ya kuingia uwanjani'' lakin anampongeza kwa kusema hajapata kuona dunian mtu anaejiamini kama Cristiano Ronaldo
''Nakumbuka aliwahi kutumbia mazoezini nataka kuwa mchezaji bora wa dunia na baada ya kurudi toka katika world cup 2006 nikaona haswa mabadiliko na kujituma kwa Cristiano na akaacha yale madoido yake uwanjani na chenga nyingi na akafocus katika kufunga magoli na kushinda mechi'' maneno hayo aliyasema rooney miaka mingi iliopita na leo hii Cristiano Ronaldo ana tunzo 4 za ballon d'or!!!

Na mafanikio hayo ya Ronaldo hayakuja kama mvua bali amevumilia mengi matusi na kelele za mashabiki vichaa wa uingereza kila wiki hasa baada ya kumsababishia kadi wayne Rooney katika world cup 2006 na wengi walidhani asingerudi uingereza,lakini hakujali maneno ya watu akaja kutengeneza partnership ya hatari pamoja na Rooney Tevez akiwapa Man U mataji matatu ya Barclays na taji moja la Uefa Champions League,ni winga wa kwanza katika historia kuweza kufunga magoli 42 katika mashindano yote na magoli 31 Barcalys premier league akiifikia record iliyowekwa miaka 12 nyuma na mshambuliaji wa kati Allan Shearer!!!!

Kisha akaenda Spain kwa rekodi ya dunia wakati huo paundi million 80 na Florentino Perez akasema wazi ''tumemnunua Ronaldo ili kuja kuumaliza ufalme wa Barcelona'' ambayo ilikuwa inaonekana haishindiki wakati huo Xavi,Iniesta na Messi wako katika kilele cha ubora wao na ikaonekana Barca ingekuja kutawala miaka mingi kutokana na kuwa na vijana wengine wenye vipaji kutoka la masia kwa hiyo ikaonekana Ronaldo kuumaliza ufalme wa la masia itakuwa ndoto.
ronaldo7.jpg
Ronaldo-burns-Camp-Nou-with-shirt-celebration-696x464.jpg

La liga haikuwa rahisi kwani kila wiki alikuwa pia anazomewa na mashabiki wa timu pinzani wakimuona yupo mbali sana kujifananisha na kuufikia uwezo wa Messi, na wakati mmoja alihojiwa na muandishi wa habari anajisikiaje anapozomewa namna hiyo akasema yeye anapenda kuzomewa sababu hilo ndilo linalompa nguvu zaidi na kumfanya ajitume
Ronaldo hajamuangusha Florentino Perezi ni kweli magoli 17 katika mechi 32 alizokutanana na Barca mataji matatu ya Uefa na mawili ya la liga!!!

PESA

Ronaldo ni tajiri analipwa mshahara paundi million 19.5 kwa mwaka sawa na billion 58 za madafu:eek::eek::eek:
Ronaldo CR7 Endorsement deals 1.jpg

Ronaldo CR7 Endorsement deals 2.jpg

ana mkataba na kampuni ya Nike wenye thamani ya dola 21.7milion (Billion 45.5 za bongo) kwa mwaka na sio tu Nike ana mapato mengine kutoka Toyota, Samsung, Arnmani n.k ambayo yanamuingizia dola milion 10.7 milion(billion 24 za bongo) kwa mwaka
Sio tu soka bali bali ni mfanyabishara na hajatosheka na utajiri wake tayari ana malengo na anajua nini atafanya baada ya kustaafu soka
Anauza mavazi na viatu vya CR7 vinavyomuingizia dolaa million 6 hadi 10 kwa mwaka
Photo0363.jpg

Cristiano-Ronaldo-CR7-Underwear-Launcg-Dsquared2-high-top-stud-sneakers.jpg

dd1f2e681332.jpg

ana Hotel New York, Funchal, Madrid na Madeira
hqdefault.jpg

Messi anaweza akaja kumpita Ronaldo kwa mataji na tuzo lakini linapokuja suala la pesa Ronaldo ni habari nyingine

Kuna mambo muhimu matatu au manne yachukue kutoka kwa Cristiano Ronaldo
Juhudi na kujituma ndiyo nyenzo za mafanikio
Jiamini
Penda kazi yako nawe mwenyewe jipende bila masharti
Ishi kwa malengo umri na ujana unakimbia haraka sana

A person who doesn't fear to die lives fully
 
Tanzania. Mtu unakufa na kipaji chako. Nilipokuwa na miaka 15. nilikuwa napiga mpira balaa. Mpaka wakawa wananiita okocha. Nilikuwa napiga chenga kweli. Lakini baba hakupenda nicheze mpira alitaka jioni niende madrasa nikawa siendi naenda kucheza mpira. Kuna siku akaja kugundua siendi madrasa.
Kadri ninavyozidi kukua na ndoto za kucheza mpira zinapotea. Na majukumu yananisonga. Nazeeka huku zawadi niliyopewa na mungu ya mguu wa kushoto nimeshindwa kuitumia.
 
Usijilaumu mkuu. Baba alikuwa na malengo na mwanae.

Ulichokuwa unakikimbia vile vile kilikuwa na manufaa makubwa kwako.
 
Tanzania. Mtu unakufa na kipaji chako. Nilipokuwa na miaka 15. nilikuwa napiga mpira balaa. Mpaka wakawa wananiita okocha. Nilikuwa napiga chenga kweli. Lakini baba hakupenda nicheze mpira alitaka jioni niende madrasa nikawa siendi naenda kucheza mpira. Kuna siku akaja kugundua siendi madrasa.
Kadri ninavyozidi kukua na ndoto za kucheza mpira zinapotea. Na majukumu yananisonga. Nazeeka huku zawadi niliyopewa na mungu ya mguu wa kushoto nimeshindwa kuitumia.
pole mkuu ndiyo ilivyo africa tuna vipaji vingi vya soka ila mipango mizuri ya kuviendeleza hatuna.tungekuwa na mipango leo hii tungepata kina samata wengi sana
 
Wazazi wetu waliamini bila kusoma hakuna mafanikio. Kumbe walikuwa hawajui hata kipaji ni elimu tuliofundishwa na mungu. Tangu matumboni mwa mama zetu. Mwisho wa siku tunalazimishana kwenda shule tunakwenda kufeli. Mimi mwanangu akiniambia anataka kuwa fundi gareji. Hata Akiwa na miaka 5. Nitampeleka akajifunze.
 
ila ni haki kwa mzazi kumuhimiza mtoto katika elimu zaidi kuliko michezo sababu michezo/soka letu na mfumo wetu sio wa kuaminika, mfano binafsi nilisikitika sana mchezaji kama Alfonce Modest ambae aliwahi kuitumikia hadi timu ya taifa kukosa hata pesa ya matibabu baada ya kustaafu soka, vilabu vyetu vinawatumia wachezaji kama big g wakiisha utamu vinawatupa
 
Wazazi wetu waliamini bila kusoma hakuna mafanikio. Kumbe walikuwa hawajui hata kipaji ni elimu tuliofundishwa na mungu. Tangu matumboni mwa mama zetu. Mwisho wa siku tunalazimishana kwenda shule tunakwenda kufeli. Mimi mwanangu akiniambia anataka kuwa fundi gareji. Hata Akiwa na miaka 5. Nitampeleka akajifunze.
Mbwana Samatta amezaliwa na kukulia Mbagala leo yupo Genk.Wazazi wake na yeye walitaka asome na aende madrasa lakini akacheza soka.Kesho na keshokutwa hata Mrisho Ngassa na Haruna Moshi Boban nao watawalaumu wazazi wao!
 
Tanzania. Mtu unakufa na kipaji chako. Nilipokuwa na miaka 15. nilikuwa napiga mpira balaa. Mpaka wakawa wananiita okocha. Nilikuwa napiga chenga kweli. Lakini baba hakupenda nicheze mpira alitaka jioni niende madrasa nikawa siendi naenda kucheza mpira. Kuna siku akaja kugundua siendi madrasa.
Kadri ninavyozidi kukua na ndoto za kucheza mpira zinapotea. Na majukumu yananisonga. Nazeeka huku zawadi niliyopewa na mungu ya mguu wa kushoto nimeshindwa kuitumia.
Mkuu tatizo hatuko na mifumo mizur si wewe pekee yako,tupo wengi lakin mifumo imetuangusha, enzi zangu nilikuwa naudananda kweli.. jina la kichogo(thierry henry) halikuja bure, sasa limebadilika na kuitwa diego simeone... Nakumbuka niko o level nilikuwa nasoma morogoro, shule yetu michezo si kipaumbele, ikaja umiseta sijui ikawa lazima tushiriki, tukaulizwa wanaotaka kucheza, niliingia kipindi cha pili, na hii ilinisaidia kidogo maana pumzi zilikuwa kisoda,aisee game yetu nilipiga mpira mwingi kwa dakika km 30 hv kabla pumzi kukata, nakumbuka mashabiki wa timu pinzan walikuwa wananishangilia, baada ya game kuisha walikuja kunipa pongez kibao na kuniomba niwe napiga nao mazoezi.. beki yao iliniambia "we jamaa fundi saana" akanitania ungekuwa ulaya hamna hamna tottenham au valencia ungekipiga.. tukatabasamu kila mtu akashika njia yake

Lakin leo km ntamwambia mtu asienijua km niliupiga mwing ngumu kuamin, vipaji vingi vinapotea, huko moro vijijin niliona watu wanaupiga mpira mwing, kuna dogo sijui yuko wapi, niliamin atakuja kucheza ligi kuu bongo ila mpaka leo jina sijaliskia.. kijij kizima yeye ndio kilikuwa kipaji bora zaid kwao.
 
Ni kweli kiongozi 100%
 
Mbwana Samatta amezaliwa na kukulia Mbagala leo yupo Genk.Wazazi wake na yeye walitaka asome na aende madrasa lakini akacheza soka.Kesho na keshokutwa hata Mrisho Ngassa na Haruna Moshi Boban nao watawalaumu wazazi wao!
ni kweli mkuu ndo maisha wakati wengine hujui nini kitakusaidia maishani kipaji au elimu?
 
Tanzania. Mtu unakufa na kipaji chako. Nilipokuwa na miaka 15. nilikuwa napiga mpira balaa. Mpaka wakawa wananiita okocha. Nilikuwa napiga chenga kweli. Lakini baba hakupenda nicheze mpira alitaka jioni niende madrasa nikawa siendi naenda kucheza mpira. Kuna siku akaja kugundua siendi madrasa.
Kadri ninavyozidi kukua na ndoto za kucheza mpira zinapotea. Na majukumu yananisonga. Nazeeka huku zawadi niliyopewa na mungu ya mguu wa kushoto nimeshindwa kuitumia.
Kwahyo ulitaka usiende madrasa ukacheze mpira..???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom