CRDB ndo nini kufanyiana Weekend kuwa Mbaya?

CRDB ndo nini kufanyiana Weekend kuwa Mbaya?

32Roberts

Senior Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
109
Reaction score
17
Ajabu kuanzia Asubuhi mtandao wa CRDB Bank umekuwa ni wa kusua sua na Jioni hii wamezima ATM machine zote.Mwezi mzima wa January Shkamoo bata ilikuwa Baba Mkwe.

Kwa kuzingatia ni mwezi dume ambao una tar 45- 65 Kwa. Baadhi ya watu maana wengine walipokea mishahara nov na wengine katikati ya Dec na kwa kuzingatia holiday.

Kutokana na sababu hii niliona bora kusherehekea Kuisha kwa Mwezi dume.

Ila matarajio yametumbuka Nyongo Baada Ya ATMs kuninyima hela hivyo kulazimika kuendelea na Mfungo wa Lazima.

CRDB mtaacha lini hii tabia maana hata Holidays huwa mnazima Mashine zenu au tuanze kuweka fedha kwenye vyungu?leo mmeumiza watu wengi.
 
Ni kweli CRDB kuna tatizo. Kwa muda mrefu sasa sisi tunaopitishia mishahara yetu CRDB tunapata shida sana. Awali mishahara ilikuwa inaingia kati ya tarehe 28 hadi 30 ya kila mwezi. Siku hizi tunakaa hadi tarehe 8 hata 15 ya mwezi ili mshahara kuingia. Kuna nini? Tunawaza kuhamia NMB kwani wako 'on time'.
 
Back
Top Bottom