AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,898
Nimechukua ka m 14 toka CRDB hapa mkoa fulani, kwenye account wameniwekea m 13.4 yaani kama laki sita yote wamekata hawajadeposite. nikawafuata, walitakiwa wanikate kwenye mshahara wangu laki tatu na nusu kila mwezi, toka kwenye laki sita hapo ukitoa laki tatu na nusu inabaki kama laki mbili na nusu (250,000/=), wakasema kuwa, hiyo laki tatu na nusu ambayo wamenikata hata kabla mwezi haujaanza wamechukua kama bond, mshahara wangu ukikatwa na wao kuletewa watanirudishia kwenye account yangu.
Matokeo yake, mshahara ulishakatwa na inavyoonekana ni kama hawatarudisha kwenye account yangu, tatizo ninaloliona ni kwamba, hela hiyo imeenda wapi, imeenda kwenye mifuko wa wafanyakazi wa bank au imekuwaje, nimekatwa hata kabla mwezi wa kukatwa haujaanza. bahati mbaya nimesafiri niko mbali kurudi eneo husika si chini ya miezi miwili.
Kama kuna mfanyakazi wa CRDB hapa atueleweshe, hivi garama za kushughulikia nyaraka za mkopo mnakata hadi kufikia laki tano hadi sita kwa hela ndogo kama hiyo au? Nikiwapigia simu wanasema nimeshakatwa, na hela kwenye statement haipo, haijaingia, bahati mbaya zaidi ni kwamba wao wanalete e-statement kwenye email yangu kila mwezi hivyo inaonyesha kila transaction niliyoifanya.