CRDB bank wizi huu ni kwanini?

crdb wametoa promotion ya gari ndio hivyo tunamnunulia mwenzetu gari
 
Yani unaweka hela zako benki wanazitumia kuzungusha na kutengeneza faida, inakuwaje wakate tena makato ya kipuuzi?? Yani ukiweka 10,000 inakatwa inaisha yote na bado unadaiwa.

Siwashangai wanaoweka fedha zao benki za ulaya. Hawakumbani na upuuzi kama huu.
 
benki ni kama serikali....wakati mwingine wanavinjia vya kishenzishenzi vya kuongeza mapato...
 
Ngoma ni kurudi kwenye zile bank zetu za asili za ama chungu au kishimo chini ya uvungu wa kitanda.
 
WEZI wakubwa hawa.
Nina ka account kangu ka dollar na difference iliyopo ukichukulia pesa kwenye ATM (Tshs) na ukichukulia ndani ni kubwa mno.Exchange rate katika ATM ni ndogo sana.
 

Mimi nadhani kuna haja pia kwa sisi wenyewe kubadili fikra zetu juu ya huduma za kibenki. Hivi kuna haja gani ya kuingia ndani ya tawi la benki ili kupata salio tu?
Benki zimetoa njia mbadala nyingi kama Huduma kwa Simu za Mkononi (Simbanking), ATMs, internet banking n.k ili kurahisisha mambo kama haya.
Siku hizi benki sio tawi tena, hivyo kama unaona kuomba salio ndani ya benki ni gharama, kwani usitumie Simbanking au hata ATM? .
Price segmentations zinalenga kufanikisha mambo kadhaa ikiwemo decongestion , hili la ada ya kuulizia salio sio jipya sana nchini kwani mabenki yote ya kigeni (ikiwemo NMB) hutoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…