WEZI wakubwa hawa.Leo nimeenda bank ya CRDB kama ilivyo ada kabla ya kuchukua mkwanja mteja unapenda kujua salio lako.. yaani balance inasomeka je. kuingia nakumpatia mhudumu wa benki, ananiambia kuna utaratibu mpya.
Andika jina na account number yako kwenye kitabu kisha utachajiwa gharama ya kuona au kjua salio lako ambao ni shilling 500/=. Nilishikwa na mstuko, maswali mengi yakaniijia kichwani.Je hii huduma ni ya kulipia.
je huu sio wizi wa mchana kweupe.kila mwezi kuna makato ya benki "monthly service fee" kila ukitoa hela wanakata, "withdrawal fee" mwajiri wako au money transfer ikifanyika wana kukata "service fee" n.k hapo ni kwenye account zetu za akiba.
Hivi nini maana ya monthly fee? kama haijumulisha na kutoa balance ukiomba na hadi leo sijawahi kutumiwa bank statement ya accounti yangu yapata miaka 5, je benk wanatoa huduma gani kwangu, kama hawatumi monthly statement ya account kwanini nisiombe balance? nikiomba kwanini nilipie.
Mamlaka ya kusimamia haki za mlaji/mteja yapo wapi. BOT regulator na supervisor wa mabenki mnalijua hilo? hiyo fee inamnyonya mlaji na mteja wa huduma ya benki, kumbuka salio langu na lako na mwenigine ndo sehemu ya mikopo CRDB wanatoa na kupata faida kubwa.
CRDB Bank Please tafadhali acheni wizi wa mchana kweupe, hiyo gharama mliyo ileta haitafanikisha kuongeza wateja, labda kama mnataka kupunguza wateja.
Nawasilisha.
SP
Naungana na ww kiukweli iyo chaji waliyoleta itamuumiza Mteja, kama staff ameajiriwa kukaa kaunta ili ahudumie Wateja iweje sasa mtuchaji walaji? Mbona miaka yote iyo chaji haipo , au waneona ndio chanzo cha mapato? Hii kitu niliwahi kuisikia nmb !!
Mm siongelei crdb tu , je taifa letu...
Imagine unapata mshahara unakatwa PAYE iyo ni kidogo , alaf inaingizwa kwenye Akaunti wanakata 3,000 salary processing fee, kwenye Akaunti unakatwa 1000 ya mwezi, mila ukitoa wanakata 700 kwenye ATM, alaf ukikusanya mshahara ili uzungushe upate faida unaambiwa nenda mamlaka za vibali, uko hela iyo iyo ya mshahatmra uliyokatwa kodi mwanzoni, inakatwa tena kodi kwenye vibali, then ukiwa na ako ka biahsara unalipia tena mapato ya biashara, unalipia pango alaf kwenye mshahara/ au kama ni loan wanakata interest....hili taifa uchumi kama ulivo dunia nzima uko kinyonyaji zaidi kwa low income earner.
Mwanajf kama una elfu20 au50 bila chanzo cha kuaminika chukua 50 yako weka nyumbani kumiliki Akaunti ni sawa na kutoboa gunia lako la nafaka eti nafaka zipate hewa , zitaisha kwa kudondoka, ebu fikiria:
Umedeposit elfu20
makato ya kadi 4000
Monthly maintainance 1000
Minimum balance 10,000
ATM fee700
Utaletewa cash available 4,300/= kwenye elfu20 unabaki na 4300
Unaambiwa Mpendwa mteja huwezi kuchukua hela haitoshelezi, ongeza Salio !!
Mambo gani haya??
Tunaangamia!!