mkuu wapo labda kama wamelichukua ila kujibu hapa hawawezi mana washapigwa konzi hiliHivi hakuna mfanyakazi wa crdb humu? Ili ajibu hizi tuhuma?, ukimya unazua maswali na mashaka dhidi yenu.
Leo nimeenda bank ya CRDB kama ilivyo ada kabla ya kuchukua mkwanja mteja unapenda kujua salio lako.. yaani balance inasomeka je. kuingia nakumpatia mhudumu wa benki, ananiambia kuna utaratibu mpya.
Andika jina na account number yako kwenye kitabu kisha utachajiwa gharama ya kuona au kjua salio lako ambao ni shilling 500/=. Nilishikwa na mstuko, maswali mengi yakaniijia kichwani.Je hii huduma ni ya kulipia.
je huu sio wizi wa mchana kweupe.kila mwezi kuna makato ya benki "monthly service fee" kila ukitoa hela wanakata, "withdrawal fee" mwajiri wako au money transfer ikifanyika wana kukata "service fee" n.k hapo ni kwenye account zetu za akiba.
Hivi nini maana ya monthly fee? kama haijumulisha na kutoa balance ukiomba na hadi leo sijawahi kutumiwa bank statement ya accounti yangu yapata miaka 5, je benk wanatoa huduma gani kwangu, kama hawatumi monthly statement ya account kwanini nisiombe balance? nikiomba kwanini nilipie.
Mamlaka ya kusimamia haki za mlaji/mteja yapo wapi. BOT regulator na supervisor wa mabenki mnalijua hilo? hiyo fee inamnyonya mlaji na mteja wa huduma ya benki, kumbuka salio langu na lako na mwenigine ndo sehemu ya mikopo CRDB wanatoa na kupata faida kubwa.
CRDB Bank Please tafadhali acheni wizi wa mchana kweupe, hiyo gharama mliyo ileta haitafanikisha kuongeza wateja, labda kama mnataka kupunguza wateja.
Nawasilisha.
SP
Hapo kwenye RED wanalijua sana na wala usipoteze muda kuangaika nao kwani hautafanikiwa, labda ni sehemu ya ulaji huu. Unajua jinsi mabenki yanavyoibia watu kwenye mikopo ama umesahau, hali ni ngumu na hao hao BOT wanabariki kwani mwisho wa mwaka wanatumiwa Calender za mabenki husika labda na vijizawadi vingine.Mamlaka ya kusimamia haki za mlaji/mteja yapo wapi. BOT regulator na supervisor wa mabenki mnalijua hilo? hiyo fee inamnyonya mlaji na mteja wa huduma ya benki, kumbuka salio langu na lako na mwenigine ndo sehemu ya mikopo CRDB wanatoa na kupata faida kubwa.
CRDB Bank Please tafadhali acheni wizi wa mchana kweupe, hiyo gharama mliyo ileta haitafanikisha kuongeza wateja, labda kama mnataka kupunguza wateja.
Nawasilisha.
SP
watetezi wetu washajifia wao wanaona sawa tu sisi kuumizwa hakika inauma sna mkuu
CRDB wanafanya hivo kwa kuwa wana wateja wengi mno na kimsingi wengine hawana haja na nyie.
Nashangaa mtu analalamika wakati kuna benki kibao ndogo na zinakupa huduma zote kama crdb au zaidi. Siku hizi kuna mobile banking zinazotolewa na bank nyingi hata zile ndogo. Kwa nini mnakaa CRDB?
Ukiendelea kukaa, tulia waendelee kukufaidi na usilalamike make ni uzembe
Nilishasema hapa siku moja uzalendo kamwe hautaletwa na makampuni ya nje kwanza inapaswa makampuni ya ndani yaoneshe uzalenzo! nasikitika siku hizi tunashindwa kutofautisha kampuni la nje na la ndani wote wamejikita kutafuta overprofit kwa kumuumiza mwananchi haijulishi kampuni za simu au laa! mfano mzuri kampuni za sukari zinazalisha sukari nchini zinauza 2000 kwa kilo moja wakati za nje zinauza 1600 mtaani
mara nyingine mi natamani hata bora makampuni ya nje tu tujue moja tunaibiwa kuliko kuumizwa na watanzania wenzetu hebu fikiri mtu anaelipwa mshahara laki mbili bank si atachukua laki na nusu kunakoelekea kwa ajili ya uhujumu huu unaofanyika wa taasisi binafsi
Hata Mimi nmesikia rafiki yangu analalamika kuwa naye kaibiwa.Kwa kweli sio vizuri maana Tumewaamini ili muhifadhi pesa zetu alafu mnatuibia acheni huo mchezo
Hivi hakuna mfanyakazi wa crdb humu? Ili ajibu hizi tuhuma?, ukimya unazua maswali na mashaka dhidi yenu.