kazikubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 597
- 151
Imekuwa ni mchezo wa kawaida kwa benk ya CRDB kuwafanyia makusudi watumishi wa Serikali kwa kuchelewesha kupost mishahara hiyo kwenye akaunti za watumishi. Kwa mfumo wa Serikali mishahara yotye huanzia NMB ambao nao hizitawanya kwenye benki nyingine. Mara zote hutokea watumishi wote wanaolipwa kupitia benki nyingine hupata mishahara yao mapema na wa CRDB huchukua zaidi ya wiki licha ya kuwa wameipokea mapema. Mchezo huo umeanza mwezi October, 2012.
Kuna habari za chini chini eti kuna ugomvi wa kibiashara kati ya benk hizo hivyo wanakomoana. CRDB acheni hizo, hamuikomoi NMB bali mnawatesa wateja wenu.
Kuna habari za chini chini eti kuna ugomvi wa kibiashara kati ya benk hizo hivyo wanakomoana. CRDB acheni hizo, hamuikomoi NMB bali mnawatesa wateja wenu.