ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Kiukweli inauma sana, Watumishi wa serikali ambao waliokuwa wanahitaji huduma za mikopo toka benki hii wanaendelea kusumbuka pasipo sababu za msingi .
Tangu mwezi march / April fomu za mikopo zimerundikana benki huku fomu hizo zikiwa zimeshakamilka kwa kupitishwa kwa waajiri wao na wengine mikataba imeshajazwa inafikia hatua ya kuingiziwa fedha benki inasimamisha taratibu kwa madai kwamba imesimamisha kutoa mikopo kwa waajiriwa wa serikali.
Huu ni usumbufu kwani kama mngekuwa na plani hiyo mngesema mapema ili watu wasihangaike na benki yenu ili waende mabenki mengine yanayoendelea kutoa mikopo kama NMB , posta nk..
Kila mtu anapoamua kuchukua mkopo anakuwa ameshaona opportunities mahali fulani hivyo ana target akope aielekeze fedha huko kwenye mzunguko kama biashara za mazao nk. Sasa mnawapotezea malengo watu.
Isitoshe mtu anaamua kwenda kuchukua fomu zake ili azipitishe upya kwa mwajiri wake ili apate mkopo toka benki nyingine, waajiri wanagoma kwa madai kwamba walishampitishia awamu ya kwanza, hivyo kupelekea sasa watu kuhonga ili wajaziwe fomu upya.
Sasa huo usumbufu wote huo ni wa nini au mnagawana pasenti na maafisa utumishi. Waruhusuni watu wapewe mikopo , mbona benki nyingine wanakopesha .