CPC inajali mustakabali wa Dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Gianna Amani

Wadau mbalimbali wameeleza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinajali mstakabali wa watu wote duniani, amani haki na ushiriki wa pamoja katika kutatua changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa na siku zijazo.

Hayo yalielezwa na baadhi ya wachangia mada na washiriki katika kongamano la uelewa juu ya Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomonisti cha China (CPC) lililoandaliwa na Taasisi ya historia ya Chama na fasihi kwa kushirikiana na shirika la habari la China, Xinhua.

Akitoa neno la ufunguzi katika kongamano hilo mkuu wa taasisi ya historia ya chama na fasihi Qu Qingshan alirejea hotuba ya Katibu Mkuu wa CPC Xi Jinping wakati wa mkutano mkuu wa 20 pale alipogusia msimamo wa chama hicho kuhusu masuala ya dunia.

“Kama Katibu Mkuu alivyoeleza China inatarajia kuendelea, busara zake na suluhisho la kichina katika mataifa mengine kwa mustakabali wa pamoja kwa watu wote duniani sambamba na kuhakikisha kuwa dunia inakuwa na Amani na haki,” alisema Qingshan.

Mhariri Mkuu wa Xinhua na naibu Mkurugenzi wa kamati ya kitaaluma ya utafiti wa china mpya Lyu Yansong alisema wito ni kwa nchi zote duniani kuunga mkono amani na haki na kukubali kujifunza kutoka kwa nchi nyingine.

“Ni muhimu kujifunza kutoka kwa mwingine ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo kwa maslahi ya maendeleo ya wananchi,” alisema Yansong.

Naye Mtaalamu wa kiingereza katika taasisi ya historia ya chama na Fasihi Sean Slattery alisema miongoni mwa mambo ambayo dunia inapaswa kujifunza kutoka kwa China ni namna ambavyo taifa hilo limewaondoa watu milioni 800 katika umasikini ndani ya miaka 40 tu.

Aidha katika hotuba ya Xi katika mkutano mkuu aliweka msimamo kuwa katu China haitafanya umwamba, kuingia uhuru wa nchi nyingine wala kuvamia nchi yoyote kimabavu kwa kuwa inaheshimu misingi ya uhusiano wa kimataifa na haki duniani.

“Siku zote China inaamua msimamo na sera zake kufuatia hali halisi, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, inapinga kithabiti aina yoyote ya umwamba na siasa za kinguvu,” alisema Jinping wakati ambako umwamba wan chi kubwa dhidi ya nchi nyingi umekuwa ni mtindo mpya wa dunia.

Xi alisema China inaheshimu nchi zote bila kujali ukubwa na udogo wala nguvu ya kiuchumi na inapiga wazo lolote la vita baridi, vitendo vya kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine hivyo katu haitafanya kinyume na imani yake kwa kufanya umwamba na kuvamia nchi yoyote Duniani.

图像_2022-11-03_130024758.png

图像_2022-11-03_130046995.png
 
Back
Top Bottom