Habari zenu wana JF,
Covid-19 ni jina la ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Corona kinachoshambulia mfumo wa upumuaji kwenye mapafu. Kwa kirefu ni Corona Virus Disease 2019, hivyo 2019 ndiyo wataalamu wameugundua baada ya kuanza kule mji wa Wuhan nchini China na kusambaa duniani kote.
Hapa kwetu Tanzania uliingia kwa kuletwa na watu waliyotoka nje katika nchi zilizo athiriwa na ugonjwa huo, kwa kuwa hatujakuwa na elimu ya kutosha pamoja na kutochukulia tahadhari baadhi ya watu waliweza kuambukizwa na wengine kupoteza maisha.
Hivyo basi ili tuchukuwe hatua za kuutokomeza ugonjwa huu ni lazima elimu ya kutosha itolewe juu ya hili gonjwa kwa kuufahamisha umma juu ya asili ya ugonjwa huu na jinsi unavyoathiri watu kiafya, kisakolojia na kiuchumi na unavyoweza kuambukizwa. Kama wataalamu wa kizungu walivyoupa jina la Corona Virus Disease 19, kwa Kiswahili ina maana gani?
Corona ( Crown) = Taji
Virus = Kirusi
Disease = Ugonjwa
19 = 19
Hivyo basi kwa kiswahili tunaweza kusema ni " Ugonjwa wa Kirusi cha Taji 2019" kwa kifupi ni " UKITA-19" ili tuweze kuupa jina kama vile tulivyo upa jina AIDS= UKIMWI.
Hivyo basi hilo ni pendekezo kama kuna pendekezo lingine tujadiliane. Kwani tukianza kuwa na jina letu tutaweza kuona huu ugonjwa unatuhusu na kuzingatia jinsi ya kuutokomeza kwa njia mbalbali kama vile kujifukiza kwa miti shamba na kutumia tiba mbadala ili tuweze kutoka katika hali hii ya kujifungia ndani.