Core values

Annina

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
437
57
Nimekuwa nikisoma mijadala mingi humu JF na kuona jinsi watu wanavyochangia kwa mitizamo tofauti tofauti. Katika hilo nime note lugha inayotumika kuunga mkono au kupinga hoja ina umuhimu mkubwa sana kwa audience wako. Kwa mfano unaweza kuonekana mbabe badala ya kuwa unapingana na hoja simply kwa sababu ya choice of words...

Nimeamua kulileta hili lijadiliwe naamini litatujenga, maana pengine choice of words inatokana na core values mtu alizonazo na si kwa bahati mbaya, hili linajidhihirisha kwenye post zetu humu ndani, kila mtu ana language yake hata bila signature unaweza kutambua nani mwandishi!


Wataalam wa psychology wanasema binaadam wana core values zifuatazo:
  1. Honesty
  2. Compassion
  3. Recognition
  4. Independence
  5. Curiosity
  6. Security
  7. Diversity
  8. Power
  9. Harmony
Kutokana na core value/s mtu alizonazo, kuna tofauti kubwa ya kimtizamo kwa mfano mtu wa harmony na power hawawezi kuwa na mtazamo na lugha inayofanana wanapojenga hoja zao juu ya jambo fulani. Point yangu hapa ni kwamba tunapojadiliana tuwe na uelewa wa tofauti zetu ikiwemo hii ya values nadhani itasaidia sana.



Naomba wenye uelewa zaidi juu ya jambo hili wasaidie kuweka mambo sawa kwa manufaa yetu wote.

Wewe core value yako ni ipi/zipi? tafakari...
 
Back
Top Bottom