Aha! Sasa nimekuelewa. Kumbe wewe huamini au hujaamini bado! Basi nikuulize pia: kama wewe huamini kuwa Mungu yupo na mtu mwingine anaamini Mungu yupo, inakuwaje? Yaani, wewe usiyeamini utaweza kumthibitishia anayeamini kuwa unachosema ndiyo kweli tu na yeye anachoamini kuwa ni upuuzi?
Kwa vile huamini siyo rahisi kukufanya uamini maana imani ni mchakato. Mtume Paulo kabla hajaamini alikuwa adui mkubwa wa Wakristo na alikuwa anawaua. Baada ya kuamini, alikuwa mwalimu mkuu wa kufundisha dini ya Kikristo. Kutoamini huwa nakufananisha na mtu asiyejua kitu (ignorant). Chukulia mtu asiyejua hisabati, halafu mwulize 'namba witiri' ni namba zipi, atakujibu? Lakini ikitokea akajifunza na kuelewa, ukimwuliza siku nyingine, atakujbu vizuri. Kwa hiyo, hata kwenye imani ni hivyo. Binafsi sikuwa naamini ila niliamini baadaye. Kwa hiyo, mimi sioni cha ajabu hapo. Kama huamini nakufananisha tu na mtu asijua kitu fulani.
Huwezi kufananisha imani na kujua, utachekwa.
Huwezi kuamini unachojua, na huwezi kujua unachoamini. Unaamini kitu usichojua, na unajua kitu ambacho umepitisha level ya kuamini.
Inaonekana unachanganya mambo. Sababu watu wa dini "wanaamini" katika mungu ni kwamba hawajui kwa uhakika kama mungu yupo. Wangejua wasingeamini, wangejua. Huwezi kukaa juu ya kiti, ukawa na uhakika kabisa kwamba umekalia kiti, halafu ukasema "naamini nimekalia kiti" utaonekana mwehu. On the other hand, ukifumbwa macho, ukawekwa ukalie juu ya kiti, ukahisi kwamba umekalia kiti, lakini kwa sababu umefumbwa macho hukioni kiti, lakini unahisi umekalia kiti, unaweza kusema "naamini nimekalia kiti" huna uhakika 100%.
Kuamini kunaashiria kutokuwa na hakika.Ndiyo maana dini ina deal na imani, haina hakika na mambo yake. Haiwezi kutoa proofs za kuonyesha roho iko wapi, mbingu iko wapi, motoni kuko wapi etc.Hizi ni imani tu, meaning hazijathibitishwa na hazithibitishiki.
And don't tell me to prove god doesn't exist, the onus of proof is always on the positive side. Wewe kama polisi unakuja nyumbani kwangu unasema "wewe una madawa ya kulevya unaficha humu ndani" huwezi kuniambia "nionyeshe kwamba huna madawa ya kulevya" nitakuona wewe mtu wa ajabu, nitakutegemea wewe unayesema kwamba nina madawa ya kulevya humu ndani, uje na search warrant, unionyeshe madawa ya kulevya yalipo nyumbani mwangu. Nionyeshe mungu yuko wapi?
Wakati, unless you resort to your age old refuge of "god works in mysterious ways" which is laughably nonsensical as to justify anything from anybody, ukimchambua mungu logically kwa mfano huo wa hapo juu utaona. Kwamba.
Either
Mungu si muweza wa yote
OR
Mungu hana mapenzi yasiyo kikomo kwa wanadamu
Or even better
Mungu ni kamba tu.
Otherwise kwa nini atengeneze mwanadamu mwenye mapungufu? Kwa nini amuumbe shetani? Kwa nini aumbe ulimwengu ambapo uovu unawezekana? Kwa nini aumbe ulimwengu unaoweza kuwa na matetemeko, vita, njaa na maovu mengine kama hayo yatakayoumiza na kuua mpaka vitoto vichanga visivyo hatia.
Huyu mungu kama angekuwa binadamu mwenzetu si tungempeleka kwenye mahakama ya mauaji ya halaiki kama wanavyopelekwa watu Arusha na The Hague huko?
Huyu ndiye mungu muweza yote kweli?
Hakuna mungu wala nini, tuache kupigana fiksi hapa. Ukiangalia historia ya mungu na dini utagundua ilianzishwa na watawala ili waweze kuwatawala watawaliwa vizuri. Kuanzia Babylon, mpaka Misri mpaka mpaka leo Uingereza, mfalme/ malkia ndiye mkuu wa dini.Vatican Papa ana title ya head of state, hata Marekani kina George W. Bush na mpaka Obama sasa wanatumia dini kama tool ya kisiasa kuweza kukaa madarakani.
Kama mungu ana uwezo wote mbona biblia na Quran zimejaa inconsistencies na uongo?
Kama alivyokuuliza mzee PlancScale hapo juu, kama unaamini kila kitu complex kama binadamu na ulimwengu ni lazima kiwe na muumba, then inevitably huyo muumba atakuwa more complex kuliko vilivyoumbwa, na yeye kwa sababu ni more complex atahitaji kuwa na muumba kwa mujibu wa kanuni yako, kwa hiyo mungu na yeye katoka wapi? Kaumbwa na nani? Haiwezekani akawa katokea tu au alikuwepo siku zote, kwa sababu ukisema hivyo unatoa an exception to the rule ambayo inaweza hata ku apply kwa mwanadamu na ulimwengu.Kama mungu hana mwanzo, au alijiumba mwenyewe somehow, what makes you think the same cannot apply to binadamu?
Nakushauri ukitafute kitabu cha Bertrand Russell kinaitwa "Why I Am not a Christian And Other Essays On Religion And Related Subjects". Jamaa yuko crisp and clean kichizi on these subjects.
Tatizo letu wanadamu tunapenda sana wishful thinking, hatutaki kuukabili ukweli mgumu kwamba hatuna big brother wa kutusaidia.Hakuna mungu wa kumuomba akakufanyia kazi yako. Wewe mwenyewe ndiye mungu na wewe mwenyewe ndiye shetani.Ukifanya vizuri ndiyo unakuwa mungu, ukifanya vibaya ndiyo unakuwa shetani.Hamna mungu wala shetani.
Tunapenda ku employ psychology ya mtoto na baba kwa sababu mostly ndivyo tulivyokua, tumekua na baba na mama wanatufundisha na kutulea, kutulisha na kutupigania, kwa hiyo tunapokua wakubwa na kuiona dunia ilivyo na challenge, tunataka ku employ wishful thinking kwamba kama tulivyokuwa wadogo tukawa na baba na mama, kuna "baba yetu aliye mbinguni" ambaye tunaweza kumuomba tu halafu akatutimizia.I wish life was that simple lakini ukweli ni kwamba mungu huyu personal wa kuombwa na kujibu sala hayupo.
To borrow from Raphael Patai from "The Arab Mind" kama waarabu, tunapenda "infatuation with ideal forms" to which we cling emotionally even while we know these forms are contradicted by reality.
I reject this baseless romantic, even chauvinistic, infatuation of a personal godhead.