Mkuu
Sting007 na
Mrimi,
Asanteni kwa elimu kidogo kuhusu hizi FTAs receivers.
1. Je mnaweza kujua iwapo hizo FTAs zinapatikana Dar? ( Iwapo nyie mpo Dar)
2.Hapo penye red...; receiver yaMPG4 ndio ipi? ndio hizo FTAs au?
Asante.
Ingawa mimi sio mtalamu sana wa hivi vitu lakini kwa kifupi iko hivi:
FTA maana yake ni Free To Air.Hizi ni channels ambazo zipo free kupata,kwa maana kwamba huhitaji kulipia.Vituo vya TV/Radio vinakuwa vinatumia satelite mbali mbali huko angani ktk kurusha matangazo yao ili kumfikia mtazamaji.Sasa kama ulishawahi kuona madishi kwenye paa za nyumba za watu(hata Dar yapo),maana yake ni kwamba wao wananasa matangazo ya TV kupitia hayo madishi.
Hii ni rahisi tu kuelewa.Kwa namna ulivyokuwa unatumia antena kunasa matangazo kutoka kwenye minara ya TV iliyopo kisarawe au maeneo mbalimbali nchini,ndivyo inavyokuwa katika kutumia madishi(satelite dishes),tofauti tu ni kwamba madishi badala ya kuelekeza ilipo minara ya matangazo,yenyewe huwa yanaelekezwa ilipo satelite inayorusha matangazo ya chaneli unayotaka.Kwa mfano,ukitaka kupata ITV,StarTV,TBC1 etc,unaelekeza dish lako upande wa mashariki.
Kumbuka huko angani kuna Satelite nyingi,na kila moja inacover eneo fulani la dunia.Kwa mfano,zipo zinazocover Asia au Europe tu,haziwezi kucover Africa au Amerika.Kwa hiyo wenye vituo wa tv/radio wanatumia satelites zinazocover eneo la watazamaji wake.Kwa hiyo kwa mfano local channels za TZ zinatumia satelites zinazocover eneo la TZ/East Africa.Kwa kwa hakika local channels zetu zinatumia satelite moja,except Ch10 inayopatikana ktk satelite zaidi ya moja.
Ukishatambua kuwa satelite zina coverage tofauti,warusha matangazo wanatumia satelite itakayoweza kucover as larger area as posible,kwa hiyo kwa local channels ztu za TZ zinatumia satelite inayocover TZ nzima.Hivyo basi hata wewe wa Dar ukitumia satelite dish utanasa kama watu wengine tulioko mikoani.Tatizo lilipoonekana ni kwamba TV nyingi za kwetu zipo Dar,na katika mfumo wa analogy uliokuwa ukitumika hapo awali uliwafavour watu wa Dar kwa kuwa ulikuwa ukichomeka tu antena kwenye TV screen yako unapata matangazo bila shida.Kwa mikoani ni tofauti kwa sababu minara ya kurushia matangazo ipo mjini na hasa miji mikuu ya mikoa;na kwa kawaida ile minara ina uwezo wa kurusha signal kwa umbali wa kilomita chache tu,kwa hiyo watu wa wilayani na maeneo yaliyopo mbali na mnara wanashindwa kunasa matangazo.Pia kituo cha TV/radio chenye mnara ktk eneo hilo ndicho kinachoonekana tu;na kwa hakika vituo vyetu vya tv/radio havijaenea kiasi kikubwa.Kutokana na sababu hiyo watu wa mikoani kimbilio lao kuu lilikuwa ni kununua madish ambayo kwa asili yake tayari yapo ktk mfumo wa digitali,ndio maana hili tufani la tarehe 31/12/2012 halikuwadhuru watu wa mikoani.
Kuhusu MPEG4 receiver iko hivi.Kama una deck ya kucheza CD hapo nyumbani utakuta wameandika ni aina gani ya format inacheza,kwa mfano,VCD,MP3,DVD etc.Hali kadhalika na tv nazo zina format ya urushaji wa picha/matangazo.Currently,tuna receivers za MPEG2 & MPEG4(plus some other different specifications),MPEG4 receiver inacheza pia video za mfumo wa MPEG2 ila MPEG2 haiwezi kucheza za MPEG4,hivyo basi ukiwa na MPEG4 unakuwa na uwanja mpana wa kupata matangazo ya tv nyingi zaidi kuliko mwenye MPEG2.
Pia upataji wa tv nyingi unategemea wewe umeelekeza dish lako kwenye satelite gani,ukubwa wa dish lako,aina ya receiver,fundi mzuri na mambo kadhaa ambayo fundi wako(mzuri) atakushauri.Kuna satelite zinakuwa na FTA channels nyingi kuliko zingine.Kwa mfano,satelite wanayotumia TBC1,Startv,ITV na wenzake,haina channels nyingi sana.Tatizo unaloweza kupata ni kwamba unaweza ukapata satelite yenye FTA channels nyingi na nzuri,lakini ikawa sio wanayotumia wenzetu wa local channels.Kwa hiyo hapo unaweza kuaamua mwenyewe aidha ubaki na local channels ambazo ni chache,au upate hizo zilizo nyingi,it's your choice!
Lakini pia usisahau kuwa sio local channels zote zinazotumia mfumo wa satelite ktk kuwafikia watazamaji wake.Kwa mfano,Mlimani tv,CTV,Sibuka etc hutaweza kuzipata kupitia mfumo huu.Na hizi ndio miongoni mwa TV zilizosombwa na mafuriko ya 31/12/2012.Kwa sasa local channels ambazo unaweza kupata kupitia mfumo huu ni TBC1,Startv,Ch10,ITV,EATV na Capital tv.