Computer programing na ma-software jamani!

Wakuu naomba na mimi nafasi japo nipate kuchangia kidogo, Programming kwa hapa kwet Tanzania ni Janga la kitaifa kama ilivyo kwa masoma ya Hisabati.Kwani kiukweli hakuna chuo cha serikali labda kama vipo vya binafsi vyenye waalimu ambao ni competent kwenye maeneo hayo.Si hivyo tu bali bado syllubus za vyuo vyetu havimuandai mwanafunzi kua programmer zaidi ya kufundishwa Introduction ya programming languages kama C++,Pascal,Visual Basic, etc, na jinsi ya kutengeneza very miner programas kam kujumlisha moja na mbili, with alote of blah blah katika masuala ya msingi kama arrays, linkers etc, Mitaala ya vyuo vyetu hakuna inaposisitiza katika masuala haya na wala serikali zetu na mashirika yetu ya binafsi ama hata costech wamekua hawaweki msisitizo wowote wa kuwafanya vijana wetu waconsentrate katika fani hiyo. Kwani katika kila mradi tumekua tukitafuta consultants kutoka nchi za nje,tukinunu software kutoka nje kwa kisingizia kuwa proffessionals katika eneo hilo hakuna wakati tunaruhusu certifications kam OCA,MCSTP etc, na kuwaita watu wenye vyeti hivyo kuwa eti ndo MaICT gurus.

Sijui tutafika wapi na changamoto mpya ya CLOUD computing ambapo watu wote waliosoma IT watakua ni watazamaji kwa sababu maanalist na maprogrammer wa MArekani, India, Uingereza na kwingineko wataweza kutoa support hukohuko walipo kwa kutumia clremote login.
 
Reactions: KXY
Kutengeneza software sio kazi ngumu kabisa, ukitaka kujifunza kutengeneza software mwenyewe unaweza kama uko tayari kuweka muda kidogo kwa ajili ya kujifunza huko, personally ninekushauri kununua kitabu nenda maduka ya bongo angalia wana vitabu gani vya beginners kisha nenda Amazon.com checki review zake nunua kizuri, ningekushauri kuanza na kati ya Java/C#/Python kama lugha ya kwanza. Kama hauwezi kununua kitabu kuna vitabu vya bure kibao mfano C Sharp Programming Course kuna list ya vitabu vya bure hapa free - List of freely available programming books - Stack Overflow.

Pia siku hizi kuna video course kibao za bure unaweza kufanya tena kutoka university bora duniani Stanford/MIT/IIT etc.

Introduction to Computer Science I | Harvard Video Course

Computer Science I: Programming Methodology | Stanford Video Course

Introduction to Computer Science and Programming | MIT Video Course

NPTEL PHASE 2 - Courses

Zaidi ya hapo search YouTube au Google tutorial za programming yoyote utapata.
 
Umeongea kitu cha maana sana kuhusu Cloud Computing mkuu. Wasiwasi wangu ni kwamba taasisi zinazoendeshwa kifisadi hazitakuwa tayari kuhamia huko maana watu wateweza hack nyaraka nyeti. lakini 10 to 15yrs to come nafikiri itakuwa hakuna jinsi lazima tuelekee huko
 
Ahsante bro! Katika course ninazosoma Mathematics imo, katika kozi za Math tumesoma introduction za kozi kama (C++ na Numerical Analysis)! Nahisi nitafikia malengo yangu...........!
 
Reactions: KXY
Ukweli ni kwamba kutengeneza commercial software kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ni jambo gumu. unaweza tengeneza software inayofanya a b c kwa kampuni au taasis A. its ok, kwa sababu its unlikely kwamba itaonwa na kutumiwa nje ya hiyo taasisi A. lakini kutengeneza ambayo inauzwa kibiashara its not a joke my friend. There are a lot of things that need to be considered and handled accordingly eg multi user support, session handling, security, easy of use, modularization etc. Haya mambo yote hatafundishwa universities za Tz. Kimsingi mwanafunzi anayemaliza chuo computer science au IT or Whats ever they call it, anakua amejifunza introduction tu kumuwezesha kusomea kazi. Bahati mbaya hapa kwetu wakipata hicho ki degree ndo wanajiona wamefika. Software industry hapa bongo bado sana. We need to do something.
 
kwa ushauri wangu unaweza soma software engineering hapo utajifunza language mbalimbali za kompyuta na utakuwa jirani sana na mambo ya software japo utengenezaji wa software ni jambo gumu lakini ukiwa na bidii utafanikiwa, zaidi ya hapo mimi mwenyewe nasoma S.E ni mahali sahihi kwa mahitaji yako. lakini uctegemee wepesi hata kidgo.
 

Ni kweli aisee.
 
Nimeona watu wanataja hesabu. Je ni hesabu gani hizo unazohitaji kujua kuwa programmer mzuri. Is it Logic mathematics au trigonometry ?

Binasfi nilipass tu programming. NIna theoretical knowledge ya programming nzuri tu lakini practical applicatin na experince mhhhh. Na hili nadhni ndio tatizoletu wengi.

Kingine nilikuja kugundua material nzuri za programming online baada ya kumaliza kanmumbas college na kuichukia programming.

Nadhani kama una nia ,muda , internet na muongozo( mwalimu vitabu video). Cha mwisho baada ya hayo yote ni kujaribu na kufanya coding kwa language yeyote.
 

Naunga mkono hoja lakini kwa maoni yangu graduate wa CS ana basics nzuri sana za software development, tatizo mi naliona linahusu industry nzima sio tu hao wanafunzi.

Kwenye Software development life cycle (SDLC) kuna mambo huwa hatutilii maanani aidha kwa kuepuka gharama ama kukosa wataalamu au vyote, watu wengi wanakazania hatua ya implementation na maintenance ndio maana tunashindwa kutengeneza commercial Software. Kila hatua katika SDLC inahitaji timu ya kufanikisha majukumu ya hiyo hatua, hapa ndio unakutana na tatizo maana kama requirements analysis haijafanyika kwa kina kazi zinazofuata zote hazitaenda sawa sababu plan yenyewe haiko sawa.

Udhaifu mwingine ni documentation, bila hili inakuwa vigumu sana ku enhance product yako maana huwezi kumbuka kila ulichokifanya kama hakijaandikwa na inakuwa vigumu kazi hiyo kuendelezwa na mtu mwingine kama wahusika wa mwanzo hawapo. Software hata iwe nzuri kiasi gani yenye ufanisi wa hali ya juu kwa mtumiaji kama haiko well documented haitakubalika kuwa kwenye kiwango cha kimataifa.

Mi naona kufanikisha vitu kama hivi inahitaji investment kubwa kwenye suala la kuwa na wataalamu wa kutosha na uwezo wa kuwahudumia mda wote ambao wanakuwa jikoni kutengeneza System. Ukifuata hatua zote na kufanya kazi iliyo kwenye standard ya kimataifa inatumia mda mrefu sana na hapa ndio napoona watu wanakimbia gharama.

Pia kwa upande wa programmers wetu inabidi kujizoesha kufuata utaratibu rasmi maana hata mini-projects ndogo tu watu wanalipua, ni mara chache sana utakuta kwenye project za wanafunzi wanaweka comments kwenye codes.

Tubadilike haya mambo yanawezekana jamani.
 
Ukitaka kuwa programmer mzuri inabidi uwe unaandika codes kila siku kwa muda wa miaka 10. Au ujifunze algorithims na uwe unacode kila siku for 2years!
 

Hii ni myth kwenye programming, kuwa unatakiwa kujua hesabu kuweza kuprogram. Of corse kuna sector za programming utahitaji hesabu lakini ni minority na hesabu hizo ni very specific ambazo mara nyingi unaweza kujifunza kama utazihitaji, vectors kwenye 3D kwa mfano.

Kwa kifupi 99% ya programming usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hesabu.
 


Umeongea point nzuri sana
kila sku naongelea hii kitu,Masharobaro wananiponda tu.ICT kwa bongo ni kwa ajili ya kutafutia kazi tu.hakuna jipya
 
Wachangiaji wote hivi sasa nawapiga gape kubwa sana kwenye software development
 
Hoja hujibiwa kwa hoja. Nimeupenda uchambuzi wako.
 
Chamalama umefikia wapi ktk ndoto yako? Je umeisha master basics zote au bado unajifikiria? Weka mrejesho huu mwaka wa saba sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…